ng`wana ong`wa kulwa
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 2,420
- 1,752
- Thread starter
-
- #21
Kuna sababu kadhaa zinazifanya uchangiaji upungue,
1. Umakini wa mada.
2. Kutokujieleza vizuri kwa waleta mada.
3. Kutorudisha majibu/maendeleo ya msaada uliotolewa.
4. Kujirudia rudia kwa tatizo/mada ile ile.
1. Umakini wa mada.
- Hapa mada italetwa ikiwa ya mzaha, kukejeli n.k wakati kuna jukwaa husika (Utani, Udaku, n.k).Hii hufanya jukwaa kupoteza hadhi yake, mvuto kwa sababu, wachangiaji makini wa jukwaa hili hili utawakuta kule Jukwaa la siasa, Intelligence, Great thinkers forums!
2. Kutokujieleza vizuri kwa waleta mada.
Kuna vitu kadhaa ni lazima kuvieleza, inawezekana daktari haviulizi mkiwa pamoja kwani anakuona, lakini katika mazingira ya kutoa ushauri katika jukwaa vitu kama Jinsia, Uzito, Umri, n.k ni muhimu sana hivi husaidia katika dozi ya dawa/kupanua wigo wa ufikiri zaidi wa tatizo n.k.
3. Kutorudisha majibu/maendeleo kwa msaada unaotolewa.
Wakati mwingine, wanajukwaa hutoa msaada hasa pale msaada unapohitajika kwa kuonana mf. Namba za simu za madaktari, watoa huduma za afya, n.k lakini watu hawaleti maendeleo ya walipofikia, hii hufanya watu kukosa moya wa kufanya hivyo mara nyingine.
4. Kujirudia rudia kwa mada ile ile.
Ninatambua magonjwa ni yale yale lakini yaweza kujitokeza kwa namna mbalimbali, lakini wakati fulani mada inayoletwa ni ile ile, yaani mf, Tatizo la Fangasi (Fungi),mada hii italetwa leo, kesho, siku inayofuata n.k Sasa iwapo tungekuwa tunajaribu kusoma mada ya ugonjwa tunaotaka kuuleta jukwaani kabla ya kuandika, angalau hata kwa ku-search, ingesaidia.
Hivyo basi mkuu ng'wana ong'wa kulwa , tukijirekebisha kwa mambo hayo na mengine mengi, jukwaa litarudi katila hadhi yake.
hippocratessocrates za siku mkuu siku nyingi nimekumiss hapa, mchango wako mzuri nakumbuka vema,mambo ya msingi umeyaeleza kwa kweli ni juu yetu wadau kuyafanyia kazi.Karibu sana mkuu.