gasto genaro
JF-Expert Member
- Oct 15, 2014
- 780
- 554
Na: Gasto Di Genaro
Ukimwondoa Sir Alex Ferguson, José Mourinho ndio kocha niliyetokea kumhusudu kupita maelezo katika maisha yangu ya ushabiki wa soka.
Mourinho amepata kibarua chake kama meneja wa Man Utd mwaka huu 2016. Kwa hakika, nilipata furaha hadi utosini nilipozipata habari za meneja huyo kapata kandarasi Man Utd.
Mourinho akiwa wa Man Utd, ameianza ligi ya EPL vizuri sana kwa kupata ushindi wa mechi tatu mfululizo, ukiacha ile ya ngao ya hisani ambacho Utd ilimcharaza vibaya mno Leicester city kwa goli 2-1
Lakini ndani ya siku nane zilizopita, Man Utd imekua na matokeo mabovu, na siyo matokeo mabovu pekee, bali na mpira mbovu sana uwanjani..
Ubovu huu wa matokeo ya Manchester United, naweza kusema umesababishwa na sababu mbili kuu; nazo ni Kocha na Uzembe wa baadhi ya wachezaji.
*Kocha*
Mourinho ni kocha mzuri sana, na uzuri wake unatokana na mazuri mengi aliyokwishayafanya.. Japokua ana ubora huo, kuna mambo kadhaa ambayo yamemfanya timu yake ifeli kwa mechi tatu mfululizo..
Ifike pahala Mourinho atambue ya kwamba, soka linabadilika, na mifumo ya soka inabadilika. Kitendo cha Mou kutegemea mpira wa Physic zaidi na kuutelekeza mpira wa creativity kwa kiasi kikubwa, ndicho kilichomfelisha kwenye mechi tatu mfululizo
Mourinho kwa sasa inambidi abadili mfumo na mbinu ili timuicheze kwa ubunifu zaidi na siyo nguvu. Mpira huo wa ubunifu hautopatikana kwa kumtumia mchezaji kama Fellaini,, bali wachezaji kama Carrick, Herrera, Mata and the likes.
Selection ya wachezaji kwenye Mechi tatu zilizopita, pia kimemgharimu Mou. Kitendo cha kumwanzisha Lingaard na Mkhitaryan mechi ya Man city, hakikua sahihi kwani walikua wagonjwa na ndo maana hawakufanya chochote chanya kwenye ile mechi..
Pia kitendo cha kumtegemea Fellaini kwenye moyo wa kiungo, ndiyo kunamgharimu Mourinho mara dufu. Fellaini ni mchezaji mzito, asiye na speed wala ubunifu. Pia Fellaini na Pogba wote ni box to box Midfielders yaani, wanalenda kupanda kushambulia na kuliacha eneo la kiungo wazi... Kuwachezesha viungo wa aina hii kwa pamoja, kunamgharimu timu. Kilichomfungisha chelsea ndo hicho hicho cha kutumia viungo wa aina moja i.e Kante na Matic Halafu Fabregas bench(no creativity). Kwaiyo Fellaini uzito wake ule na kukosa speed, pindi akikutana na kiungo mwenye speed(Fernandinho) anashindwa kuhimili kasi.. Kwahiyo Mou kumtegemea Felaini kumemcost.
Pia kitendo cha kuendelea kugandamana na Rooney, kinaigharimu timu. Nadhani mou aangalie namna ya kumweka Rooney bench. Kuendelea kumpa nafasi ni kosa kubwa.
Kwahiyo, selection ya line up ya wachezaji kama hao niliowataja, kumemwangusha mou kwenye mechi tatu zilizopita.
New Mourinho
Mourinho anadai kuwa anataka kuwa new Mourinho. Nahisi hapa panamfanya timu idorore zaidi. Mou wa sasa siyo yule wa kugomba timu ikizingua. Mou anatakiwa awe mkali, mchezaji ukicheza chini ya kiwango bench likuhusu. Mou wa sasa anawachekeachekea wachezaji.. Aache hilo suala na awe mkali timu itacheza poa.
*Wachezaji*
Kuna baadhi ya wachezaji wa Man Utd kama wameyasahau majukumu yao, na badala yake wanarukaruka tu uwanjani badala ya kufanya wanachotakiwa kufanya. Rooney amekuwa akicheza chini ya kiwango, Rooney huyu wa sasa, anapiga pasi fyongo nyingj, anapoteza mipira mingi, na pia haiungi timu kutoka kwenye moyo wa kiungo hadi safu ya ushambuliaji.. Huyu anatugharimu karibu asilimia 50 ya form yetu mbaya..
Fellaini kama nilivyosema hapo awali, hastahili kuanza, anarukaruka na kukimbia kama kaliwa funza miguuni, na urefu ule hata set pieces anashindwa kuziunga na matokeoye zinadondokea kwa maadui.. Kiungo gani hana ubunifu? Kwa soka la sasa, tunahitaji kiungo mwepesi(hapa utagundua kwann Guardiola amempiga chini Toure Yaya). Fellaini anampa kazi nzito sana Pogba maana utakuta pogba huyo huyo akabe, huyo huyo apandishe timu... Nadiriki kusema kwa sasa Fellaini ni Liability(Mzigo)
Martial. Huyu wa mwaka huu siyo yule wa mwaka jana. Martial anarukaruka tu siku hizi. Nadhani ana tatizo la kisaikolojia. Akalishwe chini, apigwe session ili asahau matatizo yake arudi form.
Way foward :
Mou aache kuwatumia Fellaini na Pogba kwenye Moyo wa kiungo. Partnership hii haitokuja kuleta consistent possitives. Pogba anahitaji achezeshwe na Holding /Defensive Midfielder kama Schneiderlin / Carrick / Schweinsteiger.. Lakini zaidi Morgan Schneiderlin kwasababu, huyu ata offer long term partnership with pogba.. Carrick na Schweinsteiger siyo wa kuwategemea sana maana ni wachezaji wa wodini.
Ni wakati wa kuacha pia Mazoea na kumpiga Rooney Bench na kuweka wachezaji kama Mkhitaryan, Mata, Herrera.
Martial pia asipojirekebisha, nafasi yake ichukuliwe na Memphis Depay.
Kama ningeambiwa nimshauri Mou line up, basi ningemshauri hii
De gea
Valencia Smalling Bailly Shaw
Schneiderlin
Pogba Herrera
Rashford Mkhitaryan
Ibrahimovic
Subs: Memphis, Romero, Carrick, Rooney, Mensah etc
_______________________________
Gasto Di Genaro
Shabiki wa kufa wa Man Utd, Simba Sc, Rvp na Memphis Depay