GE2025 Jeshi la Polisi Mbeya limewakamata makada sita wa CHADEMA kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
TAARIFA KWA UMMA
WAFUASI WA CHADEMA WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI MBEYA.​

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewakata wafuasi sita (6) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Rungwe akiwemo Mwenyekiti wa Jimbo la Rungwe Gidion Mwakila kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali ili kupanga na kufanya maandamano ya kuadhimisha siku ya Mashujaa wao kimkoa.

Watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 07.09.2025 saa 06.30 mchana katika Kijiji cha Ndaga Wilaya ya Rungwe wakiwa wamevalia sare za Chama cha Demokrasia na Maendeleo pamoja na mabango huku wakitumia mbinu ya kupita mmoja mmoja kama wanaenda kwenye ibada lengo likiwa ni kufanya maandamano hayo ambayo hayakufuata taratibu za kisheria.

Aidha, uchunguzi unaendelea kukamilishwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kufuatwa.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa viongozi na wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.

Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
 
Bado itafikia hata ukikutana na raifiki zako,mpenzi,jamaa mtaulizwa kama ni CHadema wawa kamate.Hii nchi naona tumefikia patamu
 
Wafanye online meetings! Kwa sababu hawapangi njama.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia makada sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali na kupanga kufanya maandamano.

Maandamano hayo yalipangwa kufanyika jana, Jumapili, Septemba 7, 2025, nchini kote, ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Mashujaa kimkoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, ameliambia Mwananchi Digitali leo, Jumatatu, Septemba 8, 2025, kuwa wafuasi hao walikamatwa katika Kijiji cha Ndaga, Wilaya ya Rungwe, saa 6:30 mchana.

Amesema walikamatwa wakiwa wamevaa sare za Chadema pamoja na mabango, huku wakitumia mbinu ya kupita mtu mmoja mmoja kama wakiwaelekea kwenye ibada.

"Lengo lao lilikuwa ni kufanya maandamano bila kufuata taratibu za kisheria na kupelekea Jeshi la Polisi kuwatia nguvuni," amesema.

Aidha, Kamanda Kuzaga amesema bado wanaendelea na uchunguzi wa kina, na endapo utakapokamilika, hatua za kisheria zitachukuliwa.

Awali, akizungumza na Mwananchi Digitali kwa njia ya simu, Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Hamad Mbeyale, amesema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo katika vyombo vya habari.
 
Jeshi la Polisi Mbeya limewakamata makada sita wa CHADEMA kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali
Kwani hao makada wa Chadema wakifanya mikusanyiko yao policcm na ccm wanapata hasara gani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…