Sewando MP
Member
- Jan 25, 2014
- 56
- 116
JOCHO LA TOFAUTI: UWEKEZAJI WENYE TIJA KATIKA SOKA LA TANZANIA.
Uwekezaji katika Sekta ya michezo ya kubashiri Tanzania (Gaming/Betting Indutry) umekua kwa kasi sana ndani ya miaka 7. Kuna zaidi ya Makampuni 25 ya kubeti Tanzania na yanazidi kuongezeka kwa kasi sana.
Lakini, moja ya kilio cha makampuni haya ya kubashiri, ni asilimia kubwa ya marejeshi ya kodi itokanayo na faida wanayotengeneza. Mfano: Mbali na Winning Tax 10% ambayo hutozwa kwenye Sports Betting, Pia kuna;
1. 10% ya GGR itokanayo na faida wanayopata kwenye Sports Betting.
2. 25% ya GGR itokanayo na faida wanayopata kwenye Casino Betting.
3. 10% ya GGR itokanayo na faida wanayopata kwenye Virtual Games.
4. 05% Levy itokanayo na faida wanayopata kwenye Virtual Games
Kwa mchanganuo hoo, unaweza kuona namna gani kulivyo na utitiri mkubwa wa Kodi katika Sekta ya Michezo ya kubashiri. Na hapo bado kuna Leseni za kuendesha shughuli za michezo ya kubashiri kila mwaka, ambapo:
1. Sports Betting Licence ni Dollar 30,000 na
2. Casino Betting Licence ni Dollar 40,000.
Na mpaka sasa, bado Serikali inatafuta namna ya kuendelea kuyakamua kodi makampuni ya kubashiri, maana yanaona kuna hela nyingi sana.
Lakini, Ukitazama kwa jicho la tofauti, kuna fursa ambao laiti kama Serikali yetu ingeona, basi ni fursa nzuri sana ya kuendeleza Soka la Tanzania.
Kama ambavyo uwekezaji katika Sekta ya madini ulivyo na sera ya kuwepo ulazima wa kuwekeza katika maendeleo ya eneo husika ambako uwekeza unafanyika, basi katika Sekta ya michezo ya kubashiri inawezekana pia.
NINI KIFANYIKE?
Ni wito wangu wa Serikali, kupitia Wizara ya Fedha (Waziri, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba) na Wazara wa Utamaduni, Sanaa na Michezo (Waziri, Mhe. Mohamed Mchengerwa) kuja na Sera Maalum ya kutengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji katika michezo ya kubashiri kwa;
1. Kupunguza utitiri na asilimia kubwa za Kodi.
2. Kila Kampuni ya Kubashiri iwekeze moja kwa moja kwenye soka la Tanzania, katika moja ya maeneo;
(a). Kudhamini Timu angalau 1 ya Mpira.
(b). Kuendeleza Viwanja vya Michezo
Nina uhakika, ndani ya miaka 5 hadi 10;
1. Hakutakuwa na Timu za Ligi Kuu zinazolia lia njaa na kushindwa kulipa mishahara wachezaji na wafanyakazi
2. 50% ya Timu za Mpira zitakuwa na Viwanja vyao vya Mpira.
3. Tutakuwa na Viwanja vya Michezo vyenye hadhi fualani
Haya ndio mambo ya msingi sana ambayo wenye dhamana na Soka la Tanzania na Serikali wanatakiwa kutupia macho, na sio kuendelea kukwapua kidogo wanachokipata Makampuni ya Kubashiri Tanzania. Sekta ya Michezo ya Kubashiri Tanzania ni zaidi ya Gaming & Entertaiment. Tukitengeneza mazingira rafiki, basi tutafungua milango katika Uchumi, Ajira na Maendeleo ya Soka la Tanzania.
#AmuaUshindiWako #Dakika10AuDabo #SlotsMarathon #DakaUzi #SportsBettingTanzania #CasinoPesa #BestBettigTZ
Kwa Leo niishie hapa, Kama kuna mwenye maoni zaidi, Karibu tupaze sauti pamoja.