JF talk garden, eneo lenye vituko na vitimbi. Msimu wa kwanza..

Haaaa haaaaa haaaa haaaa mkuu kula like kwanza na Asante kwa appreciation
 
Hongera kwa ubunifu, hapo kwa Joseverest, nimejikuta nachek kwa sauti sana.
 
Dah, mkuu hili dude si mchezo...

Pale Joseverest alipokupamia amenichekesha sana, halafu kuna kama mara 2 nimemuwahi kwenye kijiwe cha story sasa ulivyosema watu wanamtania ...

Mwana fanya kuzifupisha fupisha ili ziwe nyingi...

Ngoja nielekee kwa Jembekillo kwenye lile jengo la kupigiwa makofi.
 

Jamaa katisha mkuu, yaani nimejikuta nacheka kwa sauti ulipompamia.

Halafu kama umenote ni kwamba watu tukiona kuna mtu anaanzisha story basi tunakimbia ili tukuwahi.

You have set some kind of standard ambayo ni exception, reply early with relevant response.
 
Yap yap bro, tuko pamoja tuendelee kufurahia JF yetu pendwa
 
Na mende msafi

Episode 02

Previously in JF talk garden

mshana jr: unataka ujiunge na chama la mafuvu?

mende msafi: mafuvu?

mshana jr hageuki wala kujibu, bila kutembea huku miguu ya mshana ikiwa imegusa chini anaondoka kwa kasi kuelekea jukwaa la picha lilipo. Anateleza kwa manjonjo na madoido kama amevaa viatu vya matairi. mende msafi anabaki kustaajabu tukio lile.

Tuendelee….

mende msafi anageuka na kuanza kupiga hatua kulekea kwenye jengo la chit chat. Anafika na kuingia ndani. Anasimama kwa muda kisha anaanza kupita kikundi baada ya kikundi na kusikiliza maongezi yao. Kila kikundi anachopita anakuta kina mada inayovutia sana. Anafika katika kundi la wale wanaoonyeshana picha za wanawake. Anaangalia kila picha inayoonyeshwa. Mara anaanza kuhisi ule mkono usio na mfupa unaanza kunyanyuka. Anaingiza mikono mfukoni na kuutengeneza vizuri ili usije muaibisha.

Anaamua kusogea pembeni baada ya kuona unagoma kutulia. Anawaza jinsi ya kuufanya utulie. Anapata wazo. Wazo la kuwatafuta watu wapige story pamoja ili mawazo ya wale wanawake wa kwenye picha yatoke. Anasogea pembeni kidogo na kuanza kusema kwa sauti.

mende msafi: habarini wakuu njooni basi tubadilishane uzoefu katika hili, kwa wale ambao mlishawahi kutumia mswaki halafu muda mfupi ukaja ukagundua kuwa huo si mswaki wako, wewe ulifanyaje au ulijisikiaje? (watu hawaonyeshi dalili ya kusogea kumfuata. Anakohoa kidogo kutengeneza koo kidogo na anavuta kiti na kukaa) jamani eeh..mkuje basi tupeane uzoefu kuhusu jambo huli.

Anakuja Numbisa na kuvuta kiti na kukaa

Numbisa: (huku akimwangalia mende msafi) ngoja waje wenyewe, mi ntakuwa msikilizaji tu (Numbisa anamwangalia joseverest ambaye alikuwa anatembea juu ya meza kwa kasi kuelekea iliko kona ya jengo la chit chat). Samahani jose kwa kuwahi nafasi yako

Joseverest: (Joseberest anageuka nyuma kumwangalia numbisa huku akiwa bado anatembea kwa kasi juu ya meza) sawa mkuu, nakuja (kisha anaruka kwa kasi na kutua chini na kuendelea na safari zake)

mende msafi: (akiwa anamwangalia jose) hahahahaha(anamgeukia numbisa) vipi we hujawahi tumia mswaki wa mtu kwa bahati mbaya?

Numbisa: hapana mkuu. (kisha anaondoka)

Mara anakuja babu asprin

Babu Asprin : we dogo ina maana umetoka huko kujaa kuongea upuuzi humu? Watoto wa siku hizi mkoje?. Umekosa vitu vya maana vya kuongea?

mende msafi anashusha pumzi huku akimuangalia babu Asprin aambaye alikuwa bado amesimama pembeni yake. Akiwa bado hajui ajibu nini anakuja bibi faiza foxy, anasimama mbele ya mende msafi na kisha kulamba midomo yake minene. Kisha anamgeukia babu asprin

Faiza foxy: yaani mzee mwenzangu siku hizi JF tumevamiwa, vitoto vipo vingi sana siku hizi.

mende msafi anameza mate na kuangalia chini kwa aibu. Akijiangalia yeye ni kijana mdogo na pembeni yake amezungukwa na watu wa makamo umri wa bibi yake na babu yake. Taratibu ananyanyua macho yake kwa bibi faiza na kukuta bado anamwangalia, anayashusha tena kwa kasi.

Babu Asprin: huu ndo ubaya wa shule kufungwa. Yaani humu huwa kunajaa vivulana tu

Bibi faiza: kweli mzee mwenzangu, JF yasikuhizi sio kama zamani. Wametuharibia sana. Angalia huko ukutani walivyochorachora na kuandika madudu ya ajabu, hata ile rangi ya ubluu na nyeupe iliyokuwa inapendezesha humu ndani haipo.

Anakuja billy walter II.

billy walter II: anacheni kuzingua aisee. Kwanza nyinyi ni wazee huku jukwaa la chi chat vepeee!! Si muende kule jukwaa la uchumi na siasa kama mnataka kuongea mambo ya maana!

Bibi faiza: “vepee” ndo nini? Huko shuleni huwa mnaenda kusomea ujinga? (bibi faiza anamshika mkono babu asprin) mzee mwenzangu twende tutoke humu naweza jikuta nimetoa laana kwa watoto wa watu bure.

billy walter II: asie kweli.. nenda kalee wajukuu zako huko. Tuachieni chit chat yetu.(kisha anaondoka)

Mara anakatiza Miss Natafuta. Ana umbo zuri si mchezo maana ana chura wa maana. Babu asprin anageuza macho yake na yanaenda kutua kwenye chura ya Miss Natafuta.

Bibi faiza: twende kule jengo la intelligence basi.(bibi faiza anageuka anamwona babu asprini akimuangalia Miss Natafuta. Bibi faiza anakunja uso kwa hasira)

Babu asprin: (kwa sauti) Miss Natafuta

Miss natafuta anageuka, anamuona babu asprin na bibi faiza.

Miss Natafuta: naona uko na bibi yetu

Babu asprin: njoo bwana, huyu asikutishe (bibi faiza anamwachia mkono babu asprin, bila kuongea chochote anaanza kutoka nje ya chit chat.)

Miss natafuta anafika na kumsalimia babu asprin. Babu asprin anaushika mkono wa miss natafuta na kumvuta kwake, miss natafuta anajikuta anajaa kifuani kwa babu asprin na kisha anamkumbatia)

Miss Natafuta: heee mzee wewe huoni aibu?

Babu asprin: aibu gani bwana, ulikuwa unaenda wapi kwanza.

Miss Natafuta: MMU

Babu asprin: MMU kufanya nini bwana, twende kule PM

Miss Natafuta: mh mzee wewe, PM kufanyaje?

Babu asprin: (huku akimshika mashavu kimzaha) aaah bwana we twende tu. unanihofia hata mimi babu yako?

Miss Natafuta: hatukai sana lakini.

Babu asprin: twende zetu basi

Miss Natafuta na babu asprin wanaondoka. mende msafi anawatazama babu asprin na Miss Natafuta wanavyoondoka Huku akiwa na maswali mengi kichwani. Wanafungua mlango nakutoka nje. Kabla ya mlango haujajifunga anaindia Deogratius Kisandu akiwa anatembea kwa kenesa huku mkono mmoja akiwa ameuweka mfukoni. Anasimama na kuwangalia watu waliokuwamo ndani kisha anapiga hatua tatu mbele. Annapiga makofi matatu kwa nguvu, gafla kuna kuwa kimya, watu wanageuka kumwangalia.

Deogratius Kisandu: mnajua nini wakuu, mimi lazima nije niuone Malia Obama.

Chumba kizima kinalipuka kwa kelele, wengine wakiwa wanacheka wengine wakimtukana. Wengine wanampuuza na kuendelea na mambo yao. mende msafi anaamua kuungana nao kwenda kuona kilichojiri

to yeye: hivi wewe kisandu huwa unafikiria kwa kutumia kiungo gani

Slim5: hebu leteni maji tumwagie huyu, naona ameanza kuota ndoto za ajabu ajabu

jakitoo: mmh yaani vyuma vimekaza hadi watu washaanza kuchanganyikiwa.

Slim5: to yeye, huyu kisandu naona anafikiria kwa kutumia utumbo mpana

Mbwa dume: (anaangalia kushoto na kulia katika llile kundi kama anamtafuta mtu) Joseverest siku hizi unazingua ujue..

@deogaratius kisandu: achene upumbavu nyinyi..mbona mna wivu sana nyinyi. Kwanza tokeni hapa kama hamuwezi kuongea vya maana ntamwaga meno yenu wote chini hapa kwa teke moja tu.

Mod Two: (huku akimyooshea kirungu cheusi deo kisandu) we kisandu, kuwa mstaarabu tutakutoa nje sasa hivi.

Itaendelea…..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…