Jf ilinikutanisha na tapeli wa mapenzi


Pole kwa yaliyokukuta, na bahati yako kupata ufunulio kabla mambo hayajaharibika, vinginevyo ungejuta kuzaliwa na kuona aibu hata kutamka hadharani kama unavyofanya leo. Majuto ni mjukuu.

Kwa namna nyingine nakupongeza kwa kuwa na uvumilivu na subira ambayo imekuepusha katika janga lililojificha ndani ya ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu mkali. Hata hivyo halijaharibika neno kwa kuwa tunajifunza kutokana na makosa. Jipe moyo Mungu yuko upande wako, soon atakufunulia lililojema zaidi kwako.

Nakupongeza kwa kutoa tahadhari kwetu sote. Mimi na wenzetu wengi tumetahadharishwa vya kutosha.
 
Mkome kutafuta wachumba kwenye mitandao kwani mtaani hamuonekani???

Humu ni usanii tu
 

nimependa ulivyo ... you seem to be wise and confident ... usikate tamaa, vuta subira na enenda taratibu; utampata atakaye kupenda kwa dhati ... amini kuwa yupo ... ni suala la muda tu!
 

Na wa siwasi na wewe unaweza ukawa ndyo mlengwa hapa mbona unakuwa mkali.
 
Hata wanawake nao hivyo hivyo wengi wao unakuta mwanamke anawanaume zaidi ya mmoja na anawapanga kama foleni ya ATM za NMB na hawajuani

ngoja nicheke kwanza:lol: ni bora tuseme binadamu hatuaminiki hakuna cha mwanamke wala mwanaume, hapo ni kuomba Mungu akufungie ni kweli wapo wenye kuolewa wakianzia mahusiano humu humu mitandaoni ingawa ni wachache , wanaolizwa ni wengi na sio wanawake tu, hata wanaume wameshalizwa sana tu.
 
Reactions: Sal
Pole Nakadori, mitandao hasa hii ya kijamii haifai, hebu cheki hii video Clip uone jamaa alivyokutana na Jini mtandaoni
hahahaaaaaaaaaaaaaa.... sasa hii si avatar tu ajamni??

aisee kumbe tuko mbali aisee, LOL
 
Last edited by a moderator:

Nakubali kabisa wapo wanaume matapeli lakini huu ushahidi aliotoa mtoa mada haudhibitishi kama kweli amedanganywa kwani ana uhakika gani kuwa alieyemletea email ni mwanamke fake na kwamba huyo ndiye aliyemzidi maarifa kwa kumdanganya ni wachumba. nasema hivi kwa sababu mazingira amabayo huyu dada amemfahamu mtoa mada hayako wazi na kuna kila dalili kuwa amezidiwa maarifa na mwanamke mwenzake.
 

Linaweza kuwepo tatizo la mchujo, sasa kabla hajakaa sawa huyo mwanaume alikuwa bado katika kukusanya kwa ajili ya mchujo, na kumbe waliokusanywa tayari walishaanza kutambua kwamba wako members hivyo kuamua kumlipua jamaa. Hilo nalo ni tatizo na pengine ni kuchezea nafsi za watu. Hili si kwa wanaume tu hata wanawake lipo sana.

Mfano mtu anayepangisha nyumba au kuuza nyumba kwa mtindo wa mnada ni kutesa watu kwa vile kila anayekwenda anakuwa na lengo la kununua, matokea mwenye mkono mrefu wa kufikia pale juu ndiye anaychukua. Wakati mwingine dau lake likipita kiwango kurudisha chini huwa si utaratibu na hivyo hufikia mnada wake kukosa mteja.

Deal nzuri kuna baadhi ya malandlord ambao akishatangaza tena anayekuja na kumwamini basi anaamua kudeal naye kuona kama ana vigezo anavyovitaka, kama hafii basi anamtolea nje na kumkaribisha mwingine hadi anampata mwenye kiango anachotaka.

Wazungu wansema fanya kitu kimoja kwa wakati mmoja hadi kikamilike, lakini vyote kwa mkupuo utakuja kushuhudia hakuna kilichokamilika, ni viporo tu. Kwa hoja yangu hii mwanamke au mwanaume asipokuwa na utaratibu huu anaweza shtukia anaachwa solemba na miaka inazidi kukatika na kushtukia anaangukia ambapo wengi wanamshangaa kana kwamba ni kanyagaboya. Haya mambo ndo hivyo, tunapeana mawazo ya kuwa wa kweli na wawazi ndio maisha mazuri.
 
Mkome kutafuta wachumba kwenye mitandao kwani mtaani hamuonekani???

Humu ni usanii tu

Aliyekwambia mtaani ndio kuna malaika/watakatifu ni nani?kila mahali kuna mapretender wa ajabu na mafisadi wa mapenzi.
Cha msingi mtumaini Mungu wako kwa moyo wako wote wala usizitumainie akili zako(source: Proverb in the Bible).
 
Pole sana ndugu, huyu usanii mwingi. Kuna watu wana tabia chafu ila mtandaoni wanapenda kujionesha ni watakatifu, wengine ni micharuko mitandaoni kiasi kwamba huogopwa na watu ila katika maisha yao hukuta ni wapole na wastaarabu sana. Kuwa makini hata na watu unaojenga nao urafiki wa kawaida.
 
Yeye akasambaze huko kwa wasojua kama kuna ukimwi, biashara ya ku-do bila ndom mbona ishapitwa na wakati siku nyingi. vinginevyo, tukapime. na nikikuhisi utulivu bado, ndom inarudi.

Chunga sana, kuna kisa kililetwa juzijuzi na mwana JF wa zamani kuhusu haya mapenzi ya kwenye mtandao kumbe mtu alikuwa unausambaza UKIMWI makusudi kabisa. Pole.
 
pole sana mdada shukuru Mungu amekuepusha, Muombe Mungu atakupatia aliye wa kwako
 
the only advice to men and women.... Be careful, most of social network love is just nothing more than a waste

this is true. Jamani mimi nimejaribu several times haya malovee ya kwenye social forums. Almost 99% ni usanii. Ushauri wangu kwa wale ambao wako serious na kutafuta wapenzi wapige magoti wamwombe mungu watafanikiwa tu. Other altenatives are very complicated and contradictory.

Kumbukeni kwamba ndoa ilianzishwa na mungu katika bustani ya eden kwa ajili ya utukufu wake. Mkono wa shetani ndio ulioingia kuvuruga mpango huu mtakatifu wa mungu. Ndiyo maana yote hayo yanatokea.

Baada ya dhambi wanadamu tulianguka na hatukuweza wala hatuna uwezo wa kujiokoa wenyewe mikononi mwa shetani bali tunahitaji uongozi wa mungu.

Mwomba munu hachoki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…