Jeshi nchini Burkina Faso latangaza kurejesha Katiba

Jeshi nchini Burkina Faso latangaza kurejesha Katiba

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jeshi la Burkina Faso limetangaza kurejesha katiba, wiki moja baada ya kutwaa mamlaka katika taifa la ukanda wa Sahel. Tangazo hilo limetolewa katikati mwa mazungumzo baina yake na wapatanishi wa kimataifa.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ghana ambaye anaongoza ujumbe wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS Shirley Ayorkor Botchway, amesema mazungumzo ya mjini Ouagadougou na viongozi wa kijeshi "yalikuwa ya kweli" na kwamba viongozi wa kijeshi walionekana kuyapokea mapendekezo yaliyotolewa, akiitaja kuwa ishara nzuri. Mjumbe huyo amekutana na kiongozi wa mapinduzi Luteni kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba na wanachama wengine wa jeshi.

"Burkina Faso sasa ni mwanachama aliyesimamishwa, ECOWAS bado itaendelea kufanya kazi na Burkina Faso. Mapambano, hali ya usalama, ni mambo yanayoathiri Afrika Magharibi nzima na hata nje ya Afrika Magharibi, kuelekea Afrika ya Kati. Na hivyo sisi hatutoiacha Burkina Faso peke yake, tutaendelea kushirikiana na Burkina Faso kupambana na tishio hili la ugaidi, migogoro ya silaha na kadhalika. Kwa hiyo tutafanya kazi na utawala mpya."

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Afrika Magharibi na ukanda wa Sahel UNOWAS, Mahamat Saleh Annadif ambaye pia ameyataja kuwa yenye matumaini.

Juhudi hizo za mazungumzo zinakuja muda mfupi baada ya Umoja wa Afrika kusimamisha uanachama wa Burkina Faso kufuatia mapinduzi ya Januari 24. ECOWAS nayo ilisimamisha uanachama wa taifa hilo tangu siku ya Ijumaa na kuonya juu ya uwezekano wa vikwazo kulingana na matokeo ya mazungumzo na viongozi wa kijeshi.

Mapema siku ya Jumatatu, katika taarifa iliyotolewa kupitia televisheni, jeshi lilitangaza kuwa limeidhinisha "kitendo cha msingi" kinachoondoa kufutwa kwa katiba. Jeshi hilo, limelitaja rasmi Vuguvugu la Wazalendo la MPSR kuwa litaendelea kuhakikisha utulivu wa nchi likisubiri kuanzishwa kwa kipindi cha mpito. Hata hivyo halikutoa muda wa kipindi hicho, lakini limemtambua kamanda wa kijeshi Damiba kuwa rais wa MPSR na kiongozi mkuu wa kijeshi.Jeshi Burkina Faso lakemewa licha ya uungwaji mkono
 
West Africa naona wameanza kuchoka na hizi demokrasia mfu, zenye kulinda corruption. Waafrika tujifunze kutumikia umma wakati tumepewa madaraka.
Ukiona mwenzako ananyolewa.....
 
Kwa hiyo hao wanajeshi ndio watatumikia umma? 😆😆😆😆
Ukimwaga ugali na mwenzako akamwaga mboga unafikiri nini kitaendelea? Turudi kwenye uhalisia...uongozi mbovu ndio unazaa matatizo yote tuliyo nayo kwenye bara hili.
Tusiendelee kujificha kwenye kivuli cha demokrasia wakati uhalisia ni kuibia wananchi mali zao kwa kutumia madaraka tuliyopewa. Wanajeshi nao ni sehemu ya raia hao.
 
Hujajibu swali langu,hao wanajeshi ndio wataleta utawala Bora?
 
Mapinduzi huwa na thamani tu pale mamlaka ya nchi yanaporejeshwa kwa wananchi. Tofauti na hapo, ni upuuzi mtupu!
 
Hujajibu swali langu,hao wanajeshi ndio wataleta utawala Bora?
Sio lazima? Inategemea wana agenda gani na kama wana uchungu huo mkubwa kwa nchi yao. The source is corruption of the democratic leaders.
Halafu, kama democratic leaders don't care, why do you think the army generals will care?
 
Kwa.hiyo maisha sasa ya wa Bukinabe ni mazuri sio? 🤣🤣
 
Back
Top Bottom