Jeshi la Uhamiaji wamenirudisha Nyumbani wakidai sipo Fiti. Nimepoteza dira ya maisha

Dada yetu pia naomba nikushauri jambo,Kama unahisi uliwahi kuwakosea wazazi wako au kama Kuna jambo unahisi waliwahi kusikitika,naomba sana uende kuwaomba Radhi/Kaa nao waombe Radhi pia...Mzazi/Wazazi ni Mungu wa pili
Hizi ni changamoto za kawaida kwenye maisha.. hapo anaimarishwa kiimani...mbona wengi wameshuhudia humu kama yeye na wapo vizuri kwa sasa....... Usimtishe mtu hivi aanze kuwaza vingine. Atavuka kama wengine.
 
Sijasoma saaaaaaana maelezo yako ila mshukuru mungu kwa kila jambo namana ungepata huko huku huyo mtoto babaake naye anamuhitaji bila shaka ungekuwa na dharau kwake hata kupelekea kuchinjwa TENGENEZA mgahawa uuze
Kama ungesoma ungeelewa zaidi... Kama ada ya mtoto analipa yeye baba wa mtoto yuko wapi.... Usiingilie sana mambo ya watu toa ushauri kwa ulicho ombwa ....kwahiyo bora hajapata ajira kwakuwa angekuwa na dharau??? Kuwa na utu basi.
 
Kuwa na Mtoto ndo kilichomuondoa na si vinginevyo,
Pili; Tukiachana na hii habari ya upande wa dada,Jeshini hawaanini majibu kutoka hospital nyingine na ndio maan hata kama umepimwa wapi lazima na wao wachukue vipimo vyao,
Na vipimo vyao wanachukua muda wanaotaka wao na ndio maan kuna mtu amesema aliachishwa mafunzo akiwa amekwishatumikia miezi mitatu,
Cha mhimu usikate tamaa,endelea kupambana hata na biashara ndogo ndogo na usione aibu kumrudisha Mtoto st kayumba
 
Dada mifumo ya hii nchi ni migumu sana Suala la kwenda cjui bungeni, mara kuandika barua kwenda makao makuu au kwa waziri masauni ni kupoteza tu muda wako, Bora tu ukae utulie kwanza na ajira ikija ije kweny mashirika au nje ya nchi ama uwaze tu jinsi ya kupata hela ufanye biashara zako basi mambo mengine ni kupoteza tu muda wako, usijutie sana kutokupata hiyo nafasi huwez jua kesho yako ikoje
 
Yah ni kweli mkuu, nashukuru sana...
 
Pole sana dada kwenye hizo kazi ukiwa mafunzoni unaweza kurudishwa kama utakutwa na mimba, magonjwa ya zinaa au changamoto zingine za kiafya na Mara nyingi huwa hawakuelezi una tatizo gani hapo ndo huwa inawaumiza watu zaidi.
ila usijali hiyo haikua rizki yako, endelea kupambana ipo siku utapata neema zaidi
 
Pole sasa lakini Hongera kwa mwandiko mzuri.
 
Kwanza usikate tamaa kwasababu you deserve the best.... every thing happen for a reason.
Apply kazi zilizotangazwa jana na tamisemi.
Programu uliyosomea mi nadhani inauhitaji sana huwezi ukakosa sehemu ya part time.
Jiunge kwenye makundi ya ajira mtandaoni huwezi kosa
 
CV imeshiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…