Jide na Gadner, sasa ivi kama paka na panya

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Pamoja na kutumia nguvu nyingi kukanusha kwenye mitandao kwamba ndoa yao haijavunjika, mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ' G . Habash ' na ' mtalaka' wake, Judith Wambura Mbibo ' Jide ' , Jumamosi iliyopita walifanya tukio lililowashangaza watu kufuatia kila mmoja kuingia ukumbini akiwa na kampani yake na kukwepana kama paka na panya.

Amani liliwanasa kwa vile lilikuwepo.

Mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ‘G . Habash' akiwa na Miss Mara 2000, Rashida Wanjara.

Tukio hilo lililoamsha minong ' ono kwa watu waliosoma mchezo mzima, liliibukia ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge ( zamani Business Park) uliopo Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uzinduzi wa albamu ya Bongo Fleva.

WALIVYOKAA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Gardner alipoingia alikwenda kukaa kwenye meza na watu wengine watatu, baadaye akafika Miss Mara 2000, Rashida Wanjara na kuunga ambapo walikuwa wakibadilishana mawazo na kufunguliana vinywaji kwa meno na kumiminiana kwenye glasi.

JIDE NAYE
Wakati Gardner ambaye pia hujulikana kwa jina la utani la Kapteni akiendelea kujipoza na Rashida na wengine, Jide yeye alikaa meza moja na kijana mmoja aliyevalia shati la kitenge la mtindo uliowahi kutamba miaka mitano nyuma, wengine huita Mackezie sanjari na wadada wawili.

WALICHOTAKA WATU
Baadhi ya watu walisikika wakishauri kwa sauti ushauri ambao haukuwafikia wawili hao ambapo walisema kama kweli ndoa hiyo haijavunjika, ni vyema Jide angeenda kwenye meza aliyokaa Gardner na kusema chochote kisha kuondoka hali ambayo hakuwepo.

PAKA NA PANYA
Mtu mmoja aliyekuwa amehudhuria shughuli hiyo na mkewe, alimuita paparazi wetu na kumuuliza: "Kwani, Jide na Gardner sasa ni paka na panya?"
Mwandishi: "Kivipi?"
Mtu: "Namwona Jide yuko na kampani yake, Gardner naye na kampani yake kule. Unajua paka na panya ni vigumu kukutana.
Hawa kweli hawapo sawasawa," alisema mtu huyo alijitambulisha kwa jina la Yahya.

Akaendelea : "Unajua ninavyojua mimi, Gardner ni kijana mpole sana, mwenye upendo, ila Jide ni mkali.
Halafu kwa sababu yeye Jide ana pesa naamini alitaka kumpandia kichwani mumewe wakati anajua yeye ni kichwa cha nyumba. Pesa na ndoa mambo mawili tofauti."

WAWINDWA NA KAMERA
Muda mwingi paparazi wetu aliwavizia Gardner na Rashida na kufanikiwa kuwafotoa picha kadhaa lakini kimbembe kilikuwa kwa Jide ambaye alionekana kuwa makini na kukwepa kamera ya paparazi wetu mara kadhaa huku akionekana kuwa na hasira na kuna muda meza yake iliparaganyika baada ya mwanga wa kamera kuwamulika yeye na kampani yake.

ANGALIA HII
Katika hali iliyodhihirisha wawili hao hawako sawasawa, muda fulani Gardner aliinuka na kuelekea upande aliokaa Jide ambapo mwanamuziki huyo naye alionekana kama kutaka kukimbia na kumfanya Gardner kubadili mwelekeo wa safari yake.

KUNA HII PIA
Mmoja wa mashuhuda aliyekuwa ukumbini hapo naye alimwambia paparazi wetu kuwa, aliwaona wawili hao wakikwepana baada ya kukutana kwenye njia ya kuelekea maliwatoni.

GARDNER AZUNGUMZA NA AMANI
Juzi Amani lilimtafuta Gardner kwa njia ya simu na kumuuliza ni kwanini yeye na Jide kila mmoja aliingia ukumbini na kampani yake. Gardner: "Kaka , yeye ( Jide ) alikwenda pale kumpa tafu yule aliyekuwa akizindua albamu yake pale.

Sasa isingekuwa rahisi tugandane pamoja kila wakati.

Lakini hayo unayoniambia ni madai tu.
 
Attachments

  • 1411015899698.jpg
    37.8 KB · Views: 1,993
Wanaogopa kuachana au hawataki watu wajue kuwa wameachana?wanaficha nini.
 
Wanaogopa kuachana au hawataki watu wajue kuwa wameachana?wanaficha nini.

Naona wametengana kwa mda, hawa hawawezi kuachana wewe, wamezoeana mno halafu walikuwa wanaishi kama mapacha na marafiki, yani walikuwa wanaishi maisha zaidi ya ndoa, ni vigumu sana kuachana
 
Huyo Rashida si alikua anatoka na Prof ndio maana alikuwepo

kwenye uzinduzi huo....., Jide n G ni kweli kila mtu alikuwa busy

kivyake
 
Naona wametengana kwa mda, hawa hawawezi kuachana wewe, wamezoeana mno halafu walikuwa wanaishi kama mapacha na marafiki, yani walikuwa wanaishi maisha zaidi ya ndoa, ni vigumu sana kuachana

hahaaaaa binam eti walikua wanaishi kama mapacha LOL
maisha zaidi ya ndoa LOL
 
hahaaaaa binam eti walikua wanaishi kama mapacha LOL
maisha zaidi ya ndoa LOL

Ndio binamu, unajua kuna wana ndoa wengine wapo serious mno hawana hata mazoea, mtu unakuta umeoa/olewa zaidi ya miaka mitatu ila bado mnaogopana maana sio kusema mnaheshimiana, sasa ile mbaya mno hata mkiachana hamkumbukani, jide nadhan atakuwa kammiss sana gadner hata gadner pia.

Jide na gadner hawaishi kama wanandoa bali marafiki walioshibana, wanashirikiana kwa kila kitu kama washkaji, nilikuwa nawaona pale nyumbani lounge kama mtu huwajui waweza kusema sio wana ndoa, wapo charming mno wanajiachia hadi raha
 
Binamu unavyowaongelea hawa watu kwa ukaribu.......

Ila wasiachane maana zilikuwa zikiongelewa ndoa za macelebrities hii nayo ilikuwa top
They used to look Good together.. Jide ndio kakomaa hataki kubeba mizigo tena
 
Jide hatakagi ujinga yule, ila jamaa hanaga shida kabisa ni mpole mno sema kwa kupenda papuchi sasa ajambo

Naona jide siku izi yupo na wancy model, wanapendana na wenyewe maana watu waliwachamba sana pale nyumbani lounge ila bado wenyew wanapendana kama mtu na dada yake
 
Binamu unavyowaongelea hawa watu kwa ukaribu.......

Ila wasiachane maana zilikuwa zikiongelewa ndoa za macelebrities hii nayo ilikuwa top
They used to look Good together.. Jide ndio kakomaa hataki kubeba mizigo tena

anajishaua na yeye wakat kwa gadner kafa kaoza, ngoja asikie kaoa atakavyokuja juu mkurya yule.
 
mi ningemshauri jide arudiane na G. tu. ni mwanaume mvumilivu na busara sana, tangu amekuwa na jide amevumilia kashfa na majina kibao alioitwa na watu.
hata kama anadhan ana hela kumzidi but G hashindwi kuishi coz ana kazi nzuri na kipaji cha umc kingemtoa tu.
jide kwa hali aliyonayo hawez kuishi mwenyewe na mwanaume mwenye busara kama G sijui atamtoa wapi. atafakari kwa kina wote wanamapungufu tu
 
Hata Diary iliyopita JD alionekana na Wakazi na Jamaa zake wengine wakati wanapanga nyumba Mpya ! ...by the way NDOA ngumu haijalishi wewe Supastaa, celebriti au Raia wa kawaida hii kitu Ngumu Inahitaji uwepo wa Mungu sana aisee!
 
Ila gpl ni wamekaa kichokono chokono kisa jide aliwapa ukweli wake,unajua sometimz mtu unahiaji kupumzisha akili kwa kile kilichotokea,wakimaliza matatz yao watakua pmj so kwa kufosiwa na social media,hawez kumfurahisha shetan huku kiti anakonda mwacheni raha ajipe mwnyw.
 
Huyo Rashida si alikua anatoka na Prof ndio maana alikuwepo

kwenye uzinduzi huo....., Jide n G ni kweli kila mtu alikuwa busy

kivyake

Rashida Wanjara ft Prof Jize Heavy weight Mc Vina Vikali Usipime ft Gadner ni Sheedaaaa!
 
Hata Diary iliyopita JD alionekana na Wakazi na Jamaa zake wengine wakati wanapanga nyumba Mpya ! ...by the way NDOA ngumu haijalishi wewe Supastaa, celebriti au Raia wa kawaida hii kitu Ngumu Inahitaji uwepo wa Mungu sana aisee!

Jide anapanga nyumba mpya au nani??
 
Huyo Rashida si alikua anatoka na Prof ndio maana alikuwepo

kwenye uzinduzi huo....., Jide n G ni kweli kila mtu alikuwa busy

kivyake

KWa hiyo wanjara alienda kum support x wake?? Mmh na usikute bado wanaminyana hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…