Jeshi la Rwanda kwenda kukomboa miji iliyokuwa chini ya waasi huko msumbiji je ni kutuonyesha ubabe au?

Jeshi la Rwanda kwenda kukomboa miji iliyokuwa chini ya waasi huko msumbiji je ni kutuonyesha ubabe au?

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Nimesikia Jeshi la Rwanda limeenda Msumbiji na limefanikiwa kurejesha miji iliyokuwa imemilikiwa na waasi huko msumbiji ila katika historia kuna ukweli kwamba kuna majeshi yalisha kwenda huko kupambana na waasi bila mafanikio ya kurejesha miji hiyo.

swali ni Je, Rwanda inatupa ujumbe gani sisi wana Africa Mashariki, Sadc, Comesa na nchi zingine jirani na Africa mshariki kwamba ni taifa ndogo ila wana uwezo mkubwa kivita wa kufanya kitu flani kupitia majeshi yao.

Nadhani wana tuelewa kuwa Tanzania, Uganda na Kenya kati ya wengine wengi tumewasoma vizuri kwa hiyo tusiwajaribu.
 
Mkuu sio kila mzozo ni lazima Tanzania iingilie. Nchi yetu imeshasaidia nchi mbali mbali kijeshi na kufanikiwa kuzikomboa nchi hizo kutoka mikononi mwa maadui zao.

Hivi mleta mada hujui ukombozi uliofanywa na nchi yetu katika nchi za kusini kama vile Zimbabwe, Msumbiji, Afrika kusini nk. Je mleta mada haukumbuki tulichokifanya kwa wale waasi wa Comoro waliotaka kumpindua raisi wao, au kile tulichofanya Burundi kumrudisha raisi wa wakati ule hayati Ngurunziza madarakani? haukuona tulivyowachapa M23 kule Congo?

Kifupi ni kwamba Tanzania ilikataa kuingia kijeshi Msumbiji kwa kuhofia wimbi la wakimbizi ambao ungekuwa mzigo kwa nchi. Haujiulizi ni kwanini Rwanda imepeleka wanajeshi wao Msumbiji lkn haikufanya hivyo kwa Congo au Burundi?
 
Mkuu sio kila mzozo ni lazima Tanzania iingilie. Nchi yetu imeshasaidia nchi mbali mbali kijeshi na kufanikiwa kuzikomboa nchi hizo kutoka mikononi mwa maadui zao...
Mimi nimeulizia tu ubabe ambao Rwanda inataka kuonyesha sijazungumzia swala la Tanzania kuweza a kushindwa, Si kweli kwamba Rwanda haikuwa DRC wale waasi wa congo bado wapo, Rwanda ilikuwa na majesh yake Congo toka enzi za Kabila, Rwanda haiwez peleka Majesho Burundi kwa sababu hawaelewani na sio marafiki kivile. kwa hiyo nilitaka kusema Rwanda inaonyesha misuli yake pia huko msumbiji
 
Mimi nimeulizia tu ubabe ambao Rwanda inataka kuonyesha sijazungumzia swala la Tanzania kuweza a kushindwa, Si kweli kwamba Rwanda haikuwa DRC wale waasi wa congo bado wapo...
Inaonyesha misuli? Kwani wanashindania Nini?Rwanda Wana jeshi lao pia huko Central African Republic CAR wamepigana na waasi na kukomboa maeneo mengi ya nchi hio na wanamlinda rais wa nchi hio pia Sasa na huko CAR Wanamtunishia misuli Nani?
 
Rwanda ni kibaraka. Kagame anajaribu kujipendekeza kwa Ufaransa ili wasahau kesi waliyomfungulia kwa kupeleka wanajeshi wake kupambana na raia walioamua kushika silaha kulinda gesi na madini yao dhidi ya wawekezaji wa Ufaransa
 
Mkuu sio kila mzozo ni lazima Tanzania iingilie. Nchi yetu imeshasaidia nchi mbali mbali kijeshi na kufanikiwa kuzikomboa nchi hizo kutoka mikononi mwa maadui zao...
Kwahiyo jw wangeenda msumbiji wakimbizi wangekuja Tz ila rwanda wakienda msumbiji wakimbizi hawata kuja Tanzania? Aisee acha porojo mjomba!

Achana na mziki wa kagame! Jamaaa wanajuacsana guerrila war! Ule mziki wa mozambik unataka watu wanaojua vita za msituni!

Tatizo la watz hudhan jeshi lao ni kila kitu kumbe no!

Halafu vita ya comoro ilikua ni mchezo wa kitoto hakuna vita pale!
 
Rwanda ni kibaraka. Kagame anajaribu kujipendekeza kwa Ufaransa ili wasahau kesi waliyomfungulia kwa kupeleka wanajeshi wake kupambana na raia walioamua kushika silaha kulinda gesi na madini yao dhidi ya wawekezaji wa Ufaransa
Hizi ndio akili za watz!!! Pole gaid wenzio wamepukutishwa
 
Rwanda ni kibaraka. Kagame anajaribu kujipendekeza kwa Ufaransa ili wasahau kesi waliyomfungulia kwa kupeleka wanajeshi wake kupambana na raia walioamua kushika silaha kulinda gesi na madini yao dhidi ya wawekezaji wa Ufaransa
😄😄😄 eti wamfutie kesi? Sio Rais wa France majuzi aliyeenda Kigali kuomba 'msamaha' kwa nchi yake kushiriki kwny genocide 1994? Kagame huyu huyu aliyemfukuza balozi wa Ufaransa Kigali Kama Mbwa leo ajipendekeze kwao?😄😄😄.

Aliwaambia Ufaransa Kama mnasema mnaweza kukamata raia wa Rwanda kwa kigezo kua Ni universal jurisdiction then Nami nitakamata raia wenu kwa makosa ya genocide waliyoyafanya hapa 1994 sababu mmesema hio Ni universal na sio 1 way.Mpk leo Ufaransa haijawahi kukamata hata kuku mmoja kutoka Rwanda achilia mbali kukamata raia wao.

Yaani ktk watu hawamtishagi Kagame basi Ni France na Belgium.
 
Hiyo ni hisia yako mkuu, ila haina ukweli maana kwa msuli wa kijeshi Rwanda hawezi kuishinda Tanzania.
 
[emoji1][emoji1][emoji1] eti wamfutie kesi? Sio Rais wa France majuzi aliyeenda Kigali kuomba 'msamaha' kwa nchi yake kushiriki kwny genocide 1994? Kagame huyu huyu aliyemfukuza balozi wa Ufaransa Kigali Kama Mbwa leo ajipendekeze kwao....
Huyo hajui kitu ndio watz walivyo
 
France wanailipa Rwanda kwa kupeleka majeshi msumbiji kulinda kiwanda Chao cha gesi ...

Hizo vitu huwez ambiwa
 
😄😄😄 eti wamfutie kesi? Sio Rais wa France majuzi aliyeenda Kigali kuomba 'msamaha' kwa nchi yake kushiriki kwny genocide 1994? Kagame huyu huyu aliyemfukuza balozi wa Ufaransa Kigali Kama Mbwa leo ajipendekeze kwao?😄😄😄.

Aliwaambia Ufaransa Kama mnasema mnaweza kukamata raia wa Rwanda kwa kigezo kua Ni universal jurisdiction then Nami nitakamata raia wenu kwa makosa ya genocide waliyoyafanya hapa 1994 sababu mmesema hio Ni universal na sio 1 way.Mpk leo Ufaransa haijawahi kukamata hata kuku mmoja kutoka Rwanda achilia mbali kukamata raia wao.

Yaani ktk watu hawamtishagi Kagame basi Ni France na Belgium.
Yaan ufaransa imuogope Rwanda emu toa ngada zako jamaa
 
Kwahiyo jw wangeenda msumbiji wakimbizi wangekuja Tz ila rwanda wakienda msumbiji wakimbizi hawata kuja Tz!?? Aisee acha porojo mjomba!!! Achana na mziki wa kagame !!! Jamaaa wanajuacsana guerrila war!!! Ule mziki wa mozambik unataka watu wanaojua vita za msituni!!!
Tatizo la watz hudhan jeshi lao ni kila kitu kumbe no!!!
Halafu vita ya comoro ilikua ni mchezo wa kitoto hakuna vita pale !!!!
Jeshi letu makomando wao wanateswa na polisisiemu lipo kimya[emoji16][emoji16]
 
Siyo mbaya na wao wakifanya mazoezi ya kivita. Kwa nchi kama Tanzania masuala ya kukomboa miji iliyochukuliwa na waasi tushafanya mission nyingi tuu uganda,congo , comoro tulimuondoa kanali Mohamed bakari kama unakumbuka kwahiyo siyo mbaya na wao wakijenga uzoefu hapo msumbiji.
 
Mimi nimeulizia tu ubabe ambao Rwanda inataka kuonyesha sijazungumzia swala la Tanzania kuweza a kushindwa, Si kweli kwamba Rwanda haikuwa DRC wale waasi wa congo bado wapo, Rwanda ilikuwa na majesh yake Congo toka enzi za Kabila, Rwanda haiwez peleka Majesho Burundi kwa sababu hawaelewani na sio marafiki kivile. kwa hiyo nilitaka kusema Rwanda inaonyesha misuli yake pia huko msumbiji
Sasa rwanda imeonesha ubabe gani au ulitaka ishindwe kuwaondoa hao waasi huko msumbiji? Sijakuelewa
 
Back
Top Bottom