Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Mataifa yanayoheshimika duniani kwa kuwa na intelejensia ya kiwango cha juu duniani kwa sasa ni Marekani, Urusi, Israel, China na Uingereza.
Intelejensia ya kiwango cha juu katika mataifa haya zimeyawezesha mataifa haya kuweza kuzimudu kwa kiwango cha juu sana siasa za dunia (geopolitics) na kuyafanya mataifa haya yaendelee kuwa juu kiuchumi.
Katika machafuko yaliyotokea na yanayoendelea Msumbiji taifa lililoathirika zaidi ni CHINA. China kama marafiki wakuu wa chama cha FRELIMO waliwekeza sana nchini Msumbiji.
Vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi wa Msumbiji zimeathiri sana biashara za wachina maana wananchi walichoma maduka ya wachina na kuharibu mali zao wakiamini kuwa China imeshiriki kuifanya Frelimo kuiba uchaguzi.
Soma, Pia: Wachina wanafanya nini kwenye Uchaguzi wa CHADEMA?
Tukio la CHINA kukubali mualiko wa CHADEMA na kwenda kwenye mkutano wao Mkuu inamaanisha kuwa Idara ya Intelejensia ya CHINA imeishauri Serikali ya CHINA kuanza kuwa marafiki na vyama pinzani vya Afrika ili kulinda uwekezaji wao na maslahi yao.
Kwa watu wasioona kwa jicho la 3 wanaweza kulichukulia lile jambo kama jambo la kawaida sana ila kwa wanaojua kuwa CHAMA CHA MAPINDUZI kinategemea kwa asilimia zaidi ya 70 kwa CHINA ili kuendelea kuongoza Tanzania wataanza kuamini kuwa hali ya chama cha Mapinduzi inaanza kuwa mbaya nchini Tannzania.
Inawezekana huu ukawa ujumbe kuwa Chama cha Kikomunisti na China kipo tayari kufanya kazi na CHADEMA endapo itachukua nchi.
Sasa naelewa kwa nini kuna hofu kubwa CHAMA CHA MAPINDUZI baada ya mkutano mkuu wa CHADEMA na ushindi wa LISSU.
Mwaka 2025 unaweza kuja na suprise ya karne nchini Tanzania.