JF na makala za Mohamed Said miaka 10 iliyopita

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
JAMII FORUMS NA MAKALA ZA MOHAMED SAID:UKIPENDA KUSOMA HISTORIA YA TANGANYIKA/TANZANIA

''HISTORIA YA UHURU ISIMULIWAVYO NA MOHAMMED SAID YAKOSOLEWA''

Mjadala huo hapo juu katika Jamii Forums ulivunja rekodi kwa kuwa ulidumu kwa miezi sita mfulululizo na ulichangiwa na watu zaidi ya 900,000.

Aliyefungua uzi huu alifanya hivi baada ya kusoma makala zangu za historia ya uhuru wa Tanganyika nikieleza mchango makhsusi uliotolewa na Waislam wa Tanganyika ambazo kwa kweli kwa wengi historia hii ilikuwa mpya kwao.

Katika Makala zangu niliweka picha ambazo ambazo wengi hawakupata kuziona kabla na walisoma mengi ambayo walikuwa hawajapata kusoma wala kusikia kabla.

Wengi waliingia kuchangia kwa kutaka kutafuta ukweli na wako wengi walioingia wameghadhibika wakimuona mwandishi kama ‘’mchochezi’’ na Muislama wa ‘’Siasa Kali.’’

Wako wachache waliingia kuchangia kwa kuniunga mkono na kunipongeza kwa kuandika historia ambayo ilikuwa imepotezwa kwa miaka mingi.

Haya yalitokea sasa imepita karibu miaka 10.

Nina wajibu wa kuishukuru JF kwani wao walichapa kila makala niliyoandika.

JF kwa kufanya hivi ikanijengea jina na watu wengi wakanijua na watu wengi sana wakatambua kuwa kwa miaka mingi sana walikuwa wanasoma historia ya uhuru ambayo ilikuw ana upungufu mkubwa usiolelezeka.

Kwa mchango wangu huu JF wakanitunuku Cheti cha Shukurani na kunizawadia Simu Janja.

Mambo yalikuwa kama hivi:

''...leo hii umesomwa na watu 490, 472 na unaendelea kusomwa daah!!. Kuna huu uzi mwingine unamuhusu Mudeer Mohamed Said, huu ulianzishwa na Mag3 huu umeishasomwa na watu 112, 133 huu bado upo hewani unaweza kuupitia hapa chini kiduchu... Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa...''

Picha: Mexence Melo Mkurugenzi Mkuu wa JF.

1656795622095.png
 
Tatizo hizo historia unaziegemeza sana kwa mudi
 
Safi sana kazi iendelee, ila mi naomba Mohamed Said uandike pia historia ya utumwa Zanzibar ili tuipate na picha pia na huko ilikuwaje
Just...
Historia ya Utumwa ipo soma Cross Atlantic Slave Trade Kisha soma Belgian Congo Slave Trade.

Ukimaliza soma historia ya Utumwa Zanzibar.
Rejea zipo nyingi search Google.
 
JAMII FORUMS NA MAKALA ZA MOHAMED SAID:UKIPENDA KUSOMA HISTORIA YA TANGANYIKA/TANZANIA

''HISTORIA YA UHURU ISIMULIWAVYO NA MOHAMMED SAID YAKOSOLEWA''

Mjadala huo hapo juu katika Jamii Forums ulivunja rekodi kwa kuwa ulidumu kwa miezi sita mfulululizo na ulichangiwa na watu zaidi ya 900,000.

Aliyefungua uzi huu alifanya hivi baada ya kusoma makala zangu za historia ya uhuru wa Tanganyika nikieleza mchango makhsusi uliotolewa na Waislam wa Tanganyika ambazo kwa kweli kwa wengi historia hii ilikuwa mpya kwao.

Katika Makala zangu niliweka picha ambazo ambazo wengi hawakupata kuziona kabla na walisoma mengi ambayo walikuwa hawajapata kusoma wala kusikia kabla.

Wengi waliingia kuchangia kwa kutaka kutafuta ukweli na wako wengi walioingia wameghadhibika wakimuona mwandishi kama ‘’mchochezi’’ na Muislama wa ‘’Siasa Kali.’’

Wako wachache waliingia kuchangia kwa kuniunga mkono na kunipongeza kwa kuandika historia ambayo ilikuwa imepotezwa kwa miaka mingi.

Haya yalitokea sasa imepita karibu miaka 10.

Nina wajibu wa kuishukuru JF kwani wao walichapa kila makala niliyoandika.

JF kwa kufanya hivi ikanijengea jina na watu wengi wakanijua na watu wengi sana wakatambua kuwa kwa miaka mingi sana walikuwa wanasoma historia ya uhuru ambayo ilikuw ana upungufu mkubwa usiolelezeka.

Kwa mchango wangu huu JF wakanitunuku Cheti cha Shukurani na kunizawadia Simu Janja.

Mambo yalikuwa kama hivi:

''...leo hii umesomwa na watu 490, 472 na unaendelea kusomwa daah!!. Kuna huu uzi mwingine unamuhusu Mudeer Mohamed Said, huu ulianzishwa na Mag3 huu umeishasomwa na watu 112, 133 huu bado upo hewani unaweza kuupitia hapa chini kiduchu... Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa...''

Picha: Mexence Melo Mkurugenzi Mkuu wa JF.

View attachment 2279540

Just a certificate!!, where is the simu janja??!
 
Back
Top Bottom