Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
TFF imethibitisha kuwa wanajeshi wa Madagascar, wamevamia hoteli iliyofikia Taifa Stars huko Antananarivo na kukaa kwenye korido ya vyumba vya wachezaji wakiwa na bunduki kabla ya mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Madagascar. Askari walidai wanataka kuwatoa wachezaji wa Taifa Stars ambao wao wanadai wana maambukizi ya Covid-19.