Elections 2010 JF mmejiandaa kwa hili?

Kituko

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2009
Posts
9,555
Reaction score
9,357
kutokana na mwenendo wa kiasasa unavyoelekea kuna kila dalili ya wizi wa kura kutokea, na kwa kipindi hichi kifupi habari za njama hizo ya wizi zimekuwa zikilipotiwa humu (JF), kwanza na baadae kwenda sehemu zingine,

kwa maana hiyo JF inaonekana ni kama kituo muhimu cha kupatia info zote muhimu na ni ukweli ulio wazi kuwa matokeo mengi yatawasilishwa humu kwanza na jumla sahihi ya kura za uraisi inaweza kupatikana humu (kwa kujumlisha kura za vituo vyote), na hili linajulikana na hao wachakachuaji na sidhani kama watakuwa tayari kwa idadi/jumla ya kura za uraisi zijulikane na mtu mwingine yoyote kabla ya wao (wachakachuaji) hawajajumlisha, MAANA JK ALISEMA HAPO KWENYE JUMLA NDIPO WANAPOWEZA KUFANYA UHUNI WAO

hofu yangu kubwa ni JF kuhujumiwa wakati huu wa kusubiri matokeo 31Oct mpaka 3Nov, MODs na wengineo wanaohusika, MMEJIANDAA KWA HILI?
 
Giv me a break
 
Pamoja na kuwa sheria hairuhusu kutangaza matokeo, lakini tunaweza kupata provision results hapahapa kwa kila kituo Tanzania nzima, hii itaweza kusaidia kutuweka sawa kirecords
 
Pamoja na kuwa sheria hairuhusu kutangaza matokeo, lakini tunaweza kupata provision results hapahapa kwa kila kituo Tanzania nzima, hii itaweza kusaidia kutuweka sawa kirecords

tatizo mtandao hautahujumiwa?
 
Pamoja na kuwa sheria hairuhusu kutangaza matokeo, lakini tunaweza kupata provision results hapahapa kwa kila kituo Tanzania nzima, hii itaweza kusaidia kutuweka sawa kirecords

Ni sheria gani hiyo ambayo inazuia kutangaza matokeo? Hakuna sheria kama hiyo, kinachokatazwa ni kutangaza mshindi, kazi ambayo hufanya na NEC tu.

Matokeo yote yanabandikwa ukutani na hivyo mtu yeyote anaweza kuya kopi na kuweka sehemu yoyote.

Ila msije mkaletewa matokeo fake na mkaanza kushangilia ushindi ambao haupo.
 
Ni kweli hujuma inaweza kutokea ili jamvi lisiwe hewani. Mods inabidi wafanye kazi OT ili kuhakikisha kila kitu kiko shwari na pia nadhani kutakuwa na umati mkubwa sana ambao haujawahi kuonekana tangu jamvi lianzishwe.
 
na ndio maana miminilkuwa naona hapa JF, inaweza kuwa ni center nzuri ya kuyapata matokeo ya pande zote, na jumla kujulikana humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…