Jeshi la Kenya limetumia busara sana.

PintoG

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2017
Posts
612
Reaction score
732
Dunia ilitarajia leo yangetokea machafuko wakati Odinga akijiapiza kuwa raisi wa watu wa kenya.ilitarajiwa police wa kenya wangezuia na kusababisha umwagikaji wa damu hasa kutokana na umati mkubwa wa watu uliokuwa ukitarajiwa.
Nampongeza Kenyatta kwa kuamua kutulia na kumuacha Odinga afanye alichokusudia bila ya kubugudhiwa na police, hii imeepusha sana umwagikaji wa damu .
Hongereni askali police wa KENYA.
 
Hongera uongozi wa kenyatta, alieona madhara ambayo yangeweza kutokea, kama nguvu zingetumika.. Busara ni moja ya njia muhimu sana ya kuzuia maafa.. Bahati mbaya hatuwezi kulisema hilo kwa Utawala wa hapa..
 
Unajua wakenya ni watu jasiri sana , na kizuri wamempata raisi mwenye akili sana kenyatta ana akili sana na kupenda kushauriwa ndio kunamfanya awe bora zaidi

Na hiyo ndio faida ya kuwa karibu na viongozi wenye akili duniani ni lazima na ww utakuwa msataharabu tu, katumia akili sana kuzuia kumwagika damu

Mwisho wa siku ukweli unabaki pale pale kuwa yeye ndiye raisi halali wa kenya
 
Wale wanajitambua sio wa kupelekeshwa vitu vingine ni busara tu kwani akiapishwa anakunyimia nn usingizi,mwache aapishwe ikulu nyumbani kwake,kule hata maandamano anamaneni na ulinzi mtapewa,mkichoka mrudi home mkalale.
 
Ni jambo kupewa pongezi kwa jeshi la polisi la Kenya,ingelikuwa nchi Fulani ndo ungeliona polisi wanavyotanda mtaani na kuwaua wananchi wasio na hatia.piga tu.
 
Na si tutamuapisha lisu awe rais
 
Jamaa balaa, haikutegemewa kama umati huu ungepata nafasi ya kukutanika uwanja uleule alioapishwa yeye
 
Angekuwa nanihii sasa hivi NASA wangekuwa wanaugulia maumivu ICU
 
Reactions: BAK
Kilichonifurahisha baada ya kuona odinga anajiapisha akakimbia Ethiopia kurudi nyumbani kuhofia odinga asije akaenda ikulu[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Rais Uhuru Kenyatta ni mfano wa kuigwa katika jamii ya viongozi wa kiafrika.

Alichofanya ni kumfanya Raila aonekane kama kituko hivi.
 
Kilichonifurahisha baada ya kuona odinga anajiapisha akakimbia Ethiopia kurudi nyumbani kuhofia odinga asije akaenda ikulu[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Hivi ni "amekimbia" mkutano Na kurudi nyumbani au ni Mkutano umeisha sasa karudi nyumbani?
 

Malizia”Kwa mujibu wa katiba”
 
Hivi KDF hawana shuhuli ya usafi mtaani kama huku kwetu
 
Kwingne wangenunuliwa tuu.... unawanunua mpka wanabaki wachache...
Wanaokataa wape kesi uone kma siku ya kuapisha atakuepo mtu....
Hyo nayo ni busara ya kisukuma..
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…