Jifanye Mjinga Unufaike

Jifanye Mjinga Unufaike

Gordian Anduru

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2021
Posts
369
Reaction score
747
Kuna huyu Dogo ambaye ukimwekea Noti ya shilingi elfu kumi na Sarafu ya shilingi mia tano yeye anachagua ile sarafu ya mia tano anaacha ile noti ya elfu kumi.

Dogo aliwashangaza watu wengi na kila ikitokea mtu haamini jambo lile basi yule dogo anaitwa na vile vile anachagua mia tano.


Siku moja jamaa kamkuta dogo ndo katoka kuchukua mia tano yake sehemu kanunua zake ice cream anakula, akamuuliza "Dogo kwanini kila siku unachagua mia tano?"

Dogo akajibu "Siku nikichagua noti ya Elfu kumi itakuwa ndo mchezo umeisha! Hakuna atayeniita tena"
 
Huyo dogo kaiba falsafa yangu!! miaka km 20 hivi, ilo pita hata mie ndo zilikuwaga zangu hizo!! lkn sikusemaga km yeye!
 
Usijaribu huu mchezo kwa Karne hii/kizazi hichi...watoto wanajua value ya pesa balaaa
 
Back
Top Bottom