Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Jeshi la kujenga Taifa (JKT) limebaini uwepo wa vyeti vya kughushi vinavyotumika na baadhi ya vijana ambao siyo waaminifu kwa lengo la kujipatia ajira katika taasisi na makampuni yanayohitaji watendaji kupitia mafunzo ya jeshi hilo na kusema kitendo hicho ni kosa watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hayo yamesemwa leo Alhamis, Machi 13, 2025 na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala la JKT, Kanali Juma Mrai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Amesema kijana yoyote anayehitaji kupata cheti cha kuhitimu mafunzo ya Jeshi hilo anapaswa kujiunga kwani vijana wamekuwa wakichukuliwa kila mwaka katika makundi yote mawili.
Aidha, Kanali Mrai amesema JKT lipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi na makampuni yote yanayohitaji uhakiki wa vyeti vya JKT kwa watumishi wao waliopitia mafunzo ya JKT.