Jeshi la Uhamiaji wamenirudisha Nyumbani wakidai sipo Fiti. Nimepoteza dira ya maisha

Kwa nini hukuwasikiana na huyo bwana aliyekufanyia mchongo wa kupata nafasi uhamiaji huenda anazo mbinu za kukuvusha
 
Yes imagine mfadhaiko watu wanaoupata saa ingine ni excuse ya kuweka watu wao why waache mtu ashaingia Hadi kambini, then mumutoe mara unfit mara vile inasikitisha sana.
Yeah, ni kuweka watu wao, Rushwa everywhere
 
“Pesa niliopata kiasi nikatumia kumtumia alionisaidia kupata nafasi “

Pole sana ila hiyo sentensi hukupaswa kuiandika imeharibu maana nzima ya malalmiko yako, inawezekana sasa kuondolewa kwako kukatetewa na point hiyo kwamba au ulipata nafasi kwa njia isiyo sahihi.

Mungu akufanyie wepesi na akujalie kila lililoheri zaid ya hili
 
Pole sana aisee kwa mtihani mkubwa unaopitia. Kwa maelezo yako fani yako hasa ni huko kwenye research na tayari una uzoefu mkubwa. Sijajua ni kwa nini hasa uliamua kwenda huko Police/uhamiaji kwa sababu naona hata kama ungebahatisha ingekuwa imekutoa kwenye profession yako. Pengine ulifanya hivyo ili upate tuu hiyo kazi na kamshahara but in a long run ingekutoa kabisa kwenye fani yako. Jambo lingine ambalo lilikupotezea focus ni kuamua kuiuza biashara yako ili uende chuo. Kwa ninavyojua changamoto za kifedha ukiwa chuoni hiyo biashara ilikuwa utafute namna ya kuiebdesha ili pia ikusaidie kipindi uko chuo. Mimi nilipoenda chuoni, tena miaka 3 sikuuza biashara yangu bali niliingia ubia na jamaa yangu biashara ikawa inaendelea. Ushauri wangu: tafuta haraka sana sehemu ya kujitolea aidha kwenye taasisi za utafiti au maabara ili kwanza utoke ndani na ujichanganye na wenzako kuliko kujifungia ndani. Pili kwa wewe mdada, na uzoefu ulionao, tena kwenye tafiti, it's a matter of time utarudi kwenye mstari na sooner or later hiyo changamoto yako itabaki historia tuu. Once again pole sana, but take it from me hiyo changamoto itapita na utarudi kwenye mstari, toka ndani haraka acha kujutia makosa ingia mtaani.
 
Amen nashukuru sana mkuu,
Nimesoma uzi wako nakwambia usilalamike wala usikate tamaa kabisa. Mwenyezi Mungu inawezekana anataka uwe mfanyabiashara na sio Mfanyakazi wa serikali. Tuliza akili jipange tena rudi kwenye biashara kuna siku utaleta uzi hapa ukisema UNASHUKURU KUONDOLEWA KWENYE HII AJIRA. Endelea kumuomba Mungu akupe baraka zake tu
 
Asante nashukuru sana mkuu, ushauri nimeupokea
 
Amen Amen nashukuru sana mkuu
 
Amen Amen nashukuru sana mkuu
Ushauri mwengine usikae ndani toka nje randaranda mitaani angalia shida za watu walio kuzunguka. Shida yao mtaji kwako mfano ulipo nunua majani ya Alizeti jaribu kuchukuwa mali kauli kwao halafu rudisha hela yao. Leo watakupa gunia moja kesho magunia matano hii ndio njia ya kunyanyuka, tafakari wapi pa kuanzia au jaribu kuongea na mzee/ndugu au rafiki wanaweza kukupa muongozo mzuri zaidi. Wazee wengi wanajua wapi watoto wao wapo vizuri zaidi
 
pole sana nimejisikia vibaya ila kukosa nafasi mwenue saili yoyote iwe kampuni au serikalini ni moja ya changamoto za kidunia wengi tulishapitia huko
Muhimu mtangulize Mungu kwake kila jambo linawezekana
 
Shahada ya kwanza, maabara ya sayansi, mnashughulika na nini hasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…