Jicho toka Tanzania : Kwa nini ugaidi nchini Kenya

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
January 20, 2019

Ni nini chano cha ugaidi nchini humo? Je, Kenya itaweza kutokomeza ugaidi kwa kwa asilimia 100. Nini kifanyike. Ungana na wachambuzi hawa watakaokupa mwanga na majibu ya maswali uliyonayo juu ya Ugaidi nchini Kenya.

Wataalamu wa nyanja ya siasa Bw. Abdulkarim Atik na historia Bw. Francis Daud wanachambua hali hiyo ya nchi jirani :

Source : Azam TV
 
Marekani pamoja na rasilimali zao zote na jeshi lenye silaha na tecnology ya kutosha wameshindwa kumaliza ugaidi.
 
ni kitu kinacho changanya sana akili ukifikiria sanaa na kugundua our EAC no longer a safe place mamia ya raia wanapoteza maisha ktk matukio mbalimbali ya kujilipua au mashambulizi ambayo yanapangiwa na kuratibiwa na baadhi ya wananchi waliopo ndani ya EAC
 
Marekani pamoja na rasilimali zao zote na jeshi lenye silaha na tecnology ya kutosha wameshindwa kumaliza ugaidi.
Hahahaha, kwasababu wamarekani wanauliwa, kwahiyo ni sababu nzuri kwa wakenya kuchinjwa kama kuku, endelea tu kuchinjwa na endeleeni kujiliwaza kwasababu mabwana zenu nao wanachinjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna nchi inayoweza kutokomeza ugaidi kwa asilimia 100% ikumbukwe kwamba hawa tunaoita magaidi, kunao wanawaona kama mashujaa, na hilo tumeliona hata humu JF, kuna baadhi ya Watanzania waislamu na pia nilishangaa kuona baadhi Watanzania Wakristo pia walikesha humu wakisifia na kuchekea wakati mauaji yalikua yakiendelea. Hivyo ina maana magaidi hawawezi kutokomezwa kwa mtutu wa bunduki, hata ukiua wangapi, bado kuna wanaozaliwa na kuaminishwa hizo itikadi.

Kinachowezekana ni kupunguza matukio ya kigaidi, na hii inabidi juhudi ziongezeke za kuwahusisha jamii haswa ya Wasomali, kuwaonyesha upande wa pili wa shilingi, manufaa ya amani na nia njema, ukishinda vita kwenye mioyo ya hawa Wasomali, utakua umepunguza ugaidi pakubwa maana watatoa ushrikiano mkubwa, ikiwemo kuwafukuza wageni waliojaa kwao ambao wanahusika pakubwa kwenye ugaidi, kunao magaidi wakutoka mataifa tofauti kule Somalia, wakiwemo mamia ya Wakenya, Watanzania na hata Waarabu.

Changamoto za ugaidi Kenya sio za kawaida, hakuna nchi Afrika yenye changamoto kama za Kenya, kila mtu anayejadili kuhusu ugaidi Kenya lazima atulie na kuwaza haya hapa
- Wakenya wenye asili ya Kisomali ni zaidi ya 800,000
- Hawa hauwezi kuwatofautisha na ndugu zao kule, ni kama Mmaasai wa Kenya avae shuka na kutembea barabara za Dar, huna jinsi ya kumtofautisha na Mmaasai wa Tanzania, nimewahi kuwaona Wamaasai wa Tanzania ambao Kiswahili ni changamoto kwao, tena pale Morogoro.
- Wakenya hawa wenye asili ya Kisomali tumeingiana nao yaani hadi tumewahi kuwa na mkuu wa majeshi mwenye asili ya Kisomali. Kwa hivyo hauwezi ukaamka na kukurupuka uanze kuwabagua.
- Wamemiliki mkoa mmoja mkubwa, ambao upo kwenye mpaka na Somalia
- Mpaka wa Kenya na Somalia ni pori tupu na jangwa, ni vigumu kuendesha shughuli za usalama pale, japo serikali inawekeza kuweka ukuta, lakini kwangu mimi na kwa maoni yangu hayo ni mawazo ya kipumba tu

Kama nilivyosema hapo juu, njia rahisi ya kupunguza ugaidi Kenya ni kuwahusisha jamii, haswa hawa Wakenya wenye asili ya Kisomali, kuwafanya wawaone wale kama magaidi na sio mashujaa, maana wanajificha ndani yao, kuendelea kuwahusisha kwenye ujenzi wa taifa na kuchochea uzalendo, na pia kule Somalia, KDF wazidishe uhusiano mwema na raia walio na mtizamo wa kati.
Lakini pia viongozi wa dini wahusishwe pakubwa kwenye kuhubiri amani, maana na wao ndio wamekuwa mwiba, humo kwenye ibada ndipo wanahubiri chuki za kidini na kusababisha waumini kuiva na kuwa tayari kulipuka.

Hii ramani hapa chini inaonyesha mikoa ya Kenya, mkoa namba tano unaishi hao Wakenya wenye asili ya Kisomali na ndio mpakani mwa Kenya na Somalia, hivyo kila siku wanahusiana kwenye mambo yao, ni vigumu kuwatenganisha, ni kama Wamaasai Wakenya na Watanzania, wale huwa na undugu ambao imekua vigumu kuwatenganisha hata ukikamata ng'ombe wala nini, kila siku wanapishana kwenye mpakani na kusaidiana kwa hali na mali.

https://upload.wikimedia.org/wikipe...ed.svg/300px-Kenya_Provinces_numbered.svg.png
 
Umejitahidi kuweka sawa. Lakini kwangu naona kukaa KDF Somalia ndivyo moto unavyoongezeka!

kama nitakuwa nakumbuka vizuri.
ugomvi wa al Shabab na Kenya ulivyoanza.
NI BAADA YA AL SHABAB KUWA TEKA RAIA WAWILI WA KIGENI NA KUWAUA.
sikumbuki mwaka.ila ni miaka hii ya 2000.
kuanzia HAPO NI VISASI,VITA,,NA MAUAJI.
vita hivi vitaisha kama wakiamua kukaa chini
NA KUMALIZA TOFAUTI ZAO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom