Jezi za Taifa Stars zimeangalia maslahi ya Yanga

Mbegu ya utengano iliyopandwa katika Taifa inaota kwa kasi sana.

Kama si Yanga na Simba basi CCM na Chadema. Kama si Ukristo na Uisilamu basi Uzanzibari na Utanganyika. Kama si Uchaga na usukuma basi ni mwanaume wa Dar na wa Mkoani.

Wakuu tusipoangalia kuna bomu kubwa sana linatunyemelea.

Hii ni kitu kidogo sana mkuu, hukupaswa hata kupeleka mawazo yako kwenye uYanga na uSimba.
 
Sijawahi kupenda rangi ya blue katika jezi zetu za taifa. Kwanza mimi ni mnazi ya Simba (Mimi ni Kilomoni Jr.) ila ahuweni tutumie rangi hizi mbili (kijani na njano) au kama tunatumia blue basi iwe kwenye soksi ama bukta na iwe blue ya kukoza kama ile ya Brazil.

Fulana zikiwa kijani zitaleta muonekano mzuri sana na iwe kijani ya kukoza sana na bukta ndizo ziwe za blue.

Mwisho: kwa aina ya wachezaji wetu hata ukiwapa jezi za dhahabu ni sawa na kipini cha dhahabu juu ya pua ya nguruwe.

Wapeni tu hayo hayo majezi mabaya yanayoendana na uchezaji wao wa hovyo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…