Jide na Gadner acheni hizooo!

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Mhhhh wamependeza sana sana kwanza napenda kuwapa hongera baada ya hapo nimeshangaa mmejitahidi kuelzea vyakula mlivyokuta na picha za menu...mbona hamjawahi kupiga picha zile pweza za feri jamani na umuhimu wake katika jamii hamuoni mnatangaza soko la watu wakati kwenu wanakimbia....haya Zanzibar nako ndio hivyo wamarekani no.

Asalaleh!

Mwisho nawapongeza maisha na raha wajipe jamani msisubiri kupewa na kampuni ama mashirika

=====================


SAFARI YA KUELEKEA JELA ALIPOFUNGWA MWANAMAPINDUZI WA KWELI COMRADE MADIBA



Vivutio mbali mbali ambavyo vipo Waterfront ni pamoja na huyu mtu wa Gold ambae akisimama hatingishiki unaweza ukadhani ni sanamu ila ukimtupia pesa kwenye ki box kidogo kilichopo pembeni ndio ana swing kama ishara ya kushukuru




Kuna duka linalouza suvenir mbali mbali za Mandela zikiwemo tshirts, keyholders, magnet za kwenye fridge n.k mi nilikamata ya kwangu...size zote hazikunitosha ikabidi ninunue ya size ya watoto wa miaka 7-8 ndio ikanikaa...kazi kweli kweli


Mlango wa kuingilia sehemu ya kupandia Boat kuelekea Robben Island,(Nelson Mandela GetAway)




Huku nako kumbe mpaka kuna cha kiswahili nimepanga nitarudi kukila




Manka na Mtu wa dhahabu



Manka na mtu wa silver




Berna na Gardner kuelekea katika boat (Sikululekhile)




Mkiwa nje ya boat kabla ya kupanda mnapigwa picha wakati wa kurudi mnazichukua kwa kumbu kumbu, kama bongo vile




Tuko kwenye foleni kabla ya kuingia kwenye boat, sio unampita tu mwenzio ukikuta amesimama...na utake kuhudumiwa wewe kwanza huku wa kila sehemu unapanga foleni



Sio lazima kungoja wadosi wakuuzie, kama wanazingua sio mbaya kwenda front mwenyewe..African Marimba Band wanapiga na kuuza Cd's zao wenyewe hapo hapo, pia watu wanaopendezewa wanawapa chochote kila wanapopita




Duka la Suvenir za Comrade Madiba, ...wadau wachache nimewachukulia zawadi nikirudi tu nawacheki msikonde





Lango kuu la kuingia jela alipofungwa Comrade Nelson Mandela miaka 18 kabla ya kuhamishiwa magereza mengine mawili tofauti ambapo alikamilisha miaka 27.


Gereza la Posmo alifungwa miaka 7 na Gereza la Paarl alifungwa miaka 2



Moja kati ya watu waliokuwa Tour guide wetu ambae alifungwa miaka 2 katika gereza la Robben Island na sasa ndio anawaelezea watalii vizuri kuhusu yaliokuwa yanajiri humo ndani...


Aliwahi kuchapwa viboko mwili mzima. Lakini alipojaribu kuwaonyesha wahusika wakuu na doctors kuwa ameumizwa sana hawakujali na walikuwa wanamfukuza na kumuita muongo, na kudai kuwa ni stress tu za yeye kutokulala usiku, huyu guide ni moja kati ya wanaoitwa coloured (halfcast)
Alipona kwa kudra za mwenyezi MUNGU

Kumbukeni gereza hili walikuwa wanafungwa watu weusi, Asians na Coloured tuuu, hakuna mzungu aliekuwa anafungwa humu.
Pia wanawake walikuwa hawafungwi humu
Ubaguzi ulikuwa wazi wazi, kabla Comrade hajaachiwa na kuibadili Afrika Kusini



Moja ya Picha za kumbukumbu zilizopo kwenye kisiwa hicho, ya wafungwa waliokuwa wakiingizwa huku wamefungwa minyororo miguuni na mikononi tayari kwa mateso.

Mkono wa kulia katikati ni askari weusi waliokuwa wanapewa mikuki na rungu tu kwaajili ya kuwalinda weusi wenzao wasitoroke,
Wakati askari wa kizungu walikuwa na bunduki,
Askari mweusi hakuruhusiwa kuwa na bunduki



Tukiwa kwenye Bus kuelekea gereza kuu hii ni moja ya barabara za ndani ya gereza hilo




Kulikuwa hakuna vitanda gerezani humo wafungwa wetu walikuwa wanalala kwenye matandiko kama haya, na hapo juu pichani ni Tour Guide mwingine akituelezea habari zote kuhusiana na gereza hilo




Menu ya chakula ilikuwa kama hivi, Coloured na Asians walikuwa wanapewa chakula cha afadhali, na Chakula cha wabantu (watu weusi) kilikuwa kibaya kuliko vya wote.


Soma Menu vizuri utaona, upande wa kushoto ndio chakula cha Coloured na Asians na upande wa kulia ni chakula cha mtu mweusi, gerezani humo



Watalii mbali mbali hufika gerezani hapo kutembelea, na gereza limefungwa kuwa kama gereza limebaki kuwa kivutio cha kitalii ambacho kinaingizia South Africa pesa za kuisaidia nchi.




Hiki ndicho chumba alichofungiwa Comrade Nelson Madiba Mandela (Our Miracle Father)

Tanzania pia tulikuwa nae wa kujivunia Our Miracle father J.K Nyerere



Hapa ndipo alipokuwa akijiegesha, maana humu huwezi kuita ni sehemu ya kulala wala kujipumzisha, unaweza ukalia mwanzo mpaka mwisho wa safari unapokwenda kisiwani humo.

Ukielezewa story ya kusikitisha kama hii



Captain akishuhudia jela aliofungwa Madiba miaka 18, kabla ya kuhamishiwa jela zingine alizokamilisha miaka 27



Berna, Flower la Venture ndani ya gereza la Mandela



Manka ndani ya Gereza alilofungwa Madiba




Mlango mkuu wa kutokea ukiwa umeachiwa huru, na picha ya gereza kwa nje kama linavoonekana




Tour Guide aliekuwa akituhadithia yaliojiri, yeye alifungwa miaka 7 ndani ya gereza hilo. Mwanaharakati wa mapinduzi, ambae alibambikiwa kosa la ugaidi lakini hivi leo yuko huru na anatuelezea makaburu walivowatesa




Watalii mbali mbali tulioongozana nao, wakipiga picha gereza la Komandoo wa Afrika, COMRADE NELSON MADIBA MANDELA.

Miaka 27 gerezani, katoka akiwa hai na kawasamehe wote waliomtesa na kumfunga?????????

Mungu nisaidie niwe na roho ya hivo...eeehhhhhhhhh!!
Na hakutaka kufukuza wazungu kaamua taifa liwe la amani kwani binadamu wote ni sawa, Wazungu na weusi wote ni sawa hapa Afrika ya Kusini na hii yote ni kwasababu ya Mandela...we love you tata Madiba



Berna na Manka nje ya gereza
 
Hapa hata sijaelewa kitu kama vp jaribu kuweke sawa mwana!
 
it is good to have vacation like this, wakirudi waende mkumi au serengeti watangaze na utalii wa ndani
 
2namshauri dada yetu hana uwezo wa kutumia pesa kijinga asije akayavaa makubwa awe makini, ni kijana mdogo sana anahitaji kutulia...hayo mambo ya akina britney spears wenzao wana mabilioni na mabilioni...yeye hata m 100 kwenye account hana, afu anatuzingua hapa na mambo eti ya edgers, nani asiyepajua cape town bwana mpaka picha kibaoooo.nawewe pia hapo juuu usimsemee.mwambie ajibu yeye.pumbav
 
mbona wabongo mnakuwa hampendi wanayofanya wenzenu,kwanini hamuwaelezi wageni wanaokuja kutalii kwetu wasiweke pesa zao badala ya kuja huku nyie mnawaona jide na Gardner tu?acheni wivu,je kwa mimi ambaye niliamua kwenda vacation makkah mtasemaje?
 
mimi ni mkristo lakini sasa hivi nipo makkah kwa mapumziko mafupi,mtasema vipi?
 
usulebritee bongo kaaazi kweli kweli gggggggggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrrhhhhhhhhhh!!!!
 
ningeona wamuhim sana angepiga picha ngorongoro au serengeti ambazo ni maarufu duniani na zingeisaidia TZ kuliko hiyo robbin island,kwi kwi kwi kwi..afu anavaaaaa manguo ya SA

PUUUUMBAAAVVVVVVVV
 
usulebritee bongo kaaazi kweli kweli gggggggggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrrhhhhhhhhhh!!!!

🙂,mi ni hapo tu,mengineyo sitiii neno,kwani kila mtu na maisha yake bwana,hata ka akikamua mahela yake yoooote,sidhani ka kesha wahi kwenda kumgongea SEMANYA ,,,ngo ngo ngo!!!!!,"Baba nsaidie tu utumbo twa kuku ili nirumangie na ka ugali kangu ka muhogo",,,,Jamani wazee life is too short bana,kamua leoleo,ukichelewa watakuja zichoma ndugu zako au wajinga wajinga wengine tu.
 
Last edited:
Mawazo ya kijamaa!! Sasa kazi ya TTB na Wizara ya Utalii na Maliasili ni nini?
 
mwacheni mwenzenu atoe tongotongo. Kwani kinauma nini ilhali anatumia hela yake. Tangu nimesikia dada huyu akiimba kwa takribani miaka kumi sasa, hii ndiyo mara ya kwanaza kumsikia akienda vacation wakati watu wengine huenda kila mwaka. Tatizo lake ni kujitangaza kuwa yuko wapi; angeenda kimya kimya na kujirudia kimya kimya kama wengine tunavyofanya, ni dhahiri hizi kelele zote tusingezisikia. Nina imani kuwa huko hatotumia zaidi ya $4000 ambazo ni sawa na shilingi milioni nne tu za kitanzania; kelele za nini sasa.
 

Tatizo Michuzi ndiye aliyeanzisha haka kamchezo ka kujitangaza tangaza kila mara anapotaka nje ya nchi.Sasa na wengine wameanza kuiga....kazi kwelikweli!!!
 
the angle should be every Tanzanian for example one from tandahimba, Mkuranga, Mwakaleli should have enough cash from the national cofers or from their efforts to enable them be tourists. Je unaweza amini kuwa kuna watanzania hawajawahi kuona twiga pamoja na kuwa entrance fee mbugani Mikumi ni shs 1,000/=.

Kwanza hana nauli ya kutoka mkuranga kwenda mikumi na kama anayo basi ina kazi ya michango ya mwenge , madawati, kumkaribisha DC, dawa ya watoto ( alu ay duo cotexin) ambayo dozi ni shs 10,000/=.

vile vile maisha yake yote anajaribu kubalance maisha hawezi kufikiria kupumzika, mtanzania wa kweli kupumzika kwake ni kifo na sio kwenda vacatation. Vacation wanaenda watanzania elites,, politicians na first class citizens.wengine vacation ni heaven au hell kutegemeana na jinsi walivyoishi.
 
mmh....hizi mambo sijazielewa wajameni.......
 
Mimi sioni kosa la jayde na mume wake kwenda kutembea, yupo likozi ameamua kupumzika sisi inatuhusua nini? na hizo picha amewawekea wapenzi wa blog yake ambao wamekuwa wanamuomba awawekee picha zaidi. na kama wewe hutaki kujua anafanya nini usiende kwenye blog yake kuangalia,
na kuna mtu kasema kwa nini asivae nguo yenye bendera ya Tanzania , kama ulianagalia vizuri wakati anaenda alivaa scafu iliyokuwa ni bendera ya Tanzania, kutoka airport mpaka huko alikoenda. sas aavae hiyo kila siku kwa ni haifuliwwi.
Halafu swala la mtot hayo ni mapenzi ya Mungu, nadhani hakuna mwanamke ambaye hataki kuwa na mtoto kila mtu anatamani, siku yake ikifika Mungu atampa sisi siyo tunaotoa watoto mpaka uulize kwa nini hazai? Mungu hachelewi wala hawahi siku yake bado na yeye ataitwa Mama.
Kuhusu kupiga picha samaki wa Tanzania nenda kwenye blog yake kwenye kumbukumbu utaona mara nyingi amepiga picha samaki wa ferry, na kule msasani baharini yuko kwa wavuvi ananunua samaki amewapiga picha.
 
some pipo bwana, yaani mtu anatafuta pesa kwa jasho lake mtake kumfundisha jinc ya kuzitumia kama vile mwamsaidia kuzitafuta, aitangaze serengeti my foot, kama nyie mlishawahi kutangaza vile, majungu/wivu kitu kibaya! na huyo alieuliza kama ana mtoto inahusu? mbona watu mnafatilia maisha ya watu kiac hicho...khaaa mnakera sana! jalini yenu wajameni.
 


Mimi nakubaliana na akina Gadner kwa chochote wanachokifanya au walichofanya kuanzia kuzaa mpaka matumizi ya hela zao.

ILA tu....


Kama wangevaa fulana yenye bendera ya Tanzania pale au yenye Mount Kilimanjaro au Mbuga ya Serengeti.... hapo walipotembelea gereza, wangesaidia kutangaza TZ.......Uzalendo.

Ningewafagilia zaidi.

Mambo yao mengine personal
 
Kama mtu huna hobby ya kutalii stop critisizing others. You just better shut and keep it to yourself that if it is me I won't travel. When you are in Cape Town, Roben Island and Boats tour is something you wouldn't like to miss. if you have never been there you may surely critisize. Wazungu wakifanya mnaona sawa, wabantu tukifanya tunatumia fedha vibaya.. lazima ujithamini mwenyewe ndio watu wakuthamini. Jipe thamani Semenya.
 

Wajameni, naona kama tunaingilia privacy ya watu kwa kiasi kikubwa mno... Namuomba PDiddy a "wrap-up" hii mada for the interest of our sister and brother.

Its painful to read some of the comments made
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…