Emmanuel Mkwama
Senior Member
- Apr 24, 2013
- 166
- 124
DP world ni kampuni kutoka Dubai,yenye kumilikiwa na waarabu chini ya Dubai Emirates.
Kiukweli tangu imeingia nchini imeleta shida na kusababisha mpasuko nchini. Vyama vya siasa vimetofautiana, pia mjadala wake imeleta mpasuko wa kidini baina ya waislamu wachache na wakristo wachache. Pia imewainua wanaharakati tofautitofauti katika maeneo tofauti. Pia imefikia hatua kila rika linajadili swala la DP world si mtoto wala wakubwa.
Faida na hasara za mjadala wa DP world kwa vyama vya Siasa.
Kwa upande wa CCM ni kupoteza na kuendelea kushuka zaidi kisiasa kivyovyote vile.
Kama wakisema waendelee na DP world pasipo kusikiliza Makelele ya watu, wategemee kusababisha mpasuko zaidi na uwenda ikaleta shida ya machafuko nchi. Hii imesababishwa na elimu na makelele ya taasisi mbalimbali kuliongelea swala la DP world na kuendelea kutolewa elimu kwa kada mbalimbali nchini.
Pia wakisema waachane nao DP world hii itawapa wapinzani haki ya kuendelea kuikosoa serikali kwa kushindwa kuwa makini na kuwaongezea topiki majukwaani dhidi ya ubovu wa serikali na chama kilicho unda serikali.
Kwa upande wa upinzani na wanaharakati wao hawana cha kupoteza zaidi ya kuwaimarisha katika mapambano yao. Kusema ukweli wamepata pakuibana serikali kupitia inshu ya DP world.
Mtaji pekee walionao upinzani ni nguvu ya umma, ndiyo maana nasema wao hawana cha kupoteza. Ni kwa jinsi gani wataweza kuwaunganisha watu na kupaza sauti ili kuwashtakia serikali kwa wananchi.
Ahsanteni sana,pia karibuni katika kunikosoa.
Cc. Pascal mayalla, mshana Jr. Faiza fox, MS