Jicho la Kifalsafa: Kinachotokea Tanzania ni "Consolidation of powers" and "Judgement Errors"

Jicho la Kifalsafa: Kinachotokea Tanzania ni "Consolidation of powers" and "Judgement Errors"

Chief Ortambo Ikumenye

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2017
Posts
247
Reaction score
503
Huu ni mtizamo binafsi na hisia za kifalsafa juu ya vitendo vya utekaji na mauaji nchini.

Kwa hulka ya mwanadamu pindi anapopata nguvu fulani iwe ya kibiashara, kisiasa, kidini, kimichezo n.k nguvu hiyo huambatana na mambo mengi ya neema kama umaarufu na kujulikana ambavyo havijawahi kutokuacha kumkosha mwanadamu.

Power, Fear and Greed (Nguvu, Hofu na Tamaa)
Ukishapata nguvu na kuonja asali ya kuwa mtu mwenye nguvu, basi ndipo hisia za hofu na tamaa hutamalaki (Hizi hisia za tamaa na hofu zipo ndani ya wanyama wote). Na hofu na tamaa ni hisia ambazo zimemtawala mwanadamu kwa miaka mingi sana. Hofu ya kupoteza nguvu uliyoipata na Tamaa ya kupata nguvu nyingi zaidi, kwasababu umeshaonja matunda ya kuwa na nguvu.

Inakuwa ni ngumu kwa mwanadamu mwenye nguvu kufikiria kwamba maisha yake yatafananaje bila kuhifadhi nguvu aliyokuwa nayo? Kwa jicho la kifalsafa, hilo ni swali linaloogofya kwa watu wanaomiliki nguvu fulani.

Swali hili ndilo linalowafanya wafanyabiashara kina Mohamed Dewji, Bakhresa et al. kuendelea kuchacharika usiku na mchana ilihali wana mabilioni ya kutosha. Wasanii kina Diamond Platnumz kuendelea kukuna vichwa vya ubunifu ili kubaki kileleni. Na sio jambo baya kuendelea kupambana kuhifadhi nguvu uliyokuwa nayo, ni hulka ya mwanadamu. Na hii ndio ninayoiita 'Power Consolidation', yaani unafanya namna usipoteze nguvu ulioipata kwasababu umeshaonja asali yake.

Ubaya na uharibifu huja pale ambapo mwanadamu anaruhusu kutawaliwa na hofu na tamaa. Hofu na Tamaa inayoweza kupelekea matajiri kuhodhi na kujirundikia utajiri kwa mbinu chafu na utapeli, au labda wanamichezo kutumia dawa za kusisimua misuli, au labda wasanii kujiingiza kwenye uraibu wa madawa ya kulevywa, au labda viongozi wa dini kuhubiri uongo na kuuza kwa watu, au labda wanasiasa kupora uchaguzi kwa rushwa na vitisho...

Maskini Julius! alidhani kwamba marais wataomfuatia watakuwa na uwezo wa kushinda 'hofu na tamaa' kama yeye alivyoweza kufanya hivyo mwaka 1984, lakini alishindwa kuelewa kwamba wenye uwezo wa kushinda tamaa na hofu idadi yao ni sawa na tone kwenye bahari.

Power Consolidation and Strategies
Kwa upande wa wanasiasa ambao nguvu yao ipo kwenye mifumo ya kiushindani ya kiutawala, power consolidation strategies zinaweza kuwa za aina mbili kwa mtizamo wangu

1. Kuchapa kazi haswa na kuongoza kwa weledi, kiasi kwamba wananchi waliowengi wanakosa dosari, na hata ikifika uchaguzi, uhakika wa kushinda ni mkubwa.

2. Kuondoa vihatarishi vinavyotishia nguvu ulonayo 'Eliminate threats in cold blood'.

Strategy number 1, imewezekana kwenye nchi zenye Demokrasia za hali za juu sana, kwa hapa Africa labda South Africa. Kwa nchi magharibi ambazo mifumo yao ya kisiasa imechimbukia ndani ya falsafa za 'Liberty' ambazo sikuzote inaweka mbele uhuru wa raia wake, strategy number 1 imejeuka kama key strategy kwa wanasiasa kujikusanyia nguvu. Hii inapelekea mgongano wa hoja na hoja zikijibiwa kwa hoja.

Strategy number 2, 'Elimination of threats in cold blood' ndo ambayo naona imeshamiri kwenye nchi zinazojitafuta kama Tanzania ambazo, kutawala kwa kufuata misingi ya katiba ni jambo linalotegemea utashi wa kiongozi na sio sheria na katiba zilizopo. Msingi wa hii strategy ni kutengeneza hofu. Hapa hoja haijibiwi kwa hoja, bali hoja inajibiwa kwa kutekwa na kupotezwa.

Errors in Judgement
Napo pia kwenye strategy ya "Elimination of Threats" ili uweze ku consolidate power, kuna makosa fulani ambayo yanaweza kutokea. Moja ya makosa hayo yanaanzia kwenye ku define framework ya "Nani haswa ni kitisho?, kwa namna gani anatishia?, na je, kuna ushahidi gani anatishia consolidation of power?

Kwa maana yake, "Strategists wa zoezi la consolidation of power" wanaweza kuwa na framework ambayo imetokana na ufinyu wa wao kufikiri na ikapelekea kwamba ukajikuta umekuwa defined kama 'threat'.

Kwasababu unakaa unajiuliza maswali yafuatayo
Mtu anayekosoa serikali kwa hoja zisizo na mushikeli anaambia kwamba yeye ni threat?
Ukisema dola imepanda na si ni kweli imepanda, basi directly unageuka kuwa threat?
Ukiwa kiongozi wa chama cha upinzani chenye nguvu basi unajeuka kuwa threat?

Basi tutakuwa nchi ya watu wasiohoji chochote kwasababu tayari ukitaka kusema basi unaonekana wewe ni kitisho kwenye 'consolidation of power of whoever it is"? Sasa mawazo mazuri ya kuendeleza nchi yatakujaje bila mgongano wa hoja??

Namefikiria sana logic ilotumika kukatisha maisha ya Mzee Mohamed Kibao na kwa haraka ikanipelekea kuconnect dots kwamba yule mzee alikuwa mstaafu jeshini, kwamba alikuwa kwenye kitengo cha intelijensia ya jeshini wakati huo, na kwamba kwasababu alikuwa chadema kwenye secretariat, basi yawezekana labda anajua mambo kadha wa kadha ambayo yanatishia "Consolidation of power" ikizingatia CHADEMA imeonesha kujiimarisha sana kwa wananchi kwa hii miaka miwili, kwahiyo wanakuwa ni direct threats kwa yeyote mwenye kutekeleza "power consolidation strategy". Hiyo nadhani ndo thinking process ya watekaji ambao wamejaa hofu mioyoni mwao na wamekosa waledi wa kazi yao, ni vilio na uharibifu, unapotaka ku "consolidate power" kwa kutumia watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri.

Nikihitimisha kwa niliyosema hapo juu, tafsiri ya haya mambo yanatendeka kwa sasa ni kwamba "HAKUNA ALIYE SALAMA" Na hii ni kwa sababu iliyowazi kwamba, wanaotekeleza hili zoezi nililoliita 'Power consolidation strategy' wameshajidhihirisha kwamba framework ya zoezi lao, lipo prone to making judgement errors, ya nani ni threat nani sio threat. Unaweza kuwa wewe ni mtu mkimya kwenye jamii na haujishughulishi na siasa, lakini ukajeuka kuwa suspect kwamba, yumkini unaweza kuwa threat, na ukaishia kupotezwa kama tunayoyashuhudia kwa mifano

Hii ndio hatari nayoiona na namna ya kuliangalia hili jambo. Tujilinde sana ndugu zanguni, 'hofu na tamaa' imetamalaki kwenye mioyo ya watawala, ni uharibifu tu na machukizo.
 
Terminology hapa ni mauaji tu,hayo mambo mengine ni porojo
 
Siku utakapokutana na watu,uliyowauwa, Mungu atusamehe,Maisha yenyewe Haya mafupi,umeishi sana kwa kutegemea nguvu zako, miaka 70, ukiishi sana zaidi ya Hapo unawategemea wengine wakusaidie
 
Sasa roho zao zimefurahi nafsi zao zimeridhika kukuona ukiwa mwili mtupu usio na pumzi,Hujawahi kuwatendea baya lolote,kosa lako ni kuwa mwanachama wa CHADEMA.

Tutakutana tena Mbinguni Kamanda.
Hiki kifo kimeniuma sana.
 
Back
Top Bottom