Jeshi la rushwa la Zanzibar? (Zanzibar tourist police)

Jeshi la rushwa la Zanzibar? (Zanzibar tourist police)

Democracy999

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2012
Posts
945
Reaction score
189
Hapa Mombasa wanaongelea jeshi lililoundwa Zanzibar linaitwa Zanzibar Tourist Police, kwa Masada wa wawekezaji wa sekta za kitalii. Ila kuna tetesi kuwa wengi wao wanajihusisha na michongo ya kujipatia Chapaa tu! Wengi wao walitolewa katika vikosi vya JKU, KMKM, ambavyo ni vikosi vya jeshi la Zanzibar peke yake. Sasa je hili jeshi jipya ni Tanzania au Zanzibar?

Nasikia wanasuka mchongo na wahuni kuwauzia wazungu bangi halafu wao wanajitokeza na kuwakatamata kisha kwa vitisho hapohapo dola 300 zitamtoka mzungu ili asiende jela, wanagawana kisha usiku au mchana wanajificha ufukweni wakisubiri wenyeji wakitongozana na wazungu halafu wanawakamata na kuhoji vibali vya kutembeza watalii hata ni hapohapo maeneo ya home au hoteli. Wanatishia kuwapelekeni jela kwani wanajua mzungu atazama mifukoni na kupapatua chochote ili akimbie zake hotelini.

Wanaojua zaidi tunaomba mtueleze.
 
Wewe acha kutunga uongo wako kama huna data. Kikubwa hapa unachuki binafsi na hao polisi. Hata kama kuna udhaifu wa mtu mmojammoja ndani ya polisi hao lakini si kama unavyotaka kupotosha hivyo. Fanya uchunguzi uje tena, acha kuleta tetesi hapa............
 
mambo ya wazanzibari watayamaliza wazanzibari wenyewe!
 
Back
Top Bottom