Jezi za Taifa Stars hazivutii

Jezi za Taifa Stars hazivutii

Jafar

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2006
Posts
1,136
Reaction score
54
Kama kuna mtu ambaye amedizaini jezi za taifa stars basi mtu huyu ni bomu hajui dizainingi. Jezi za stars ziko hivi:

1. Fulana za buluu zina mistari miwili mieusi mabegani iliyoanzia karibu na kola kuishia mikononi
2. Kuna nembo ya TFF kifuani (ndogo) mkono wa kushoto ina rangi nyeupe
3. Kuna nembo ya bendera ya taifa (ndogo) kifuani mkono wa kulia
4. Fulana ina michirizi ya kijani kila upande wa ubavu
5. Chupi /bukta nyeusi zenye mchirizi wa njano karibu na pindo la chini
6. Soksi rangi ya daki-buluu na upapi mweupe juu kidogo ya enka
7. Golikipa fulana ya dhambarau

Hivi kwa nini wasichague rangi moja au mbili tu. Napendekeza rangi ya buluu, maana ndiyo alama ya muungano (bahari). Hii mpangilio wa rangi kwenye jezi unanikera sana. Afrika ya Kusini walianza na ujinga huo huo baada ya ubaguzi lakini leo wamebakia na rangi mbili tu. Kama kuna mtu aliye karibu na TFF naomba anifikishie ujumbe wangu.
 
Uzuri wa jezi hauna maana katika soka. Cha msingi ni uzuri wa timu na wachezaji wenyewe. Mfano mzuri ni zile jezi ya Ujerumani Magaharibi katika kombe la dunia la 1990 au za Argentina, Inter Milan, AC Milan na Juventus, jezi mbaya ila kutokana na makali ya timu zenyewe zinaheshimika mpaka leo.
 
Pamoja na kwamba ubaya au uzuri wa jezi taste ya mtu, nadhani weusi/giza limezidi sana kwenye jezi. Na rangi si lazima ziwe za bendera ya taifa.
 
Nakubaliana nawe kabisa Jezi za Tz stars ni MBAYA MBAYA MBAYA KABISA wala hazivutii. Kuna rafiki yangu wa nchi fulani alishawahi kuniambia kuwa jezi zetu si nzuri so it is true hazivutiii kabisa. Hata mimi nashauri zibadilishwe. Kwani hata sisi wapenzi kuzivaa ni taabu kweli kweli .. mirangi lukuki kama nini.
 
Sasa basi wekeni dizaini hapa halafu tuifanyie mpango wa kuiwakilisha kwa wahusika.
 
Back
Top Bottom