Na mende msafi
(mwandishi hana nia yoyote mbaya, lengo ni kufurahia maisha muda huu ambao vyuma vimekaza)
Tuanze……
Episode 01
mshana jr: (huku akinyoosha kidole upande wa mbele yao) mkuu, kwanza kabisa inabidi tu ulizoee tu hili jina la kuitwa 'mkuu'. Ni jina linalotumika kwa kila mtu ukiwa kule ndani.
mende nsafi: (huku akiwa katika hali ya mshangao) kwa hiyo hata wanawake wanaitwa hivyo hivyo?
mshana jr: (anatabasamu) ndiyo. Tuachane na hilo kwanza. Si unauona huu uzio hapo mbele?
mende msafi: huu wa waya?
mshana jr: ndiyo, huu uzio ulijengwa maalum ili kufanya kuwa watu pekee ambao wataruhusiwa kuingia humo ndani ni wale tu ambao wamesajiliwa na uongozi wa avenue hii ili kupewa kibali cha wao kuweza kuingia ndani na kushiriki shughuli za humu ndani. Na hao unaowaona wanachungulia nje ni wale ambao hawana vibali vya kuingia ndani . na uongozi wa venue hii haukuona busara kujennga ukuta wa tofali ili kuwazuia kabisa kuona kinachoendelea ndani, bali wakaweka hizi waya ili watu wengine waweze kufuatilia japo kwa uchache vitu vinavyoongelewa humu ndani. Na hata mimi nilikuwa nachungulia kama wao ila nikaamua kujisajili.twenzetu tuingie ndani mkuu
Wanapiga hatua huku mgeni akiwa ameyatupa macho yake ndani ya ule uzio. Anaonekana kutabasamu. Wanafika kwenye geti kuu ka kuingilia. Juu limeandikwa “JAMII FORUMS, THE HOME OF GREAT THINKERS” halafu chini ya maandishi hayo pameandikwa “where we dare to talk openly” .
mshana jr: (anamwangalia mende msafi) kwa kuwa wewe hujajisajili bado nenda pale kwenye kile kibanda kilichoandikwa JISAJILI HAPA. Hapo ndo ndo utapata kadi yako ya kudumu ya kuingilia humu.
mende msafi anaenda kukielekea ile kibanda. Baada ya muda kidogo anarudi pale alipo mshana jr
mende msafi: mshana..
mshana jr: niite mkuu, inapendeza zaidi
mende msafi: mkuu, nimeulizwa nataka nitumie utambulisho wa jina halisi au lisilo halisi. Kwani ni vipi hapa mbona kama sielewi.
mshana jr: (huku akitoa kadi yake ya utambulisho kutoka mfukoni) nakushauri usitumie jina lako halisi. Nadhani siku chache zijazo utajua ni kwa nini uliulizwa hilo swali.
mende msafi: (anapeleka kidole chake jichoni kama anasafisha macho) sasa nijiitaje.
mshana jr: mimi sijui
mende msafi anaondoka na kwenda kwenye kibanda cha usajili. Anakaa kidogo anarudi na kadi yake mkononi huku akiwa na furaha.
mende msafi: kumbe process ni fupi hivi, mi nilidhani itachukua siku nzima. Hata dakika haija isha!
mshana jr: jamaa wako smart sana na wanajali muda kwenye hilo swala. Japo kwenye baadhi ya mambo wako slows.
Wanafika kwenye mashine kukagua kadi kabla ya kuingia ndani. mshana jr anamuelekeza jinsi ya kupitisha hiyo hadi naye mende msafi anafanya kama alivyoelekezwa, mlango unafunguka na anaingia ndani. Na mshana jr naye anafanya vivo hivyo. Wanaingia ndani. mshana jr anamwanagalia mende msafi ambaye muda wote macho yake anayepepesa kuangalia kila upande. Kuna majengo mengi yametapakaa mbele yao yote yakiwa na rango ua bluu na nyuepe. Mbele yao kuna watu wanaotembea wakiingia na kutoka katika majengo hayo.
mshana jr: unasikia (anasema mende msafi ili kuvuta makini ya mende msafi) ngoja nianze kukuelekeza kuanzia hapa. Unaona haya majengo yaliyotapakaa humu ndani? Haya ni majengo maalum ambayo mijadala na mada mbali mbali huwa zinajadiliwa. Na na kila jengo lipo maalum kwa ajili ya kujadili kitu maalum na ndiyo maana kama utaweza kuona ni kwamba kila jengo mbele yake limeandikwa. Kwa mfano lile kuleee juu kabisa kule umeliona?(mgeni anatazama upande alioelekezwa) si umeona limeandikwa jukwaa la siasa. Kwa hiyo mule wanaongea mambo ya siasa tu. na ukipeleka mambo ya gigy money sijui nani..utatolewa nduki na matusi juu hadi ukome.( mende msafi anacheka, mshana jr anaendelea baada ya mende msafi kumaliza kucheka) Hili la pembeni yetu ambalo limendikwa chit chat ni kwa ajili ya kupiga dtory tu na washkaji. Na mimi binafsi nalipenda sana.(wanaanza kupiga hatu wakielekea pale jengo hili lilipo. Wakati wakiwa bado wanatembea, mshana jr anaendelea kuongea) unaweza kuingia jengo lolote lile na ukasikiliza na kutoa michango yako katika mada utakazozikuta zinajadiliwa humo ila siyo majengo yote. Kwa mfano kuna moja lipo huku upande wa chini limeandikwa “jukwaa la dini”, kule hauruhusiwi kuingia kama huna kibali maalum. Na kuna jukwaa la wakubwa, hilo hata uzunguke huku kote hutaweza liona jengo lake ila lipo nan i jukwaa la siri kwa sababu mambo yanayoongelewa kule ni ya kiutu uzima sana.
Wanafika katika mlango wa jengo lililoandikwa “chit chat” na kwenye mlango wa jengo hili pamebandikwa karatasi yenye maandishi yanayosomeka “general chat, talk about anything that falls under no category on the board, but rememberFOLLOW THE RULES”. mshana jr anasukuma mlango na wanaingia ndani. mende msafi anashangaa kukuta una kelele nyingi katika chumba kile.
mende msafi: mbona kuna kelele hivi?
mshana jr: aaaah ni jambo la kawaida tu, hata lisikuumize kichwa.
mende msafi; (huku akiangaza macho kila upande) sasa hapa story wanapigaje sasa?
mshana jr: swali zuri. Unaviona hivyo vikundi vikundi? hapo kila kikundi wanapiga story kuhusu jambo tafauti na kikundi kingine. Na ndiyo maana unaona watu wanatembea tembea mara kikundi hiki mara kile kwamba wanataka kupata na kuchangia mawazo katika story tofauti tofauti.
mende msafi: (huku akionyesha uso wa kushangaa) sasa mbona kuna vikundi ni vikubwa na vingine ni vidogo mno?
mshana jr: unajua idadi ya watu katika kikundi Fulani hutegemeana na vitu viwili. Cha kwanza ni umaarufu wa muanzisha story na aina ya story yenyewe. Kwa mfano mtu akiwa maarufu sana hata kama akianzisha story hata kama ni mbaya mbaya watu watamzunguka tu na kumsikiliza na kuchangia.
mende msafi: (anashusha pumzi) umaarufu! Ni nini kinamfanya mtu awe maarufu huma ndani sasa?
mshana jr: humu mtu anaweza kuwa maarufu kwa kupitia ukongwe wake humu, au story zake zinakuwa ni za kuvutia, uzuri au urembo wa sura hii ni kwa upande wa wanawake na hata pia kuna wengine ni maarufu kwa ajili ya story zao za kijingajinga tu.
mende msafi: anhaa na ulisema sijui aina ya sory sijui…
mshana jr: yeah..unajua kuna mada nyingine ambazo zinavutia watu ndio maana utakuta kuna watu wengi (mara yanasikika makofi mengi kutoka katika kikundi chenye watu wengi kuliko chochote mle ndani, mshana jr anageukia upande yalikosokika makofi yale) unaona kama kule, hizo kelele za makofi unazo zisikia ni kwamba kuna jamaa anaitwa Jembekillo alianzisha hiyo kitu kuwa mtu yeyote akienda pale akiongea chochote tu apigiwe makofi, hata kama ni pumba. kwa hiyo hata wewe kama unataka kupigiwa makofi we nenda pale na useme chochote tu, unapigiwa makofi ya kutosha.
mende msafi: (huku akiwa amejawa tabasamu la nguvu) aisee huku kuna mambo ya ajabu na kufurahisha sana.
mshana jr: sanaaa
Inasikika sauti kutoka katika kundi lililopo kwenye kona ya mwisho kulia mwa jeng ikisema “daa huyo mtoto ni balaa.. duniani kuna wanawake wazuri aisee”. mende msafi anageuza shingo yake kuelekea upande huo. anaona watu wakiwa wanaonyeshana vitu kwenye simu zao.
mende msafi: na pale wanafanya nini?
mshana jr: hahaha. pale bwana kuna jamaa anaitwa KakaKiiza alikuja na wazo kuwa wawe wanaonyeshana picha za mademu wazuri. Kwa hiyo kama una picha picha ya mtoto mzuri unaenda pale unawaonyesha basi inakuwa burudani kwao.
mende msafi: (huku akiwa na shauku) daah ngoja niende aisee.
mshana jr: (anacheka) unapenda mademu eeeh?
mende msafi: hapana naenda kucheki kidogo tu.
wakati mgeni anaelekea huko mara napita mtu akiwa anakimbia kwa kasi na kumgonga mende msafi na mende msafi anapepesuka, lakini mtu huyo hasimami wala kugeuka anaendelea kutimua mbio na kuelekea katika moja ya kikundi. mshana jr anamfuata na kumpa mgeni pole.
mende msafi: hivi watu wengine wakoje aisee..anaona kabisa kuna watu wengi humu lakini yeye anakimbiakimbia kama yupo nje!
mshana jr: pole, huyo anaitwa Joseverest, yeye hupenda kuwa kwa kwanza kusikia na kuchangia kila story na ndio maana mara zote huwa anakimbia kimbia ili awe wa kwanza kufuka katika kila story mpya kuliko wengine. (mende msafi anaasama mdomo kwa mshangao) kwa hiyo utaendelea kumwona akikimbia huku na huko, we mzoee tu.
mende msafi: (huku akiwa bado katika mshangao) sasa yeye anafaidika nini?
mshana jr: aah sijui, ila nadhani ni identity yake tu maana watu wote humu tunamjua kwa sababu ya hilo na ndiyo maana ikitokea mtu akawa wa kwanza kufika katika story Fulani mtu huyo huanza kumuita kwa sauti na pengine hata kumtania kuwa amempiku. Ila siku hizi amekuwa mzembe mzembe sio kama zamani.
mende msafi: mmh basi humu kuna mambo.. sasa na huyo aliyesimama juu ya meza anarukaruka ndo nini vile.
mshana jr: hahahaha…huyo anaitwa Alosto. Jamaa ni mgeni tu lakini amekuwa ni msumbufu balaa. Jana alisema eti jeseverest hachangii vitu vya maana kazi yake kukimbia kimbia tu ili awe wa kwanza.
mende msafi: jose yeye akasemaje?
mshana jr: aah sijau maana wakati jamaa anasema hivo jose hakuwepo na hadi natoka humu jose alikuwa bado hajafika pale.
mende msafi: na Yule anayetangaza na yale madude wanaotumiaga wanaouza sumu ya panya ndo nini ville?
mshana jr: huyo anaitwa DJ Sepetu. Yeye hujifanya mtangazaji na huwa anafanya mahijiano na watu wahumu. Nasikia kama kasema jumapili hii atakuwa anamuhoji alibakari ila naona kama interview hiyo haija pokelewa vizuri na wadau, sijui kwa nini.
mende msafi: duuuh..kumu kunamambo mengi aisee. Sasa mbona naona kama kuna fujo nyingi, vipi watu huwa hawapigani humu.?
mshana jr: ugomvi hutokea ila kuna walinzi ambao husimamia usalama wa humu ndani. Kwa mfano kama umetumia lugha chafu huwa wanatoa amri utengue kauli yako lakini kama ni kosa kubwa zaidi, wanaweza kukupa adhabu ya kutoingia humu kwa siku,wiki au miezi kadhaa.
mende msafi: (anastuka) miezi?
mshana jr: ndiyom au we unashangaa. Kuna jamaa alikuwaga anatoa stori za ukweli sijapata kuona alikuwa anaitwa The bold lakini sijui alifanyaje bwana, amezuiwa kuingia humu kwa miezi mitatu.sasa alikuwa nademu wake anaitwa Nifah, alipoona mshkaji kafukuzwa naye akaamua kuondoka kisa bwana ake katimuliwa.
mende msafi: aisee, kumbe na mimi naweza kupata demu humu.
mshana jr: ndiyo unaweza lakini sikushauri.
mende msafi: kwa nini?
mshana jr: wengi wao wanajipaka mamekap na kujifanya wao ni matawi ya juu lakini hamla lolote. Utaishiwa kupigwa mizinga lakini papuchi hauto pata kamwe.
mende msafi: papuchi? Ndo nini hicho
mshana jr: aaaah utajua tu ukishakuwa mwenyeji…daah halafu nilikuwa nimesahau kitu cha msingi sana. Njoo huku nje.
mshana jr na mende msafi wanatoka nje ya lile jengo la chit chat.
mshana jr: unaliona lile jengo kubwa lililoandikwa PM?
mende msafi: ndiyo
mshana jr: Mle ndani kuna vyumba vidogo vidogo vingiii. Mle ndani ni kwa ajili ya mazungumzo binafsi au tuseme ya siri. Kama kuna mtu utamuona humu ndani na ukataka kuzungumza naye kwa kina bila kubugudhi wengine unamuomba muende kuleee ndani na mnaiingia katika moja ya chumba mnaongea then mkimaliza mnatoka na kuendelea na mambo mengine. Sasa hivyo vyumba wengine wanatumia kutongozea ila kuna wengine wanavitumia kwa mambo ya msingi. Ila mimi tangu nimekuja humu sijawahi ingia mle. Sasa mkuu, ngoja mi niende jukwaa la picha. nataka nikawape picha wadau wangu. So tutusomana mkuu na tusisite kupeana hai tutakapokuwa tunakutana sehemu mbalimbali humu ndani..
mende msafi: poa poa ngoja mi nirudi chit chat.. si unajua zile picha za wale mademu sikuziona..
mshana jr: unataka ujiunge na chama la mafuvu?
mende msafi: mafuvu?
mshana jr hageuki wala kujibu, bila kutembea huku miguu ya mshana ikiwa imegusa chini anaondoka kwa kasi kuelekea jukwaa la picha lilipo. Anateleza kwa manjonjo na madoido kama amevaa viatu vya matairi. mende msafi anabaki kustaajabu tukio lile.
Itaendelea………
episode 02 post namba #36