SoC04 Jeshi la Zimamoto na uokoaji lipatiwe vifaa vya kisasa ili kukabiliana na majanga ya moto katika misitu,maeneo yasiyo fikika na majengo marefu

Tanzania Tuitakayo competition threads

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
UTANGULIZI.
Majanga ya moto ni miongoni mwa majanga ambayo hayatabiriki na huleta athari kubwa sana katika jamii kama vile watu kupoteza maisha na mali,kwa Tanzania majanga mengi ya moto yamekuwa yakileta maafa makubwa kipindi yanapotokea hii nikutokana na sababu mbalimbali ikiwepo ukosefu wa vifaa vya kisasa.

Majengo marefu,maeneo yasiyo fikika kiurahisi na misitu mikubwa ni miongoni mwa maeneo ambayo yana athirika sana pale moto unapozuka.


Msitu wa Mlima kilimanjaro ukiwaka moto. Chanzo:BBC


Zipo sababu nyingi zinazopelekea maeneo haya kuathirika zaidi pindi janga la moto linapotokea,miongoni mwa sababu hizo ni kukosekana kwa vifaa kisasa vya kupambana na moto,Pia kukosekana kwa mifumo ya kisasa ya kufuatilia viashiria vya uwepo wamoto katika misitu na hifadhi mbalimbali ili kuukabili mapema.


Askari wa JWTZ na kikosi cha zima moto wakizima moto kwa kutumia rack pamoja na matawi ya miti katika msitu wa mlima kilimanjaro. Chanzo: BBC

VIFAA NA MIFUMO YA KISASA INAYOHITAJIKA.
Vifuatavyo ni baadhi ya vifaa vya kisasa vinavyohitajika ili kugundua uwepo wa moto katika hatua za awali kabisa na kukabiliana na moto;

Ndege nyuki (Drones)
Hizi ni ndege ndogo zinazo ongozwa na rubani kwa kutumia rimoti na nyingine huweza kubeba mtu mmoja ili kuiongoza ndege na kufanya maamuzi,lakini nyingi ni zile ambazo rubani wake hutumia rimoti,ndege hizi hutumia akili bandia inayowezesha kugundua uwepo wa moto kwa kutumia sensa mbalimbali kama vile kamera na sensa ya moshi na kuonesha uelekeo ambao moshi hutokea ama mwanga wa moto hutokea ili kugundua sehemu sahihi ambayo moto umeanzia.

Ndege hizi kwa upande wa majanga ya moto zimegawanyika katika makundi mawil ambayo ni;

Ndege gunduzi au tafiti za majanga moto.
Ndege hizi kazi yake kubwa ni kufuatilia uwepo wa vishiria vya majanga ya moto,hutumia kamera pamoja na sensa ya moshi ili kugundua uwepo ama viashiria vya moto kwa kuona mwanga wa moto pamoja na kuhisi moshi kisha kufuatilia sehemu sahihi ambayo moshi ama mwanga unatokea ili kugundua sehemu sahihi ambapo moto unatokea,hutumika katika misitu mikubwa na hifadhi mbalimbali.

Ndege hizi hutumia GPS ili kuonesha kwa usahihi zaidi sehemu ambayo moto umeanzia,zipo kubwa na ndogo.


Ndege ndogo tafiti chanzo cha moto.Chanzo:shutter stock

Ndege zimishi moto.
Ndege hizi jukumu lake kuu ni kukabiliana na zoezi zima la kupambana na moto kwa kuuzima baada ya ndege tafiti kutambua uwepo wa chanzo cha moto na wataalam wa kukabiliana na moto huzitumi hizi kwenda kuzima moto,nazo pia hutumia kamera na sensa ili kujua sehemu sahihi ambayo ni kitovu cha moto.

Ukubwa wa ndege hizi hutegemeana na ukubwa wa moto unaotakiwa kukabiliwa,aina ya kizimishi inachobeba,na ukubwa wa tanki la kizimishi inalobeba kama inabidi,kuna zinazotumia maji,gesi ya kabonidaiyoksaidi,zile zinazotumia teknolojia ya moto kuzima moto ,na vizimishi vingine.

Ndege nyuki ikiwa katika majukumu ya kuzima moto msituni. Chanzo:Shutterstock

Ndege zinazotumia kabonidaioksaidi kama kizimishi moto huwa na mitungi ya gesi ambayo Hutumika kuhifadhi gesi hiyo,baada ya kuona sehemu ambayo moto umeanzia rubani huvunja kizuizi cha gesi ili kuruhusu gesi kutoka kwa kutumia rimoti yake lakini pia kuna ambazo zinajivunja kizuizi zenyewe baada ya kuona kitovu cha moto.


Ndege nyuki ndogo zikiwa zimebeba mtungi wa gesi zikikabiliana na moto. Chanzo Daily beast.com

Ndege zinazotumia maji hizi hazibebi maji isipokuwa zinategemea maji yaliyohifadhiwa kwenye tanki katika gari maalumu la kuzimia moto au chanzo kikubwa cha maji kama moto,bwawa ama ziwa,ndege hizi zina pampu ambayo husaidia kuvuta maji kwa msaada wa mpira wa maji kutoka chanzo cha maji kilicho jirani.

Hutumika kuzima moto katika majengo marefu na hata sehemu ambazo ni ngumu kwa gari ya zima moto kufika,pia hutumika kuzima moto katika misitu ambayo inavyanzo vya maji jirani


Ndege nyuki ikizima moto katika jengo refu kwa kutumia maji yanayopandishwa kwa msaada wa mpira .Chanzo: shutter stock

Ndege zinazotumia maji ili kukabiliana na moto katika majengo marefu au sehemu ambazo ni ngumu kwa gari kufika huwa zinakuwa na magari yake maalumu ambayo yanatumika kuzibeba mpaka eneo la tukio ama jirani na eneo la tukio ambapo hutolewa kwa katika sehemu yake ya kuhifadhia kwa kutumia rimoti,hutumia maji yaliyhifadhiwa katika tanki la gari lake lakini pia inaweza kufungwa katika chanzo kingine cha maji.

Gari ya zimamoto iliyobeba ndege nyuki.Chanzo: Commercialfirefightingequipmeants.com

Ndege hizi zinztofautiana pia katika umbali zinazoweza kusafiri pasipo kupoteza mawasiliano ambapo umbali mdogo zaidi ni kilomita kumi na zaidi hufika kilomita za mraba elfu kumi na zaidi.

Teknolojia ya IGNIS.
Mbali na aina hizo zilizoelezewa hapo juu,kuna aina nyingine ambayo ni ya kisasa zaidi ijulikanayo kama “IGNIS Amplified technology”ambayo hutumia moto kuzima moto,katika teknolojia hii ndege nyuki hubeba mtambo ambao unabeba vimipira vidogo mithili ya “Ping pong balls” ambavyo huachiwa na kulipuka kusababisha moto wa kawaida ilikuunguza sehemu maalumu na kuzimwa.


Ndege nyuki ikiwa imepakia vimipira tayari kwa misheni.Chanzo:IGNIS TECHNOLOGY

Vimipira hivi hudondoshwa katika mtirirko maalumu na ndege hudondosha vimipira 30 kwa dakika na hubeba vimipira 150 kwa mara moja.


Muonekano wanamna vimipira vilivyodondoshwa katika mstari mnyofu na kuwaka.Chanzo: IGNIS TECHNOLOGY.

Teknolojia hii Hutumika maeneo ambayo tayari moto umekuwa Mkubwa na hakuna vyanzo mbadala vya kukabiliana na moto huo,hivyo njia pekee ni kuukabili moto ni kwa kuondoa vitu vinavyo shika moto kama vile nyasi na vinginevyo kwa kuviteketeza haraka ili moto ukifika ushindwe kuendelea maeneo ambayo hayajashika moto .

Maeneo ya misitu na hifadhi,serikali haitakuwa na budi kujenga vituo vya kuendeshea Ndeje hizi kwa kuzingatia umbali ambao ndege watakazozinunua zitakuwa na uwezo wa kusafiri ili kuhakikisha kwamba maeneo yote yanachunguzwa ili kujikinga na majanga ya moto.

HITIMISHO.
Vifaa hivi vina gharama lakini faida zake ni nyingi na muhimu kwani husaidia kugundua majanga ya moto mapema,huwezesha kuukabili moto mapema,husaidi kuzimamoto kwa haraka na kuepusha maafa makubwa.
 
Upvote 2
Amaa kweli hivi vinauishi ule msemo wa dawa ya moto ni moto.

HITIMISHO.
Vifaa hivi vina gharama lakini faida zake ni nyingi na muhimu kwani husaidia kugundua majanga ya moto mapema,huwezesha kuukabili moto mapema kabla hausambaa,husaidi kuzimamoto kwa haraka na kuepusha maafa makubwa.
Nimejifunza vitu. Ndegenyuki ni nomaa
 
Ni jeshi pekee lisilo na kikosi maalum, jeshi wana MP, Polisi FFU, Magereza wana kikosi cha kuzuia ghasia magerezani. Hawa hawana kikosi maalum cha kuzima moto au uokoaji. Walau kiwe na watu 500 nchi nzima, au hata 300 ambao wanaweza kuwa deployed sehemu yoyote ya nchi kwa muda mfupi
 
Linaitwa jeshi la uokoaji na zima moto,lina vikosi pia kama kikosi cha zima moto,kikosi cha uokoaji majanga asilia,kikosi cha uokoaji majini,tatizo hakuna usanifu kazi katika vikosi vyote,pia kuna uhaba wa watumishi kwa 60%,na hawana vifaa vya kisasa.
 
Sasa Mkuu wa kikosi aunde kikosi maalum chenye mchanganyiko wa hao uliowataja, kwa kuwa ana uhaba wa watumishi, atie hao hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…