Jf ilinikutanisha na tapeli wa mapenzi

Nakadori

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
8,778
Reaction score
21,010
Wakuu, heshima mbele,

Najuta sana kumtafuta partner humu JF yani pamejaa usanii hapa usipokuwa mjanja kama mimi unalizwa hivi hivi unajiona.


Kipindi kile nilikuja na swala la kutafuta mchumba hapa, kweli huyo aliyejidai mchumba alipatikana bada ya kuchuja chuja na kufanya trial and error. kumbe mchumba hakuwa mchumba bali tapeli wa mapenzi tu. mkasa ulikuwa hivi....... jamaa alisema yuko single na mara ya mwisho kuwa na msichana ni mwaka mmoja uliopita.baada ya kuchat sana kupitia mtandao huu wa JF na email ilibidi tupeane mawasiliano ya simu, na majina ya facebook account. Ukweli mawasiliano yalikuwa hot sana. Simu zilikuwa hazikauki, meseji ndo dahhh siwezi sema, kutwa kuchwa ni kuchat na kupena meseji za mahaba. Ila kwenye facebook friend list yake ilikuwa imefungwa huwezi ona nani ni rafiki yake na huwezi post kwenye wall yake pia.

Basi, sisi tukiwa kwenye mapenzi motomoto na kuliwazana (ila sikuwa mwepesi kutoa tundi ndio ninachoshukuru na kujivunia) kumbe jamaa ana girlfriend wake wa long mie sikujua, basi siku moja niliona friend request ya mdada mmoja hata simjui ameni-add mie bila hiyana kabla ya kumu-accept nikawa natumiana nae inbox kujua ni nani na ni wawapi.....bi dada akaniambia nimuadd kwa faida yangu, ila akawa anadadisi sana kuhusu mahusiano yangu ya kimapenzi, sikuwa muwazi sana hadi aliponitajia jina la facebook la huyu kiumbe tulokutana JF. Huyu binti alisema yeye na huyu fisadi wa mapenzi ni wachumba wa long time ila yeye anafanya kazi mkoani huwa anakuja dsm mara chache sana. Nilimuuliza kuhusu uthibitisho ili niamini maneno yake then alinitumia hadi ushahidi wa pics ambazo sio za kawaida yani za mitego mitego ya kimapenzi zinazoonesha wako na mahusiano live (picha zilionesha hata dates za muda wa karibuni), kuforwad emails za huyu kiumbe wanazotumiana kila leo za kimapenzi n.k.

Ukweli baada ya hayo yote hasira zilinipanda ila nikazituliza nikapata ujasiri wa kumuomba kijana anipishe tugawane ustaarabu. kijana alisita huku akisistiza nimwambie why, mie nikamwambia nimeona siwezi match nae, yeye akawa anasisitiza bado ni mapema mie ku conclude hivyo. Nilipoona anasisitiza nikamwambia live kwamba ana msichana mwingine hivyo ni bora nimpe nafasi ili apumue vizuri! Kijana alibisha hadi leo hii.., pamoja na kumforwadia emails zake lakini wapi bado anakataa.

Hili tukio nimeona nililete ili kuwaasa wasichana wenzangu na hata kaka zangu ambao nao wako kwenye process ya kuisaka ndoa wawe makini sana. mimi kwa hili naweza sema ni Mungu ameniokoa kwani nilikuwa ninaelekea mbali na kuzamia kabisa! huwa nimefikiria ilikuwaje huyu dada akanijua kupitia facebook? au alipewa password na hyu kaka? hapana Mungu aliamua kunionesha na kuniokoa.

Wanawake wenzangu na kaka zangu tumuombe sana Mungu ili atupatie wanaume na wanawake wa ukweli na sio matapeli.

Mbarkiwe sana.
 
Ahsanteni sana @Lizzy na Mwali. huko ndio kujifunza, kumbuka sipochafuka atajifunzaje? japo inauma sana tena sana pale mtu anapoamua kudanganya sijui ni kwa nia gani.
 
duh nimebaki naduwaa.....huyo dada amejuaje kuwa unataka kuanzisha mahusiano na huyo kaka mpaka akufuate???.......lol pole lakini....mie nahisi ungemtaja humu tumjue...NAME AND SHAME HIM????????????????........kazi kuvizia tu humu hana haya loh,ukute kashawadanganya kibao kwa gia ya ndoa....mmmmmmnh......
 

Mama kiu ya ndoa mama. unaweza kujikuta unaparamamia gume gume lililoshindikana na mitume yote. umakini unahitajika
 
Chunga sana, kuna kisa kililetwa juzijuzi na mwana JF wa zamani kuhusu haya mapenzi ya kwenye mtandao kumbe mtu alikuwa unausambaza UKIMWI makusudi kabisa. Pole.

FF ninaomba link ya hicho kisa nami nikisome?
 
Ahsanteni sana @Lizzy na Mwali. huko ndio kujifunza, kumbuka sipochafuka atajifunzaje? japo inauma sana tena sana pale mtu anapoamua kudanganya sijui ni kwa nia gani.
Mtandao ni sehemu ya kukutana tu kama barabarani,
huwezi kuanzisha mahusiano kwa kupitia mtandao.
Lazima mvuke mtandao na mjuane katika maisha ya kawaida kwa muda kwanza
alafu ndio uamue kuanza mahusiano ya kimapenzi.
 
Nakadori pole kwa yalitokukuta. Huwa nawaona watu wako bussy na marafiki wa mtandao. To be honest kwa sisi wengine marafiki hawa huwa ni for leisure only, kwa lengo la kukutana na kufurahia maisha tuu na sikutarajia if it can get that serious!.

Pia sometime you can take chances with your heart by listening to your heart your inner self will always warn you kuwa hiyo relationship siyo ila wengi huwa wabishi na wakishaigia mtegoni yakawakuta ya kuwakuta ndipo macho yao hufunguka!.
 
duh kazi kwelikweli..ulishawahi kukutana nae jamaa na kuongea nae uso kwa uso?huyo dada unayesema ni mchumba wa jamaa yeye vipi hana wivu/hajachukia ulipomwambia kuwa jamaa anakutokea?isije ikawa ni kweli siyo wapenzi,ila huyo dada anataka kukuharibia tu?
najaribu kuangalia upande wa pili wa shilingi!
 
Naky jamani pole... Hilo lijamaa ungelianika hapa tulisute..

Kongosho mambo?
Nimeota umenletea zawadi nikaogopa kuifungua sijui bomu!
 
Mitandao ni mibaya sana katika mahusiano,especially facebuk,unakuta mwanaume au mwanamke ana zaidi ya wanawake au wanaume 6 kwa fb,kila mmoja anampromise mambo kedekede,siku ya siku ikifika kujulikana mwenza mkuu ni nani,jamaa au mdada anaanza kudata,mwishon wote wanakukimbia unabak mtupu,hujui nani wa kuoa ama kuolewa nae.
Pole sana dada,kuwa makin na watu kama hao.
 
Hapo kwenye kiu ndo tatizo. Kiu ya kila kitu itaishia kuponza.
Usitoke JF dada, nataka nikutapeli gari ama nyumba kama unayo, nahamia pm usinitose mwaya eh
Mama kiu ya ndoa mama. unaweza kujikuta unaparamamia gume gume lililoshindikana na mitume yote. umakini unahitajika
 
Pole sana kwa mkasa uliokumbana nao Nakadori. Ni vizuri kuwa makini na hii mitandao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…