Rais Kikwete athibitisha Tanzania iko salama
Na Zaina Malongo
RAIS Jakaya Kikwete amewataka wananchi wasiwe na waziwasi kuhusu usalama wan chi kwa sababu jeshi lina zana na silaha za kisasa ambazo zitaliwezesha kukabiliana na adui.
Aliyasema hayo jana alipotembelea maonyesho ya kumbukumbu ya miaka 45 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yanayofanyika katika eneo la uwanja wa ndege wa jeshi, Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete alisema kuwa nchi ipo salama na ina vifaa vya kisasa na kulipongeza jeshi kwa kuandaa maonyesho hayo ili kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi yake.
Nimefurahi kuona vifaa hivi vinafanya kazi hapa. Inanaonyesha ni jinsi gani maonyesho yaliyovyoandaliwa na nina amini wananchi wamejifunza mengi dhini ya maonyesho haya na kuona kuwa jeshi letu linavyfanya kazi, alisema.
Rais Kikwete alielezwa kwamba jeshi linamiliki ndege zenye uwezo wa kuruka zaidi ya umbali wa kilomita 2,000, 1,800 na 800 kwa saa.
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kwamba katika mkakati endelevu wa miaka 15 ijayo, jeshi litaongeza zaidi zana za kisasa ambazo zinaendana na teknolojia ya sasa.
Msemaji wa jeshi, Mbota Mwikambo alisema tangu maonyesho yaanze Agosti 26, wananchi zaidi ya 800 wameyatembelea na kujifunza mambo mbalimbali.
Maonyesho hayo, alisema yanaandamana na huduma za bure za afya kwa wananchi.
Wagonjwa wa dharura 403 walipata huduma mbalimbali za tiba, wengine kupima virusi vya ukimwi na miongoni kujitolea damu kwa ajili ya kutunisha benki ya damu nchini.
Source: Mwananchi