Jaribio la kumkamata Yoon Suk Yeol, Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani na bunge, limegonga mwamba baada ya polisi na wachunguzi wa rushwa takribani 3,000 kuzuiwa na Jeshi la Korea Kusini
Wanasheria wa Yoon wamesema polisi na wachunguzi wanaojaribu kumkamata Yoon wamevunja sheria kwakuwa waranti yao ya ukamataji ipo kinyume cha sheria na kuapa watawachukulia hatua za kisheria kwa kitendo hicho.
Itakumbukwa Bunge la Korea Kusini lilipiga kura ya kumuondoa Yoon madarakani mwezi December mwaka 2024 baada ya Rais huyo kutangaza sheria ya matumizi ya nguvu ya kijeshi akisema ni kwa ajili ya kulinda Nchi yake dhidi ya vitisho vya vikosi vya kikomunisti vya Korea Kaskazini.
PIA SOMA
- Rasmi, Bunge la South Korea lapiga kura kumuondoa Rais Yoon Suk Yeol madarakani baada ya kutangaza utawala wa kijeshi