Wanajamii;
Mwaka Jana 2009 tulifanya mchakato wa kumpata JF SuperLady & Celebrity of 2009.
Mchakato wote mpaka mshindi kupatikana unaweza kuupitia hapa:
https://www.jamiiforums.com/complaints-congrats-advice/91605-man-of-the-year-2010-a.html
Mshindi wa 2009 alikuwa ni "Woman Of Substance" ambaye anategemewa kukabidhi taji lake kwa JF Woman of the Year 2010.
Mwaka huu tunataka kuuboresha mchakato huu na tunapenda kupitia mchakato huu kupata washiriki wengi na kuipa taswira JF kuwa kuna watu wanafanya mambo makubwa.
Mwaka huu 2010 tunafanya mchakato wa kumpata JF WOMAN OF THE YEAR 2010 na pia JF MAN OF THE YEAR 2010.
Katika mchakato wa awali tutapendekeza majina mbalimbali katika kila category, na baada ya kupitia post zote za mapendekezo tutachagua watatu kutoka katika kila category na kisha kuwapambanisha kupitia JF POLLS. Mwaka huu napendekeza tutoe zawadi yenye hadhi fulani kwa washindi ili kutoa changamoto za umakini katika mabandiko haba jamvini. Tutajulishana zawadi hizi tutakapoingia katika mchakato wa Kupiga kura.
Vigezo vifuatavyo vizingatiwe katika kutoa mapendekezo ya watakaoshindanishwa katika hizi KURA ZA MAONI:
1. Kama ni category ya WOMAN lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanamke na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike. Uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Shindano hili utakuwa ni Final. wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.
2. Kama ni category ya MAN lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanaume na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike.
Katika 1 na 2: Uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya JF (JEC) wa Shindano hili utakuwa ni Final. wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.
3. Anayependekezwa lazima kuwe na ushahidi unaoonyesha kuwa ni Mwana JF aliyebobea hasa kutokana na Threads alizozianzisha na pia post alizozianzisha. Vyote lazima viwe na impact chanya kwa wasomaji wa JF
4. Awe ni mwenye uwezo wa kusimamia hoja zake na kuzijibu kikamilifu bila jazba na kwa umahiri wa hali ya juu pale ambapo anapata challenge toka kwa wachangiaji.
5. Awe ni mwenye ushawishi wa hali ya juu katika mabandiko anyochangia walau kwa muonekano wa wachangiaji kuunga mkono hoja zake.
6. Asibobee kwenye Jukwaa moja tu. Walau awe mchangiaji mzuri wa majukwaa yasiyopungua matatu
7. Asiwe mtu wa shari katika majibizano kiasi cha kupelekea Mods kumpa "BAN".
8. Aonekane wazi katika mabandiko yake anaweza akahisiwa kuwa Kiongozi Mzuri.
9. Awe Mchangiaji ambaye ni active walau mara moja kwa wiki. Ikiwa zaidi ni vizuri zaidi.
10. Awe ni mtu asiyeogopa kukemea mabandiko yenye lengo la kutukana, kudhalilisha, kubagua, kuleta mfarakano na kutokuelewana baina ya wanachama wa JF.
Sasa kila moja yuko huru kutoa mapendekezo yake ya nani wanastahili kuingia katika tatu bora katika kila category.
Nashauri kuwa mapendekezo ya majina yaambatane na maelezo mafupi.
Uwanja ni wenu. Karibuni.
------------------------------------------------------------
UPDATE 1:
Mchakato wa Kupata mapendekezo ya Majina ya wana JF watakaoingia katika king'ang'anyiro cha kumtafuta JF Man of the Year 2010 and JF Woman of the Year 2010 umeshakamilika. Kura za maoni zimefungwa rasmi Ijumaa 3-12-2010 Saa 6.00 Usiku na matokeo ya waliokuwa nominated nayatoa kama yalivyopendekezwa:
Waliopendekezwa kugombania taji la JF MAN OF THE YEAR 2010 ni:
1. JS - Kura 1
2. Acid - Kura 2
3. Kiranga - Kura 2
4. Mwanakijiji - Kura 2
5. Nyani Ngabu - Kura 3
6. Pasco - Kura 1
7. Mkandara - Kura 1
8. Superman - Kura 1 (Aliomba ajitoe mwanzoni kwani yuko JEC)
9. Malecela - Kura 1
10. Ivuga - Kura 1
Waliopendekezwa kugombania taji la JF WOMAN OF THE YEAR 2010 ni:
1. Regia Mtema - Kura 2
2. Gaijin - Kura 2
3. Woman of Substance - Kura 2
4. First Lady - Kura 1
5. Belinda Jacob - Kura 1
6. Maria Roza - Kura 1
Kura Zilizoharibika:
1. BujiBuji - Kura 1 (Haikutaja category)
Majina yafuatayo, yamepitishwa na JEC kuingia rasmi kaatika POLLS za kutafuta JF MAN OF THE YEAR 2010 ni:
1. Acid - Kura 2
2. Kiranga - Kura 2
3. Mwanakijiji - Kura 2
4. Nyani Ngabu - Kura 3
Majina yafuatayo, yamepitishwa na JEC kuingia rasmi kaatika POLLS za kutafuta JF WOMAN OF THE YEAR 2010 ni:
1. Regia Mtema - Kura 2
2. Gaijin - Kura 2
3. Woman of Substance - Kura 2
Thread Maalumu itafunguliwa sasa ili kuweza kuwapigia kura waliotajwa.
Asanteni wale wote mliotumia haki yenu ya kikatiba kupiga kura za maoni.