Jeshi la Magereza lakabidhiwa mbegu za alizeti kilo 500 kwa ajili ya kilimo

Jeshi la Magereza lakabidhiwa mbegu za alizeti kilo 500 kwa ajili ya kilimo

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Jeshi la Magereza lakabidhiwa mbegu za alizeti kilo 500 kwa ajili ya kilimo

Jeshi la Magereza, kupitia Mkuu wa Wilaya ya Geita, limekabidhiwa mbegu za alizeti kilo 500 zitakazotumika kupandwa kwenye shamba lenye ukubwa wa ekari 65.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Martine Shigella, alieleza hayo Machi 4, 2025, katika viwanja vya Gedeco, Halmashauri ya Manispaa ya Geita, ambapo alisema kuwa kupitia mbegu hizo, wanatarajia kubadilisha hali ya uchumi wa wananchi.

Shigella alisisitiza kuwa siyo tu kutegemea uzalishaji wa madini ya dhahabu, bali pia Serikali inaweka jitihada za kuwawezesha wakulima ili wafikie malengo ya kujitoa kwenye umaskini.

Aidha, katika hafla hiyo, zaidi ya tani 50 za alizeti zilitolewa kwa wakulima wa Mkoa wa Geita kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Bi. Irine Makota alieleza kuwa mtaalamu maalum ameteuliwa ili kutoa elimu na kusimamia mchakato wa kilimo cha alizeti kwa wakulima waliokabidhiwa mbegu hizo, kuanzia upandaji hadi mavuno.

 
Back
Top Bottom