Jicho la tatu la tukio la Harmonize Mkapa stadium

Jicho la tatu la tukio la Harmonize Mkapa stadium

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Jumapili iliyopita wananchi walikua na Jambo lao pale Mkapa stadium,.wasanii kadhaa waliimba mbele ya wananchi.

Lakini alipokuja harmonize alijaribu na akafanikiwa kwa asilimia nyingi kuonesha utofauti na kuthubutu kuipamba onesho lake,japo kunamakosa kiasi yalijitokeza.

Tukiliangalia tukio lile tunaweza lipeleka kwenye uwanja mpana zaidi hasa kwenye maisha yetu yakibiashara,au kwenye maamuzi furani magumu.

Tulichukue wazo la biashara au wazo la maamuzi Kama wazo lake lakutumia kamba kuingia kwenye onesho lake.

Je, hakuwaza kudondoka toka juu mbele ya kadamnasi ya watu,hivyo ndivyo utakavyowaza kula hasara ukianza biashara yako,au kutoeleweka utakapochukua maamuzi furani.

Lakini akachukua uamuzi wakutumia kamba hiyo na akaingia tukamuona,Kama utakavyoamua kuanza biashara yako au utakavyoanza kuamini maamuzi yako.

Kisha alipoingia alionekana Kama pumzi kumuishia lakini aliendelea kusogea taratibu Hadi katikati ya uwanja pale.

Hiyo inaweza kuwa sawa na wewe kwenye biashara yako,unahisi wateja hakuna,au unahisi Kama biashara yako ndogo au mbaya Ila amua kuendelea kuvumilia kuangalia njia.

Lakini pia baada ya kufika pale inaonekana hapakua na mawasiliano mazuri na washika kamba wake akaonekana kudondoka chini (tukio ambalo watu wengi wamelishikilia)

Hi ni sawa na wewe great think mwenzangu unapoendelea kupambana yawezekana wafanyabiashara wenzako au wale watu wako wakaribu wanapoamua kwenda tofauti na wewe kwa namna yoyote ile ,au kwenye maamuzi yako huenda wale watu wako wakaribu wanaamua kukukacha Ila endelea ili kutimiza lengo lako.

Sasa Ni hitimisho baada ya kitendo Cha kudondoka kwa muda alitulia Bila kupotea kwenye lengo kisha akaja kutupatia onesho zuri na kutuonesha yeye ni jeshi ,akapokelewa vizuri.

Hivyo Basi hata unapopitia kwenye wakati mgumu isiuwe Nia ya uthubutu,isiuwe lengo pambania kufikia.

Amini zaidi kwenye malengo,amini zaidi kwenye kufanikiwa,amini zaidi kwenye vyema.



kelphin kepph
 
IMG-20200831-WA0002.jpg
 
Maandishi meengi maana hamna

By the way alimaanisha yanga iliyodondoka msimu uliopita ilisaabishwa na walioshika kamba kina morson na wenzake hivo isiwe chanzo cha wanayanga kukata tamaaa Bali tusonge mbele maana yanga bila kina morson yawezekana,,,,


Sasa wewe hayo ya biashara sijui yanaingiliaje hapo.
 
Back
Top Bottom