TBL (haya majina mengine na ijumaa hii mtatufanya tutoroke kazini)...pamoja na majibu mazuri ya dada King'asti, ningependa kuongezea kama ifuatavyo:Mbu anapokuuma huwa anatoa hayo 'mate' ili kufanya damu isigande wakati akifaidi kuinyonya, haya mate ndio huwa yanabeba vijidudu vya malaria (Plasmodium) hivyo akiyatoa kwenye damu yako anakuambukiza. Na vijidudu hivi vya malaria vinafika kwenye hayo mate kwa sababu mbu anapofyonza damu ya mtu mwenye malaria, vile vijidudu katika hali ya mbegu vikifika tumboni, hupenya ukuta wa tumbo na kudevelop kuwa katika hali ya kuweza kushambulia chembe chembe nyekundu za damu. Vikishadevelop ndio vinakuwa katika matezi ya mate ya mbu huyo kusubiri anapouma ili vimwagwe kwenye damu na kusababisha malaria.Virusi vya HIV havidevelop kwenye tumbo la mbu, wala havifiki kwenye matezi ya mate ya mbu...hivyo mbu akiuma mtu mwenye HIV, virus wale hufika kwenye tumbo la mbu na kuishia hapo. Na hivyo...mbu hawezi kuambukiza HIV.[/QUOTEchezea DK.RIWA ww!!!