"Jeshi la Polisi ni "Zimamoto" ya kukamata madereva walevi

"Jeshi la Polisi ni "Zimamoto" ya kukamata madereva walevi

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
"IMEANDIKWA KWENYE MAGAZETI MENGI YA LEO"

Jeshi la Polisi nchini limetangaza msako wa kuwakamata madereva wasiozingatia sheria za barabarani, wanaotumia vilevi, wakiwa wanaendesha magari pamoja na kuwakamata wamiliki wa magari yasiyokuwa na viakisi mwanga

Uamuzi huu wa polisi umekuja ikiwa ni siku chache tu tangu kutokea kwa ajali iliyohusisha magari manne iliyogharamu maisha ya watu 20 wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga ambapo chanzo kikuu kilielezwa kuwa ni kutozingatia sheria sheria za barabarabani, mwendokasi na matumizi ya pombe kabla/wakati wa kuendesha vyombo vya moto.
" Mwisho wa Kunukuu"

Hoja yangu ninayowaomba tujadili ni kwanini nchi hii imeendelea kuwa nchi ya "ZIMAMOTO". Tumekuwa ni watu wa kusubiri jambo litokee, tufanye kampeni na kulipigia kelele kwa wiki kadhaa alafu tunalisahau, kisha tunarudi kwenye maisha yetu ya uzembe ya kila siku.

Jeshi la Polisi linapaswa kuja na mpango mkakati wa muda mrefu wa kushughulikia tatizo la ajali barabarani na sio hizi kampeni za zimamoto. Walikuwa na vipima ulevi lakini hata havitumiki siku hizi na mbaya zaidi hata wakikukuta "tungi", "ukiwapooza kidogo", unaendelea "kupiga kibati kama kawa".

Pia barabara zetu nyingi hazina ubora mzuri na ni nyembamba kwa hiyo Serikali inapaswa kuja na mikakati thabiti kukabiliana na adha hii.
Untitled design.png
 
Back
Top Bottom