Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Wajibu namba Moja wa Jeshi letu la Polisi nchini ni kuwalinda raia na Mali zao.
Sasa inapotokea Jeshi hilo ndilo linalohusika Kwa kiasi kikubwa na kupotea Kwa raia nchini, wananchi wa nchi hii watakosa kuliamini Jeshi lao la Polisi, jambo ambalo ni la hatari kubwa sana.
Siku ya Jana tarehe 14 tulipata taarifa toka Kwa kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Zakaria Bernard, akikiri kuwa Jeshi hilo linamshikilia kada wa Chadema, Kombo Mbwana, kada wa Chadema, huko wilayani Handeni, Mkoani Tanga, Kwa siku 29 mfululizo Kwa makosa ambayo Jeshi hilo linadai kuwa ni makosa ya kutumia vibaya mitandao ya kijamii
Nchi hii inaendeshwa Kwa mujibu wa sheria na tunaambiwa Kwa mujibu wa Katiba ya nchi, hakuna mtu aliye juu ya sheria.
Sasa niwaulize Jeshi la Polisi, ni kwanini wao ndiyo wanafanya kazi kama wako juu ya sheria, Kwa kumshikilia mtuhumiwa Kwa siku 29 mfululizo, badala ya kumfikisha katika chombo Cha Mahakama, kama inavyotakiwa Kwa mujibu wa sheria??
Huyo kada wa Chadema, alishatangazwa na ndugu zake kuwa watu wasiojulikana walimteka siku 29 zilizopita, lakini wao Jeshi la Polisi, wamekuwa wakikana kuwa hawahusiki na kutekwa kwake na Jeshi hilo halina taarifa yoyote kuwa kada huyo anashikiliwa na kituo chochote Cha Polisi Mkoani humo!
Ndugu zake Kombo Mbwana, walivyotembelea vituo mbalimbali vya Polisi Mkoani humo na Jeshi hilo limekuwa liikikana kumshiikilia mtu huyo.
Sasa Kwa Jeshi hilo kukiri kuwa wamekuwa wakimshikilia Kombo Mbwana Kwa siku 29 mfululizo, tafsiri yake ni kuwa, wamekuwa wakitoa taarifa za UWONGO kuwa Jeshi hilo halimshikiliii Kombo Mbwana, wakati wao ndiyo wanamshikilia!
Suala lingine ni kuwa Jeshi hilo pia linatambua kuwa wao siyo chombo kinachopaswa kutoa haki hapa nchini, Bali ni chombo Cha Mahakama pelee ambacho ndicho lkilichppewa haki hiyo Kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Niwaulize tena Jeshi la Polisi nchini, ni kwanini waliendelea kumshiikilia Kombo Mbwana, Kwa zaidi ya masaa 48, ambapo ni kinyume Cha sheria, badala ya kumpeleka mahakamani, ambako ndiko pekee, Katiba ya nchi inasema ndiyo chombo kilichopewa haki hiyo kisheria ya kuhukumu kama raia yeyote amevunja sheria??
Nitoe wito Kwa Rais weru, ambaye pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi na usalama, kulivunja Jeshi hilo na kuliunda upya, kutokana na Jeshi hilo kutoteleleza wajibu wao namba Moja nchini wa kutulinda sisi raia na Mali zetu na kujigeuza kuwa ndiyo adui namba Moja nchini wao kuwa "majambazi" wanaosuka mipango ya kuwateka raia wema hapa nchini!
Pia soma==>>> Boniface Jacob: Kombo amezungushwa mikoa 10 akihojiwa na kuteswa na Polisi kabla ya kurudishwa Tanga