Jibu group arusha kuna nini???

Kidasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2013
Posts
309
Reaction score
108
Kuna kampuni moja ipo Arusha eneo la Kijenge ya Juu karibu na Kanisa la KKKT.Kwa kweli nashindwa kuwaelewa kabisa,wamechukua hela kwa watu kwa minajili ya kuzikopesha kwa riba ya 15%.(Wao wanakopa kwa 10%),badala ya kukopesha kwa watu mwenye kampuni alizifanyia anasa na kujinunulia majumba,matokeo yake liquidity crises ikaanza baada ya depositors kutaka riba zao na principal zao.Aliitisha members kwa minajili ya kurudisha pesa za watu tangu April 2013.Cha ajabu tangu APRIL 2013 Hadi sasa ni kalenda na usanii uliopindukia.Mwezi september 2013 wakatoa list ambayo ni batch ya kwanza kulipwa ambapo utekelezaji wake ungeanza November mosi 2013.Cha ajabu kila mtu aliepo kwenye hiyo list akienda kuchukua pesa zake anaambiwa hamna fedha.Hiyo list waliitoa kwa maana gani?Wamepeleka wapi pesa walizozikusanya toka Feb 2013,au wanatuona sisi ni wajinga.Mimi na nwenzangu kama wanne tumeazimia kuhakikisha Ndugu Kombe anatukabidhi hati ya nyumba yake iliyopo Moshono.Haweizekani jamaa na Katimu chake watuchezee ushenzi wa kijinga namna hii.Kwa data ambazo zipo confirmed jamaa anadaiwa na depositors more than 4.5 billion.WADAU MLIOWEKEZA JIBU KUNA MATUMAINI AU NI DECI INGINE TENA HII.Thanks
 
pole mzee.Binafsi na rafiki yangu mwaka jana mwanzoni tulitaka kudeposit pale baada ya kuambiwa wanatoa riba ya 10% na nilishaenda pesa kwa minajili hiyo. Kufika pale tukakuta atmosphere ya pale siyo nzuri maana depositors tuliowakuta walionekana wana jazba ile mbaya kuona hali hiyo tukasepa na jamaa yangu. Baada ya kudodosa zaidi ndio tukapata ukweli huo kwamba pale ni hatari jamaa katumia zile pesa kununulia mashamba n.k na hakuna faida inayorudi. Ndio ikawa salama yetu
 
DECIIIIIII hiyoooo.

Nyie waiteni waandishi wa Habari tu muone litakavyoshughulikiwa,

Halafu fungueni kesi polisi na muache kwenda kienyeji.Maana inaonekana hata Kodi hailipiwi hapo

Sheria zipo na wanasheria wapo ,hembu fanyeni kazi kisasa sio kulalamika tu bila kufuata utaratibu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…