Jicho Pevu na Angavu

Harald Dad

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2016
Posts
353
Reaction score
263
Napenda kuwasalimu wana JF wenzangu habari za weekend na pia poleni sana kwa uchovu wa pilika pilika za wiki nzima.
Bila kupoteza muda naomba nije moja kwa moja kwenye mada;

Leo naomba niwaangalie dada zangu kwa jicho pevu ambao wanakaa tu hawataki kujishughulisha huku wakijinasibu eti wanasubiri kuolewa na mwanaume mwenye mafanikio,

Leo nimeona nisipite hivi hivi niwashauri dada zangu waachane na ndoto hizo za mchana kwani kuna misemo mingi inasemwa, ukiwemo ule , "Kila mwanaume mwenye mafanikio nyuma yake kuna mwanamke" sasa kwanini wewe dada umekaa tu kusubiri kuhujumu haki za mwanamke mwenzio?
Je unamjua mwanamke aliyechuma na huyo mwanaume hadi kufikia hayo mafanikio?
Ni kwa nn wewe dada usianze sasa wakati ukiwa na nguvu zako kujenga na mwanaume wako kuanzia ngazi ya chini na hatimaye mafanikio? Unakubalije leo dada kukubali maisha ya utumwa kisa utajiri wa mtu.

Leo hii dada ety anamilikiwa lipstick na wanja amebweteka na ndoto za kuolewa na mtu mwenye mafanikio, wasichana wenye ndoto kama hizo kweli nasema kutoka rohoni wanahitaji maombi ili shetani aliyewafunga aweze kuwafungulia pingu walizofungwa,

Dada zangu naomba wale wenye akili na mtazamo kama huu wakubali kuwa huo ni ujinga uliotukaka.

ASANTENI SANA NA NAOMBA KUWASILISHA HOJA
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] wanja na lipstick[emoji140] [emoji140] [emoji134]
 
Wapumbavu sana hawa ngoja wazidi kulizwa kwenye ndoa maana wanalaza akili zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…