Jibu hili la Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Mbunge Saed Kubenea wa Ubungo ni sahihi?

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Posts
8,271
Reaction score
9,113
Katika kipindi cha bunge jioni hii ya leo, Mbunge Saed Kubenea alipata nafasi ya kuuliza swali la kisera kuhusu Tume ya Uchaguzi. Alihoji ni lini Serikali italeta hoja hiyo ijadiliwe ili ifanyiwe marekebisho Tume ya Uchaguzi kuzuia Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi?

Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliombwa na Spika kutoa ufafanuzi akasema kuna kesi Mahakamani imefunguliwa kuhusu shauri hilo, hivyo Bunge haliwezi ingilia shauri lililoko mahakamani.

Je, ni jibu sahihi?
 
SIMPLE ANSWER,BUNGE NI BUNGE na MAHAKAMA ni MAHAKAMA,Yeye ajibu SWALI tu.
 
Kuna kazi ukizifanya nchi hii lazima ugeuke kituko hata kama wewe ni Msomi nguli, moja wapo ni kuitetea CCM.
Kwan Tatizo ni lipi hapo ambalo Mwanasheria kakosea?, nisaidie
 
Kweli wapinzani ni vibudu. Shauri wamelipeleka wenuewe mahkmani , halafu wanatak serikali itoe ufafanuzi kwa jambo lililoko mahakamani, loooh, majanga
 
Wewe ambaye haujalamba galasa mbunge wako anakuwekea ugali mezani? Tehtehteh, wewe nadhani ulienda shule kukalia madawati tu.
Vipi imechoma hiyo? [emoji16]
 

Jibu sio sahihi, alitakiwa kujibu lini mswada utaletwa bungeni, pale hakuulizwa mwenendo wakesi Wa swala hilo, Ili kuingilia tungepaswa kujua swala lenyenyewe na namba yakesi hiyo maana mahakamani kuna kesi nyingi. Nahilo ilekuwa kama kichaka kuwazuia watu juu ya jambo fulani unasema lipo mahakani aliruhusiwi kuongelea, kinachokatazwa kuongelea mambo yanayoweza kupelekea kuharibu au kushinikiza maamuzi fulani, nahilo sio jambo geni mnakumbuka Tegeta Esrow? Bunge lilijadili naswala lilikuwa mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…