Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Juma pili hii tar 20.10.2025, zoezi la kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi muhimu sana na wa kihistoria wa serikali za mitaa na vijiji Tanzania, litahitimishwa rasmi nchi nzima.
Kama mzalendo na kiongozi mwenye heshima wa familia hii pana ya JF, natoa wito na kuwarai wadau wote humu jukwaani, kuchukua hatua za makusudi, kujitolea na kuwajibika kizalendo, kwenda kujiandikisha na hatimae kushiriki katika zoezi la maamuzi la kupiga kura ili kuchagua wale watakaofaa kuongoza na kushughulika na changamoto mbalimbali za kijamii, kisiasa na kiuchumi katika maeneo tunapoishi.
Platform hii maalumu kama oversight team katika mambo mbalimbali nchini, imesaidia pakubwa sana kuchochea mageuzi na mabadiliko katika mambo mengi sana humu nchini. Hivyo basi ni muhimu sana, sote kama wadau wa kuchochea mabadiliko, kua sehemu ya mchakato huu muhimu kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa ili kua na haki, hoja Lakini pia fursa pana zaidi ya kushauri na kukosoa pale inapobidi badala ya kulalamika au kuzira pekee. Tuisaidie nchi yetu kwa vitendo.
Tututumie vizuri sehemu ya muda mfupi wa siku tatu zilizobaki na kua sehemu ya wapiga kura wa kihistoria Tanzania Nov 27, 2024.
Mungu Ibariki Tanzania