Elections 2010 JF's Maxence LIVE on EATV "Uchaguzi Express Live"


Nadhani anashindwa kuelewa kuwa, hakuna kitu kisichowezekana hasa nia ikiwepo. Kenya ambao hawana rasilimali nyingi kama Tanzania, wameweza kutoa subsidized education schemes. Sisi wengi wetu tulisoma bure hadi elimu ya juu. Inawezekanaje leo, ambapo wazazi wengi wanaweza kupeleka watoto wao shule za binafsi, serikali ishindwe kusomesha bure wote waliobaki? Hii ni kejeli kubwa sana kwa maendeleo ya nchi. Kama hii ya elimu bure kwa watoto haiwezekani, basi hakuna linalowezekana hata moja.

Kuna wanaouliza eti pesa zitatoka wapi. Swali gani hili? Pesa za magari, furniture za nyumba na ofisi za serikali, vitafunio na vitafunwa, safari zisizo na tija, marupurupu ya semina, warsha, kongamano na mikutano isiyo na tija zinatoka wapi? Mbona hizo ni rahisi kuzipata kuliko za kusomesha watoto wa Tanzania? Je, pesa za migodi, uwindaji, utalii, uvuvi, kilimo, kodi mbalimbali na nyinginezo (japokuwa kodi tu hawawezi kuikusanya zaidi ya 30%) zinakwenda wapi? Tuache kutaniana kwenye mambo serious. Gamba anajiunga na team ya wanaotia aibu. Kama hajui jinsi pesa itakaosemesha watoto wa Tanzania itatoka wapi, anabidi arudi shule upya.
 

Huyo gamba ni limbukeni..period!!
 
Silaha kubwa ya wanaccm na mafisadi ni makundi makubwa ya wasomi ambayo yameamua kutokupiga kura, jamani.......kama tunataka mabadiliko ya kweli Twendeni tukapige kura.
 
Nianze kwa kuwashukuru wachangiaji wote waliotangulia, hasa wale ambao wamejitahidi kuonesha kuwa nilichokiandika ni matokeo ya ufinyu wa uelewa wangu. lakini napenda kuwahakikishia kuwa nilichokiandika ndicho kilichokuwepo katika JF..,hata kama watu hawa wakiongozwa na maxence watajaribu kupinga ukweli huo bado nafsini mwao watabaki na ukweli huo daima.

Mtu anapoandika juu ya kitu fulani ni wazi kuwa kitu hicho kimemgusa na kina interest na yeye, hata mimi niliposema kuwa JF ni ya watu wa chadema,nilikuwa na sababu na ushahidi wa kutosha kuwa hawa watu tunaofanya nao mjadala humu ndani wakisaidiwa na administrator wanatumiwa na chadema katika kuponda na kupinga (wakati mwingine mambo ya msingi) yaliyofanywa na chama tawala ili tu watimize adhima yao ya kukichafua chama na wanachama wake. ninachokisema mimi ni kuwa si vibaya wala si dhambi kwa mwana-JF kuwa mshabiki au mwanachama wa chadema lakini lazima tukubali kuwa imani yetu katika chama isiathiri uendeshaji wa JF.


Inashangaza sana pale ambapo tunalalamikia uhuru wa vyombo vya habari ikiwa hapa JF tuko biased, hivi mnakumbuka mara ngapi mli-reject na ku-ban post zangu binafsi na hata zile za watu wengine ambazo zinamuelekeo wa kusema ukweli wa mambo na kuonesha yale yaliyofanywa na serikali ya CCM. Kama tunasisitiza uhuru, kwanini mambo hayo yaliyopostiwa hayakupewa nafasi ya kujadiliwa na hayakuwa na kasoro yoyote kulingana na taratibu tulizojiwekea hapa JF isipokuwa tu mawazo hayo yalikuwa pro-government.

Si mimi peke yangu ambae nalalamikia hili wapo wengi waliojaribu wakashindwa na ndio maana nikataka maxence awataharifub watanzania wote kuwa hiki chombo ni cha chadema ili wasije wakapata tabu ya kufuta post zitakazokuwa na mawazo ya kuonesha kilichofanywa na serikali au angewatahadharisha watu wajue ni kitu cha aina gani kinatakiwa kiwe posted katika jamii forum….!

Jueni kupingana na ukweli ni kazi ngumu hivyo jiandaeni kuvuja jasho jingi katika kupinga hili.
 

Mbona unakuwa mgumu kuelewa wewe??

Naona unaongozwa na hisia zaidi, kabla hujakurupuka na kuanza kutulazimisha tukubaliane na wewe.

Ni vema ukasoma post zote ukaelewa, zipo kwenye Lugha nyepesi saana Na Maxence katoa ufafanuzi ambao hata mtu ambaya hajaenda shule anaelewa,, sasa naona wewe unakataa kuelewa.

Ni vema ukanyamaza badala ya kuendelea kujiabisha hapa kwani unakera sasa.
 
Max ana onekana yupo camera shy na hazungumzi kwa kuji amini. Point alizotoa ni za nguvu ila presentation mushkel kabeel. Kidogo kidogo tuta fika
 
Max ana onekana yupo camera shy na hazungumzi kwa kuji amini. Point alizotoa ni za nguvu ila presentation mushkel kabeel. Kidogo kidogo tuta fika

weweeeee hebu kuja hapa.... hurry up
 

Suley,

POLE SANA KAKA! LAKINI NAOMBA KUKU ULIZA SWALI MOJA HIVI TBC1 NA MAGAZETI YA DAR LEO NA DAILY NEWS NI MALI YA CCM ETI?

NAOMBA BASI UANZE KUMFAHAMISHA TIDO MUHANDO NA WENZAKE WAWATANGAZIE WATANZANIA KUWA TBC1 NA MAGAZETI YOTE YA DAR LEO NA DAILY NEWS NI MALI HALALI YA CCM, KABLA YA KURUSHA SHUTUMA HAPA JF WAKATI UNA UHURU WA KU POST CHOCHOTE ILI MRADI USIVUNJE SHERIA TULIZOJIWEKEA.

KAKA MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU KWELI!
 

Kwa watangazaji wa kibongo mkuu wala usiulize ni ukanjanja tu ndo umewajaa!
 
Sikutaka kushiriki kwenye mjadala huu lakini watu kama Suley huwa wananifurahisha na kusababisha aidha nitoe maoni ili wanaoitembelea JF wajue uongozi wa JF unatoa kauli gani kwa baadhi ya kauli kama hizi:


Umeanza na kujihami kwanza!

Mkuu,

  1. Raha ya JF ni kuwa tunapenda kuruhusu kila aina ya comment pamoja na hizi zako! Sasa, as usual, kwakuwa una USHAHIDI haina sababu ya sisi kukuzunguuusha sana... ULETE, kama utakuwa umezisoma sheria za JF utakubaliana nami kuwa unachofanya ni kuvunja sheria, na hapo ukifungiwa moja kwa moja utasema umeonewa! Lakini inshallah, kama una ushahidi wa wazi, aidha video, au hard copy ya mkataba kati ya JF na CHADEMA kuwa JF itaendeshwa kwa maslahi ya chama hicho tu basi mwaga tu mkuu, uwanja upo wazi!
Oh yeah?

Wewe unakiri uko bias? Uko mrengo gani mkuu? Sisi wengine hatumwangalii nyani usoni! Unataka kuuaminisha umma kuwa wanaofungiwa ni kwakuwa wako tofauti na CCM? Unataka kusema Hussein Bashe na Nape ambao ni wana CCM damu kabisa na vijana wenye uwezo wa kusimamia hoja na waliojisajili JF kwa majina yao halisi na kujibu baadhi ya hoja na hata zile zilizoonekana kuwa ngumu tuwaite CHADEMA?

Uzuri nimeambatanisha sheria za JF, kwa wale wanaonyweshwa upupu huu nawashauri wazisome waangalie maandishi ya wale wanaofungiwa na waseme kama kunakuwa kuna uonevu kisa ni wanazi wa chama tawala au kwasababu ya makosa yao.

Watu kama wewe ndio mnawadanganya viongozi wetu, hivi unaweza kusema kila kinachojadiliwa JF ni kuiponda CCM na viongozi wake tu? Unataka kutuaminisha kuwa hakuna hata sehemu moja ambapo wadau ndani ya JF wameyasifia mambo kadhaa yaliyofanywa na serikali ya JK? Unataka kusema hata mkuu wetu (mkongwe!) Mtu wa Pwani naye ni CHADEMA? Unatarajia afurahie andiko lako?

Unataka kusema hizi posts zote ni za kuiponda serikali ya JK?

  1. https://www.jamiiforums.com/habari-...bo-zuri-limefanyika-tanzania-hongera-tra.html
  2. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/246-mazuri-ya-edward-lowassa.html
  3. https://www.jamiiforums.com/busines...kuvi-na-open-spaces-hongera-mkuu-wa-mkoa.html
  4. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/64122-hongera-mahiga.html
  5. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/34215-hongera-mama-salma-kikwete.html
  6. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/34102-hongera-prof-tibaijuka-kwa-2009-g%F6teborg-award.html
  7. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/26002-hongera-pinda-na-samahani-ulikuwa-sahihi.html
  8. https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/7029-pongezi-mheshimiwa-spika.html
  9. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/25944-hongera-somebody-jk-et-al-now-we-are-talking.html
  10. https://www.jamiiforums.com/interna...d-kamala-kwa-kutetea-maslahi-ya-tanzania.html
  11. etc
Upende usipende, ukipigiwa makofi mara zote utarajie kuzomewa siku moja... Hatuwezi kuwa kama magazeti ya vyama kupongeza tu bila kukosoa, lazima tukubali kutokubaliana. Ndiyo maana ya JamiiForums, kurekebishana tunapoona mwenzetu anakwenda kombo, bahati mbaya wengine hawapendi kushiriki mijadala ya kukosoana, wanataka wapongezwe tu! Kwa hili usitarajie ndani ya JF itawezekana kubadilika kuwa tutaacha kukosoa tunapoona kosa ili tuwafurahishe watawala!

Mkuu,

Naomba uangalie hao unaoshirikiana nao kwenye kulalamika, waulize kama hakuna sehemu watakiri kuwa nao walienda kombo... Sasa, ushakiri kuwa wewe uko bias, unaweza kusema post gani imefutwa na ukakiri ina objectives zipi? Mind you, JF hatufuti, tunaweka kando... Zinaweza kurejeshwa posts zako zilizokuwa trashed na ukaumia moyo endapo zitaonesha wazi zilikuwa ni hatred posts!

Jueni kupingana na ukweli ni kazi ngumu hivyo jiandaeni kuvuja jasho jingi katika kupinga hili.
As usual, watu wa aina yako mkuu huwa wanapenda kuwa na kauli za hivi,,, defensive mode ON!

TUMIA AKILI KIDOGO KUNIELEWA CHINI HAPA:

NDIYO: JF iko bias CHADEMA, na ni mali ya CHADEMA na hivyo basi:

NDIYO: CCM ni chama cha Mafisadi kama wanavyodai walio wengi na kila aliye ndani ya chama hiki ni fisadi tu!

NDIYO: CHADEMA ni chama cha wachaga na wanachama wao WOTE ni wachaga tu.

NDIYO: CUF ni chama cha waislam, hakuna hata mmoja ambaye si mkristo, tena cha kigaidi kwani kiliingiza visu nchini!

TLP? SAU? UMD? UDP? Mbona hivi haviguswi?

Kwa wale mliosoma hapo juu, the bottom line ni kuwa:

Mti wenye matunda mazuri mara zote hupigwa mawe! Tafakari...!
 
Bro, nadhani unweza kuwa very wrong

Data wanazo mods adn admins but i can bet my shoes kwamba wanaJF walio tanzania ni wengi zaidi and it could be up to 70%

I hope we will get clarification on this

Kwa sasa hii ni kweli. Mtu unaweza hata kufanya utafiti wako mwenyewe na kugundua hilo. Miaka miwili iliyopita na kurudi nyuma hadi 2006 wanachama wengi nadhani walikuwa ughaibuni.

Ukitaka ujue kuwa wanachama wengi kwa sasa wako Tanzania, jaribu kufungua JF kwenye siku za wiki (Jumatatu - Ijumaa) kuanzia saa moja asubuhi hadi kwenye mitaa ya saa kumi na moja jioni saa za Afrika Mashariki (ambapo kwa saa za Eastern Standard Time za Marekani ni 12:00AM - 10:00AM).

Kwenye mida hiyo watu wengi Tanzania wanakuwa ndiyo wameingia na wako makazini. Kwa vile Watanzania wengi hawana huduma za mtandao majumbani, wanachama wengi wa hapa JF hutegemea mashine (PCs) za makazini. Katika masaa hayo niliyoyataja hapo juu, idadi ya watumiaji wa JF huongezeka sana. Ukitaka kujua hili teremka mpaka chini kabisa ya tovuti ukiwa kwenye ukurasa wa kwanza na utapata takwimu hizi na zinginezo.

Ikifika saa kumi na moja jioni idadi inaanza kupungua kwa vile wengi ndio wanaanza kufunga ofisi na kurudi nyumbani. Wakisharudi nyumbani ndiyo jiiiiiiii tena mpaka kesho yake. Siku za mwisho za juma (Jumamosi na Jumapili) idadi ya watumiaji kutoka bongo hupungua sana na sababu nimeshailezea hapo juu. Wengi hawana intaneti majumbani achilia mbali kompyuta zenyewe.

Kuna baadhi ya watu humu hasa walioko majuu ndiyo wenye uwezo wa kuwa hapa masaa 24. Hii ni kwa sababu intaneti majuu inapatikana kwa bei rahisi na sehemu nyingi tu siku hizi zinatoa huduma hii bure. Kama mtu anaishi kwenye subdivision au apartment complex, sehemu hizo zinaweza zikawa zinatoa huduma ya wi-fi kwa bure. Hata migahawa kama McDonald's, Burger King, na Hardee's yenye kutoa huduma za chakula cha haraka na yenyewe inatoa huduma ya wi-fi bure siku hizi.

Hapo sijagusia hand-held devices n.k. Kwa hiyo ni kweli kabisa, kwa sasa wanachama wengi wapo Tanzania na wengi wa wanachama wapya hasa wale waliojiandikisha mwaka jana mpaka hivi sasa nadhani idadi yao kubwa ni kutoka Tanzania.
 
Nataka kuwahakikishia kuwa yale niliyoyasema yote ni kweli tupu..,vifuatazo ni baadhi ya vielelezo nilivyofanikiwa kuvipata katika kuthibitisha yale niliyotanguliza hapo juu kuwa JF iko chini ya CHADEMA.

Fuatilieni hivi vielelezo kisha mniambie kuwa vilistahili kuondolewa ndani ya jamii forum kulingana na sheria na taratibu tulizojiwekea.

Mnakumbuka mliifuta post hii ikiwa na kichwa cha habari "wewe ni DR slaa"..,niambieni ni kwa nini..? na ninainukuhu kama ifuatavyo

Je mnaikumbuka na hii..?

SLAA UMEMZIKA CHACHA WANGWE NA WOSIA WAKE?

Kisha mniambie kuwa hawa walioandika haya wanazusha..,ni mengi yanayofanywa humu ndani ya JF ambayo yako dhahiri kuwa yanafanywa kwa mkono wa chadema ulioko ndani ya jamiiforum na nashindwa kuelewa kwa nini watu wajaribu kulikanusha hilo hali ya kuwa liko wazi kabisa.
 

Sasa ulitaka akutaje wewe?
 
Sawa, kwakuwa unazijua SHERIA ZA JF na umeamua kuja na USHAHIDI mzuri unaoonyesha kuwa JF ni mali ya CHADEMA kwakuwa walifuta hoja zako naomba nianze nami kukujibu kwa kukuonyesha zilipoFUTWA ziliishia wapi... Nadhani ulionewa sana mkuu wangu:

Mnakumbuka mliifuta post hii ikiwa na kichwa cha habari "wewe ni DR slaa"..,niambieni ni kwa nini..? na ninainukuhu kama ifuatavyo
Wote mliokuwa mkihoji juu ya uwezo wa Slaa na kama anastahili kupewa jukumu la kuliongoza taifa hili tuliwaunganisha HAPA... Sasa nadhani utaona kuwa TULIFUTA kwakuwa wewe si CHADEMA, tulikuonea sana mkuu, tuwie radhi!

Again,

JF kama JF haiendi unavyotaka kuilazimisha iende mkuu, kwa siku zinaingia posts zaidi ya 2,000 na zote zinapitiwa kuhakiki hoja kutojirudiarudia... Sasa kwa UCHADEMA wetu kama viongozi wa JF, tukagundua kuwa ulikuwa mwenzetu hata hukuperuzi kuangalia kama kuna hoja hiyo tayari, tukaiFUTA lakini kwa bahati mbaya ikadondokea HAPA...

Nasikitika kuwa ushahidi wako haujajitosheleza na nadhani BADO hujazisoma vema sheria za JF, ilisikitisha wewe kuja na username ya PADRI na kisha kuanza kuleta mijadala ya kuliponda kanisa katoliki kwa mgongo wa jina hilo... Hii inamaanisha wewe NI MCHAFUZI WA MAKUSUDI lakini tulikuvumilia kwa muda na kukuacha uje na jina jingine!

Ushahidi mwingine ambao ni external links za kujitangaza UMEONDOLEWA kwani spamming hairuhusiwi JF, soma sheria zetu vizuri mkuu.

ONYO:

Kuna watu wana u-CHADEMA na u-CCM sana, tunaomba wekeni kando hizo itikadi mnapokuwa mnajibizana katika hoja, vinginevyo mtakuwa na jazba na kuamini kuwa hoja zenu zinafutwa tu!
 
ha ha ha,
wenzetu mnapenda sana kulialia kaa vichanga.
posts na threads zangu kibao hapa zinafutwa na mimi sio mwanaccm.

Grow up
 

Wewe Invisible,

Nakusubiri kule kwenye thread ya pongezi kwa Rev Masanilo. Ile thread haitanoga bila kuona wewe au Max mkitoa pongezi zenu.
Painkiller na Silencer najua wao ndo kabisa hawatatokea ila it's okay.
 
Ni mara kwa mara tunapoona malalamiko ya dizaini hizi dhidi ya JF, ya kwamba ni chadema au posts zimefutwa, inatokana na watu kutokujua matumizi mbadala ya computer zao au watu kutojishughulisha kwanza kutafuta au basi kuuliza tu kiungwana post zao zimewekwa wapi.

Hii inasikitisha sana kuona mtu amekaa akinyong'onyea na kuilaani JF kwa nguvu zote kuwa ni chadema kumbe posts zake ziliunganishwa tu na thread nyingine, lakini initiative ya kusearch ndo hakuna!
 

Ni wazi kuwa post ambayo ilitumwa ililenga ku-stress suala zima la maadili yanayoendana na uongozi. Tofauti na pale kwenye thread inapoelezewa kuwa ilipelekwa. hata hivyo thread ikiwa innapelekwa mahala fulani ambapo tayari ilishajadiliwa inaoneshwa kuwa iko moved lakini hilo alikufanyika pindi ilipoondolewa thread hiyo kwani nilikuwa nimelog in na nilikuwa naangalia.
kama hayo hayatoshi..,naona mmeamua kunizushia kwa makusudi na kuniwekea hila katika kitu ambacho sikukisema wala kukifanya hili mjustify kile mnachotaka kukifanya. waswahili wanasema ukitaka kumuua mbwa basi mpe jina baya,naona hili linataka kutokea hapa kwenye JF. Ninauhakika kuwa IP adress yangu mnayo na hivyo mnajua kuwa hilo la kutumia username PADRI sijawahi kulifanya wala kukashifu kanisa. kuna wakati watu wanajengewa zengwe fulani hili kuhakikisha kuwa kitu fulani kinafanyika bila kupingwa au ni tahadhari kwa mtu huyo ili asirudie kufanya kitu fulani alichokifanya hapo awali kilichopelekea kuzushiwa zengwe hilo. kama kuna ushahidi kuwa mimi nilitumia jina PADRI na nikalichafua kanisa, ungetolewa na kufanyiwa analysis kwa njia ya kiugwana na kielimu ili kumaliza jambo hili. kwanini mnajaribu kuzusha vitu ambavyo havipo...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…