Stunnaman008
JF-Expert Member
- Nov 17, 2022
- 238
- 272
Mtu mmoja ameuawa huku wengine zaidi ya 10 wakijeruhiwa baada ya mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel kushindwa kutungua shambulio la ndege isiyo na rubani (droni) lililofanywa na jeshi la Yemen dhidi ya mji wa bandari wa Jaffa (Yafa) unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel, viungani mwa Tel Aviv.
Msemaji wa Jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema vikosi vya nchi hiyo vimeshambulia Tel Aviv kwa kutumia droni mpya iliyopewa jina la 'Jaffa' na kuongeza kuwa, "Tel Aviv sio eneo salama tena kwa kuwa hivi sasa ipo ndani ya shabaha ya silaha za Wayemen."
Amesema droni ya Jaffa ina uwezo mkubwa wa kukwepa mfumo wa ulinzi wa anga, na hakuna mfumo wowote wa rada unaweza kuigundua. "Sasa tutajikiti katika kushambulia maeneo ya ndani kabisa mjini Tel Aviv," ameongeza Msemaji wa Jeshi la Yemen.
Saree amesisitiza kuwa, wanajeshi wa Yemen wataendelea na operesheni zao za kijeshi, kwa kushambulia kwa makombora na droni maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, na kuzuia meli zinazomilikiwa na Israel au zile zinazoelekea katika bandari zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu, hadi pale usitishaji vita wa kudumu utakapotekelezwa katika Ukanda wa Gaza.
Msemaji wa Jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimekiri kutokea mashambulio hayo na kusema kwamba, operesheni hiyo ya leo alfajiri imezusha hofu na wasiwasi miongoni mwa maafisa na walowezi wa Kizayuni mjini Tel Aviv.
Haya yanajiri siku moja baada ya ndege za madola vamizi ya Marekani na Uingereza kufanya mashambulizi matatu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa al Hudaidah, magharibi mwa Yemen, kama sehemu ya kuwaunga mkono Wazayuni.
Operesheni hizo za majeshi ya Yemen za kuwaunga mkono wananchi madhulumu Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, zimekuwa na mafanikio makubwa na zinaendelea kuisababishia Israel hasara zisizo na kifani.