Jicho la mwewe liko namna hii. Pongezi mwenye nalo!

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Kipindi hiki cha Usajili VPL....

Kuna watu wameingizwa sana mkenge. Pongezi zimfikie mwenye jicho hili.

Mchezaji akimaliza mkataba na timu yake, hili linafanyika. Tunakupa 50/- wale wanasema 70. Sasa hawa wa 50/- wakiona hawana uwezo wa kufikia 70, wanaona bora wafanye mchezo mchafu.

Moja. Tujifanye tunaongeza dau kujidai tunamhitaji mchezaji aliyemaliza mkataba, (wakijua tosha kuwa na upande wa pili watapanda). Basi, ikawa hivyo mpka mmoja akafika 130 ikiwa hali halisi wale wengine wanalengo la kukomoa upande wa pili ili uingie gharama zisizo za lazima. Huu mcheza ni kama kukomoana vile, wakijua kuwa ukiishiwa mpunga itawapa wao nafasi kuweza kutamba kisoka.(zingatia pia suala la Salary Bill sio tu suala la gharama za usajili).

Mbili. Namna nyingine, ngoja tuongee na mchezaji aliyemaliza mkataba ili akajifanye kuwa sisi tumeweka kumeza kiasi kikubwa kidogo kuliko kile kilichoko upande wa pili.

Mchezaji anaenda upande wa pili na wakala wake, wanasema wenzenu wameweka mezani bei 100/- kwanini nyie msipande kidogo. Upande huo utasema tuonyeshe mkataba huo, mchezaji na wakala wake wanarudi klabuni kuchongesha mkataba feki (wa kuonyesha tu). Baada ya kuuona wao wanapanda tu. Mwisho wa siku wanagonga kwenye high price. Dili la huyu mchezaji linakamilika kwa msaada wa klabu yake pendwa.
Kumbuka hii njia ni ile ambayo klabu ya mchezaji ina mchongo kidogo sana hata kushindwa kushindana na upande wa pili.

Ni mwendo wa kukomoana tu, Michezo michafu sana.

Note:
Kama hujaelewa, Kaa kimya!
 
Yule wa yanga kwenda simba?

Ina maana manji hajakoma kutumia?
 
Kwanini nikae na kinyongo wakati sijaelewa bhnaa,,, njoo uelezee ueleweke aisee
 
Kipindi cha usajili nahisi akili za viongozi wa timu zetu huwa zimefyatuka.. Vinginevyo basi mara nyingi huwa kuna kitu nyuma ya pazia
 

What a pity! You are loosers
 
Hela haijawahi kukomolewa hata siku moja, kinachoangaliwa ni kiwango cha mchezaji kama kinaweza kuisaidia timu apewe kiasi chochote anachotaka. Manji aliwahi kutoa mil 100 bure kabisaa watu wakaingia kucheki gemu hakuna aliyesema kama amejikomoa!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…