Jeshi la Uhamiaji wamenirudisha Nyumbani wakidai sipo Fiti. Nimepoteza dira ya maisha

Unfit kwa sababu walivyokupima waliona maziwa yako yalishanyonyesha tayari pia tumbo lako lilikuwa linaonesha limetoka kwenye uzazi tayari pole sana usikate tamaa....


Ishu yako inanikumbusha usaili wa TPDF mwaka 2013 pale JKT Oljoro kuna binti alikuwa amezaa tena watoto wa wili tayari lkn kwa kuwa alikuwa anatia huruma na maisha magumu mtaani nilimuombea yule binti kwa matron mmoja ivi ambae yy ndo alikuwa anajua mwanamke aliezaa huyu matron ndo alikuwa anawafanyia usaili hawa kurutu wa kike kwenye vipimo vya afya pia huyu matron nilingiaga nae jeshini mwaka 2001 kipindi iko..


Kwa kuwa tulikuwa tuna heshimiana akanielewa akampitisha yule binti ukupata tuu mtu sahihi hapo ungepita mbona vzr tuu ila pole sana


Rudi uraiani upambane wenda Mungu kuna jambo amekuepusha nalo pole sana usikate tamaaa...
 
Asante nashukuru sana mkuu
 
Imekuwaje sio raia mbona makubwa imagine mtu ka hustle miezi yote hyo loh
We acha tu kaka! kwanza walipiga jkt mwaka 1 na nusu wakachukuliwa kwenye ujenzi wa ikulu dodoma na mjomba magu akawahakikishia ajira moja kwamoja, baada ya magu kufariki wakaona issue yao ya kuajiliwa inapotezewa hakun kiongozi yyte anazungumzia kuhusu ajira zao ikabid waende moja kwa moja kwa mabeyo kuulizia kuhusu ajira zao wakainekana wameenda kinyume na taratibu za jeshi kwamba wameandamana wakarudishwa nyumbani wote walikuwa kama 1004 huvi! Baada ya kuhustle kitaani ndipo wakarudishwa tena wakapelekwa kambi ya jkt mafinga, wamekaa pale miezi 3 ndipo mwakajan mwezi wa 3 wakapelekwa msata, wamekaa mbka mwaka huu mwezi wa 3 wakatolewa 150 kwamba ni unfit na broo wangu akiwemo
 
Maisha ni vita

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana hio situation ilishawahi nikuta wakati nmemaliza chuo nilikuwa na baba yangu mkubwa alikuwa na cheo polisi yeye alishawafanyia mipango wanae wote na watoto wa ndugu zake kibao tu na hata ilipofika zamu yangu ilikuwa ni uhakika lakini nilijikuta nakosa nafasi kiukweli nililia sana hio siku na kujiona ni mtu mwnye mikosi dunia nzima.. Lakini kumbe wakat binadamu tunapanga Mungu siku zote hutuwazia mema juu ya maisha na hatma yetu.. nilikuja kugundua baadae baada ya miezi 3 mbele mpango mwingne kufunguka...

Usikate tamaa! Mshukuru Mungu kwa afya njema
 
Pole kwa changamoto za maisha...

Usiache kujaribu kutafuta nafasi za kazi kwani fani uliyosomea nafasi huwa zatoka mara kwa mara kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali...

Nimeona una uzoefu mzuri tu ikiwepo kuitumikia NIMR...
 
Mbona hyo unfit Huwa ni njia ya kupinguza watu huko na marafiki walirudishwa wazima wengine ni wajeda ila nao wajifunze utu sio kusumbua wengine kisaikolojia na hao waliogoma kipindi Cha jiwe wengi hawajatoboa kabisa. Ila maisha ni kupambana tu na Kila likuepukalo Lina heri
 
Kwa kuongezea pia, ungeainisha kiwango cha msaada unaouhitaji...mathalani ungeainisha kwamba ukifanikiwa kupata milioni 1, basi utaweza kuhuisha biashara zako n.k
 
Kwani kuzaa au kunyonyesha dhambi, mhhh vitu vingine havifai vipi wanaume wao waliozaa au vile hawana ushahidi, inasikitisha mno
 
 
Amen nashukuru sana mkuu,
 
Pole kwa changamoto za maisha...

Usiache kujaribu kutafuta nafasi za kazi kwani fani uliyosomea nafasi huwa zatoka mara kwa mara kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali...

Nimeona una uzoefu mzuri tu ikiwepo kuitumikia NIMR...
Nashukuru sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…