Jf msaada tafadhali

commited

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,624
Reaction score
871
wakuu heshima kwenu,
tafadhali naomba mnisaidie mambo yafuatayo, nataka kujiajiri katika kutengeza sabuni za kuogea, kufulia na za unga, zitokanazo na mmea wa jatropha, naomba mnisaidie

1, gharama ya mashine ya kukamua mafuta ya alizeti ni sh ngap? Je inauwezo wa kukamua kilo kiasi gani cha mbegu na kwa muda gani?? Kwani nimepata taarifa kuwa hata hiyo mashine ya kukamua alizeti naweza imodifai kidogo ikafaa kukamua mbegu za jatropha kutoa mafuta.

2. Napenda kujua tbs, na tfda wana analyse, kuhakiki bidhaa kama hii kwa tsh ngapi tafadhali anayejua anisaidie wadau ili nazo bidhaa zangu ziwe zimehakikiwa nao


3. Naomba anayejua anisaidie gharama za kudesign na kuprint mabox kama yale ya sabuni za rungu au deto inaweza kukost tsh ngapi kwa kibox kimoja?? Na kama unamjua mtu anayeweza nisaidia kwa maana ya vifungashio ni pm tafadhali


asanteni sana , kila lakheri kwenu
 
Mkuu Hongera kwa hilo,

Ila nilitaka kujua kama Mashine za Alzeti ndo hizo hizo zinazo tumika kukamulia Jatropha,

Ila kama ukoa Arusha Nenda Maeneo ya 88 kuna Kampuni fulani kule ina dili na haya mavitu ya Jatropha, ila mkuu upatikanaji wa Mbegu zake sio mchezo
Ukifika pale kuna kila kitu
1. Majiko special ya kutumia mafuta ya Jatropha

2. Sabuni

3. Majiko special ya kutumia mashudu ya Mbegu za Jatropha

4. Jinsi ya kufanya hayo mafuta yaendeshe engine ya Diseli
 
Mkuu chasha asante sana
 

asante mkuu tupo pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…