kusaini haisaidii tunao great thinkers humu jamvin wanaoweza kutengeneza rasimu ya katiba mpya inayoweza kuonesha ni vipengele gani tuvibadili ili kuitwa katiba mpyaaa kabisa na ili kupambana na hoja kama za akina kombani, mwinyi na wengineo ambao wanajua kwa kuundwa katiba mpya kuna hatari ya ICC kuja Tanzania.
Kuna watu katiba imewaruhusu kugeuza nchi hii ya kwao na wanaweza kufanya watakavyo kuanzia rasimali za nchi hii na uongozi-yaaani wameamua kuwa wanarithishana.
CCM wana kundi la watawala na wapiga makofi lakini ccm ina members 5 miliion wakati watanania tupo 42 miliion -sasa lazima tuje na mawazo ya kimkakati sio kusaini haitoshi tuanze na msingi kuainisha mapungufu ya katiba ya sasa ili kushinkiza katiba mpya.
LAZIMA WAJITOLEE WANAJF AU CHADEMA MANAKE IKO KWENYE ILANI YA CHAMA WATENGENEZE RASIMU YA KATIBA MPYA INAYOPAMBANUA KILA OUZO WA KATIBA YA SASA HALAFU TUISAMBAZE. TUPO TEYARI KUTEMBEA KWA MIGUU MTAA HADI MTAA NYUMBA KWA NYUMBA TANZANIA NZIMA KUELEZA KWANINI TUNAHITAJI KATIBA MPYA.