BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka Mkoa wa Kagera limethibitisha kuwa Ndege ya Shirika la Precision Air imepata ajali na kuanguka kwenye Ziwa Victoria wakati ikijaribu kutua na tukio hilo ni kweli.
Zimamoto zimekanusha taarifa za uvumi kuwa ndege hiyo imeangushwa kwa majaribio ya mazoezi ya utayari wa kukabili majanga na kutaka taarifa hizo zipuuzwe.
Kamanda Msaidizi wa kikosi hicho akizungumza na Clouds FM amesema ajali hiyo imetokea leo saa 2 asubuhi wakati ndege hili iliposhindwa kutua na kuingia ziwani kutokana na hali mbaya ya hewa.
Pia amesema watu 25 wameshaokolewa na zoezi linaendelea. Taarifa za madhara zitatolewa baada ya kukamilika kwa zoezi lote.