Huyu mdosi ameonyesha jeuli sana, nilipokuwa nafanyakazi Ngara kwa wakimbizi kuna visa viwili vilitakea; Muitaliano mmoja wa kampuni iliyo kuwa inajenga barabara ya lami inayokwenda Bujumbula alikuwa anakiburi na kunyanyasa wafanyakazi, sikumoja alimfanyia kitu mbaya jamaa yetu mmoja, yule jamaa akaenda polisi huyo mdosi alipoitwa akafanya jeuli, FFU walimfuata walimleta kituoni kwa kwa mguu akiwa peku alipewa masaa 24 na mkuu wa wilaya awe ametoweka nchini aliondoka. Kulikuwa pia na Mjelumani mmoja naye alileta jeuli ya kunyanyasa watu na kutukana hata viongozi wkija viongozi wa serikali ofisini kwake ana wafukuza, naye alipewa 24hrs aondoke aliondoka. Aliyekuwa anawapa 24hrs ni mkuu wa wilaya tu, Sasa huyu kaonyesha dharau kubwa kwa bunge serikali na Watanzania kwa ujumla. Kwa kweli huyo jamaa wa hotel ya VIP ashikishwe adabu liwe funzo. Mnasemaje washikadau