Aprili 29, 2025, kuna baadhi ya Wakimbizi walisababisha taharuki katika Kambi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kuingilia na kutumia mabomu ya machozi kutuliza ghasia.
Mchongo upo hivi, inadaiwa kuna Wakimbizi katika kambi hiyo walikuwa na Himaya yao na utawala wao kiasi cha kuamua kuwa wanauza pombe haramu hadharani.
Wakaonywa na Viongozi wa hapo hawakusikia ikabidi Polisi waingilie, ndio wakaamua kubadili mfumo na kuanza kuuza kwenye nyumba zao.
Wakati mchato huo ukiendelea Polisi wakapata hizo taarifa na kuanzisha msako, ndipo Wakimbizi hao nao wakaamua kuanza kumsaka mtu ambaye walimshuku kuwa anawachoma, huku wakifanya vurugu kadhaa.
Askari Polisi walipofika kuwatuliza, Wakimbizi hao nao wakaanzisha sekeseka ndipo Mabomu ya Machozi yakatumika kuwatuliza ndivyo kama unavyoona hapo kwenye picha.
Jeshi la Polisi halijatoa tamko lolote, tusubiri kuona kinachoendelea.
Ufafanuzi wa Polisi ~ Kigoma: Jeshi la Polisi lawakamawa Wakimbizi 25 na kuwafikisha Mahakamani kwa tuhuma za kufanya vurugu