Jeshi la Uhamiaji wamenirudisha Nyumbani wakidai sipo Fiti. Nimepoteza dira ya maisha

Pole na masaibu yalokupata.

Ushauri wangu kwako.

1. Endelea kuwasiliana na miradi ulokuwa ukifanya nayo kazi maana huenda wakahitaji mtu na wewe tayati walifany akazi nawe hawatosita kukuchukua tena.

2. Hata kama mradi upo nje ya nchi hiyo ndo njia ya kufungua fursa zaidi kwako kupata midadi mingine kama ya UNICEF na mingine inoshughulika na fani yako.

3. Jaribu kuwa wafuatilia nafasi za kusoma zaidi khasa programs za masters ambazo hutoa scholarships kama hii hapa: Top 10 Best UK Scholarships for Women in STEM. Tembelea pale British Council na ulizia hizi scholarships wana taarifa zote.
Ukiwa na masters na una hiyo kazi umefanya tayari wewe tayari ni expert mzuri na pengine ukaongeza zaidi na zaidi hadi phd.

4. Ukipata tena kazi *kupitia namba 1 au 2 basi endeleza duka lako na mteue mtu asimamie hivyo kuwa na "Disposable income" na ile ya kuweka akiba hata kama ni kiduchu.

5. Mwache mtoto asome mahala pamoja na si kumzungurusha na kumchanganya ingawa hiyo haiwezi kuwa sababu ya yeye kushinda kufeli. Hivyo kama shule aliopo ni nzuri mwache asome hapo.

6. Kwa jinsi ulivyojieleza weye ni mtu wa kufanya kazi sehemu nzuri yenye malipo ya maana hivyo usikate tamaa na jikite katika kufanya tafiti wapi utapata kazi nzuri.

7. Mshirikishe mzee maana bado mna mtoto ambae hajaanza kujitegemea hivyo nae msaada wake wahitajika, ingawa yategemea na mazingira ya kweye kuwa na mwanao kama SP.

Kazi za miradi ya nje zina mishahara na marupurupu mazuri sana na waweza kujipangia kabisa ustaafu baada ya miaka mingapi, hivyo usiwatupe mkono waajiri wako wa zamani, wasumbue kwa emails na charts za whatsapp.

Kila la kheri.
 
Nimepokea ushauri, nashukuru sana Mkuu, be blessed
 
Sijasoma saaaaaaana maelezo yako ila mshukuru mungu kwa kila jambo namana ungepata huko huku huyo mtoto babaake naye anamuhitaji bila shaka ungekuwa na dharau kwake hata kupelekea kuchinjwa TENGENEZA mgahawa uuze
 
Hizi Ajira zinatoka PDF hadharani,huwezi ukauzuia watu kuona....Kama ipo na ipo tu..
Huyu ndugu yetu yawezekana Mungu hakupanga awe UT,Riziki yake ipo mahali pengine.Naimani huu mwaka hauishi atakuja na ushuhuda humu wa mambo yake kufanikiwa.
Riziki hipo kwa kila mtu kikubwa uvumilivu na kuomba mungu, ajira za afya zimetangazwa kikubwa kutokukata tamaa.
 
Kuzaa kweli hawachukui, na walioolewa yaani ndoa, mi nafikilia huyu mpendwa kasema Kama kazaa, au Ile nimemkumbuka mtoto wangu, habari zimefika ngazi ya juu, kawaambia watu hapo mafunzoni, sababu Kuna marafiki zetu wameingia majeshini na walizaa na ndoa zao, Ila walivyojiunga mafunzo walificha Siri, Sasa hivi maaskari kitambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…